Unknown Unknown Author
Title: FAIDA ZA KUFANYA VITU TUNAVYO VIPENDA NDANI YETU.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitia mtandao juu wa Ufunguo wa mafanikio,Nitumaini langu ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwa...

  Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitia mtandao juu wa Ufunguo wa mafanikio,Nitumaini langu ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu.
  Ni siku nyingine nzuri sana kwetu sote na kwenda kuweka juhudi kubwa kwenye vitu tunavyo vipenda na kuamua kuvifanya vitakavyo badilisha hali yetu ya maisha ya sasa.

    Ni muhimu zaidi kujisikiliza na kujua nafsi zetu zinapenda nini na hivyo ndo tuvifanye kwa nguvu na Maarifa yetu kuhakikisha tunafikia mafanikio yetu,
   Rafiki kunafaida kubwa na nyingi sana za kufanya machaguo yetu nafsi zetu,Rafiki Ebu jitathimini unajisikiaje pale unapo fanya unacho penda? Na vipi pia unapo fanya kitu unacho kichukia au usicho kipenda ila unafanya kwa faida fulani bila shaka utagundua unapo fanya unacho kipenda unajisikia vizuri zaidi.

   Zifuatazo ni baadi ya faida za kufanya vitu tunavyo vipenda katika nafsi nzetu.

1:Unakuwa huru na unacho kifanya,
Kufanya kitu unacho kipenda kunakupa Uhuru mkubwa na kupata raha zaidi pindi unapo kifanya kitu hicho kwa ubora zaidi,Na kukipa nafasi kubwa na muda wa kutosha kwani ndicho unacho kipenda zaidi.
 
   2.Unayafurahia matokeo:
Kutokana na kufanya unacho kipenda kunapelekea kuyapokea vizuri matokeo ya aina yoyote (Mazuri/Mabaya)na yote kuona ni sehemu ya mafanikio ya unacho kipenda kwani yanapo kuwa mazuri ni bora na yanapo kuwa mabaya ni bora zaidi kwa sababu unakiwa umejifunza kwa undani unacho kifanya na kupata uzoefu mala dufu ya jana.

    3.Unakifanya kwa ubunifu zaidi:
Mfano kwa watu walio ajiliwa mala nyingi wanafanya vitu si kwa ubunifu wao ila ni kwa ubunifu wa yule alie waajili kwani yule ndo alie kichagua na kukiongezea ubunifu ili kizidi kutoa matokeo makubwa zaidi kwake,Ila kwa alie ajiliwa anakuwa amekifumbia macho anacho kipenda na kuganya unacho kipenda BOSS.

   4.Unajipa muda wa kutosha kujifunza na kukijua kwa undani.
Siku zote unapo fanya unacho kipenda unakuwa unaifurahia kila hatua ya mafanikio ya kitu hicho,Nahivyo kujipa zaidi muda wa kujifunza zaidi ili ukijue kwa undani na nje wa kitu unacho kifanya na baadae kukupa mafanikio makubwa zaidi.

   5,Utazifurahia changamoto.
Ikiwa unafanya unacho kipenda siku zote utazifurahia changamoto pasipo kukata tamaa ya kuendelea kukifanya kwa ubora zaidi kwa kuziona zile changamoto kama sehem ya mafanikio na kujifunza zaidi unacho kifanya na baada ya mda kitakupa mafanikio makubwa zaidi kwasababu tu unakipenda.

Mwisho nakupa ushauri wa kuisikiliza na kuiuliza nafsi yako je unacho kifanya unakipenda au kukifurahia?
Na kama hukifurahii tafadhali changua kujenga msingi wa kitu utakacho kifurahoa zaidi katika kukifanya kwako.

  Nikutakie siku njema na yenye mafanikio zaidi.

Tuma neno BIG KEY OF SUCVESSFULL 2017 kwenda 0715222989/Email:errynine6@gmail.com
Uunganishe na group la WhatsApp kwa kujifunza zaidi BURE
Pia unaweza kulike page yetu Facebook Ufunguo wa mafanikio kwa makala zaidi.

FANYA UNACHO KIPENDA UNAKIFURAHIA NA KUFANIKIWA ZAIDI.
Karibu

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top