Habari rafiki na msomaji wa makala kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa mafanikio nitumaini langu ni mzima wa afya njema kama ilivo kwangu,
Rafiki ni siku nyingine tena nzuri sana kwako mwana mafanikio mwenzangu tuitumia vizuri kwa matokeo chanya ya kesho,
Rafiki unatakiwa kuya jua na kwendana vizuri na mabadiliko makubwa ya Nchi yanapo tokea kama fursa ya pekee kwako kutengeneza kipato chako
#Unapo sikia hali ngumu ya kifedha nchini hali hiyo itumie kama fursa kwako kwa kufanya vitu ambavyo vitakutengezea kipato wakati umati mkubwa ukilalamikia hali hiyo,
Rafiki unaweza kuanzisha biashara ndogo ndogo za kilimo ambazo muda wako wote utatumia kuendesha shughuli hiyo wakati wengine wakitumia muda huo kukaa vijiweni na kulalamika,
Rafiki mwisho wa siku utavuna na kuwauzia bidhaa zako walalamikaji hao hao jambo la msingi ni kuangalia kitu kitakacho hitajika katika jamii yako mfano Mboga mboga,Nyanya,Mazao yote ya muda mfupi Eg Mahindi nk,
#Rafiki unapo sikia uhaba wa chakula Nchini ni fursa kwako mwanamafanikio mwenzangu ambapo unaweza kutumia pesa yako kununua mahitaji muhimu ambayo baada ya mda mfupi yata panda ghalana na kupatikana kwa nadra mfano,Mahindi,Maharage,Mpunga,Mtama wa ugali nk ambapo utanunua kwa bei iliyopo sokoni na kuhifadhi baada ya mda mfupi utayauza kwa ghalama ya faida zaidi,Pia unaweza kusafilisha toka mkoa mazao yanapo patikana kwa urahisi unapeleka mkoa mwingine ambapo mazao hayo yanapatikana kwa shida na bei kubwa.
# Rafiki mabadiliko ya Teknolojia ni fursa nzuri kwako ya kuongeza kipato chako unacho takiwa kufahamu ni kitu gani kimebadilika mfano Miaka iliyopita shughuri zote za kifedha zilikuwa ni kwa Bank lakini ulimwengu wa sasa shughuli nyingi za kifedha zinafanyika kwenye Simu hapa tunazungumzia M_Pesa,Tigo_Pesa na zingine nyingi ambapo wewe waweza kutumia mabadiliko hayo kama fursa kwako
#Rafiki wakati vijana wengi wenye elimu zao za vyeti vya chuo kikuu wamejazana mjini kutafuta nafasi za ajila mwanamafaniko mwenzangu rudi kijijini tumia muda wako kuwekeza katika kilimo kisha weka plani yako nzuri ya mda fulani ambapo utavuna na kurudi mjini kuwakuta wasomi hao wakiwa bado wanasubili ajila nawe utawaajili licha yakuto kuwa na elimu.
Rafiki hapa naomba uelewe zaidi kwamba vijana wengi tumelundikana mjini tunakidai tunatafuta maisha wakati tumeyaacha mabilion ya Pesa yaliyo katika kilimo kijijini tatizo kubwa tunataka vya mtelemko.
Mwisho ukiwa kama rafiki na mwanamafanikio mwenza siku zote za maisha yako penda kuwa chanya zaidi kifikra pamoja na maamuzi sahihi,Tumia muda wako kufikili kitu gani kitaongeza pato lako hata kama nikidogo sana kwani mafanikio makubwa ni matokeo ya mafanikio mengi madogo madogo.
Tuma ujumbe mfupi BIG KEY OF SUCCESSFULL 2017 kwenda 0715222989/Email. errynine6@gmail.com
Uunganishe na group la WhatsApp kwa kujifunza zaidi.
Nikutakie siku njema na yenye mafanikio kwako
Wako rafiki katika mafanikio
Ernest Lwilla
Chapisha Maoni