Unknown Unknown Author
Title: ANZA BIASHARA YAKO HATA PASIPO MTAJI WA PESA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  Habari rafiki na mwanamafanikio mafanikio kupita mtando huu wa Ufunguo wa mafanikio,Nitumaini langu u mzima wa afya njema kama ilivo kwang...

  Habari rafiki na mwanamafanikio mafanikio kupita mtando huu wa Ufunguo wa mafanikio,Nitumaini langu u mzima wa afya njema kama ilivo kwangu.

  Rafiki ni siku nyingine nzuri sana kwetu kama wapambanaji katika kuufanya mwaka 2017 kuwa wa mafanikio makubwa zaidi kwetu.
   Rafiki umesha kuwa wimbo na nikikwazo kikubwa  cha watu wengi kuto anza biashara kwa sababu tu wamekosa mtaji au kianzio cha biashara zao.

Rafiki hii inatokana na uvivu ulio jijenga ndani yetu wenywe na kufikili vikubwa wakati wote hasa tunapo kuwa na mawazo ya kuanza biashara zetu wenyewe,Rafiki watu wengi wanaamini kukosa pesa au kianzio basi hawawezi kuanza biashara au kuamini kuanza biashara lazima uwe na pesa Rafiki si kweli ila ni uvivu tunao upalilia ndani yetu.
  
   Tumia njia zifuatazo zitakazo kusaidia kuanza biashara yako mwenyewe kwa kuanza na 0 kisha kuwa nacho.

  1.Tumia kipaji chako,
Rafiki kipaji nikitu cha thamani sana kwako na hakuna mtu ambae amezaliwa bila kipaji ila shida inakuwa ni mtu kutambua kipaji chake na anakitumiaje ili kimwingizie kipato.
  Mfano 1.Unakipaji cha kuchekesha,Jambo la kwanza unalo takiwa kulifanya onyesha kipaji hicho watu wajue kisha ukisha fahamika utaanza kutengeza pesa kupitia majukwa ya uchekeshaji.
  Mfano 2.Unakipaji cha uchoraji,Tumia muda mwingi kuhakikisha unakuwa bora zaidi kwa kujifunza kisha onyesha uwezo watu wajue kisha utatengeza kipato kupitia Uchoraji wa michoro mbalimbali Eg,Majengo,Picha za watu,Maandishi na nyingine nyingi.
   Mfano 3.Unakipaji cha uimbaji,Jambo la kwanza fanya jamii yako ijue nafasi ya kipaji chako,Onyesha uimbaji wako wenye utofauti,Jifunze zaidi baada ya mda fulani utatengeza kipato kupitia jukwaa za wasanii kwa kuimba au kuigiza.
      Kitu cha kuzingatia onyesha kipaji chako kwa utofauti na ubora kisha jipe thamani na muda utafanikiwa.

   2,Tumia muda wako,
Rafiki kunawatu wao siku zote hawana mtaji na hawana kazi wala mawazo ya kufanya kazi zitakazo wapa mtaji wengi hufikilia aibu ya kufanya vitu vidogo,
  Rafiki muda wako unaweza kuupa thamani kwa kutoa elimu Fulani kwa watu itakayo kuwa suluhisho la matatizo yao mfano Jifunze magonjwa kisha toa elimu kwa watu bila shaka watakuuliza tiba kisha utawatafutia tiba hata kwa mtu mwingine anakupa dawa nawe unawapelekea kwa bei ya faida.

  3.Tumia watu wanao kuzunguka,
Rafiki hapo itatemea aina ya watu ulio nao ndo maana unashauriwa siku zote kuwa na ushirikiano na watu chanya kwako Mfano unamtu unae mfaham anafanya biasha  unaweza kuwa sehem ya kutengeza masoko la biashara yake kwa kamisheni yaani mtu anauza mchele debe 25500 wewe unatafuta soko la shilingi 26000 ambapo faida yako itakiwa sh 500 kwa debe na ukifanikiwa kutengeza soko la watu kumi wanunuzi na kumi  wauzaji unaweza kutengeneza faida tsh 10000 kila siku.

4.Tumia Maarifa uliyo nayo.
Rafiki unaweza kuwa na Maarifa ya kutengeneza kitu Fulani au Elimu ya ujasilia mali ambayo unaweza ukawa unaitoa kwa jamii yako kwa malipo,
Unaweza ukawa na Maarifa pia ya kutengeneza vitu vya asili ambapo baada ya hapo utavitafutia soko kisha unapata mtaji,Au ukatoa masomo ya ziada kwa malipo yaani (Tuition),Ukaanzisha masomo ya kuwapa Maarifa watu wengine kwa malipo ambapo unaweza kutoa semina za ufugaji,kilimo,Biashara n.k

  5.Tumia nguvu;
Mfano unaweza kuwa na lengo la kupata  pesa kiasi fulan kisha unaweza kutafuta kazi utakayo fanya kwa kutumia nguvu yako kisha ukalipwa,Hata inapo tokea pesa hiyo huwezi kuipata kwa mala moja fanya makusanyo au malimbikizo ya pesa hiyo baada ya mda utafikia lengo lako.

  Rafiki jua kila kitu kinawezekana ikiwa utaamini kuwezekana kwa kitu unacho kihitaji kabla hujaanza mchakato,Ikiwa utajipa matokeo yakuto weza basi niwazi haitawezekana kwa sababu umesha ruhusu hali ya kushindwa.

Tuma neno BIG KEY OF SUCCESSFUL 2017 kwenda 0715222989/Email:errynine6@gmail.com
Uunganishe na group la WhatsApp kwa mafunzo zaidi BURE.
Pia unaweza kulike page yatu ya Facebook_Ufunguo wa Mafanikio
Karibu sana

   Wako rafiki katika mafanikio
Ernest Lwilla

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top