Habari rafiki na mwana mafanikio mwenzangu kupitia mtandao huu wa Errynine Tz,
Nimatumaini yangu nimzima wa afya njema huku ukizidi kuboresha kipato chako kwa kujiwekea malengo makubwa zaidi.
Rafiki iliufikie mafanikio yako nivizuri kujiwekea Malengo lakini ili ufanikiwe kwa sehemu kubwa zaidi katika maisha yako nivema zaidi kuweka malengo makubwa zaidi.
Rafiki ikiwa utapanga malengo makubwa zaidi kunafaida nyingi sana utakazo zipata,
Zifuatazo ni baadhi ya faida kati ya zilizo nyingi zaidi utakazo zipata ikiwa utajiwekea malengo makubwa zaidi.
1.Malengo makubwa yatakuwekea nidhamu/mipaka ya matumizi yako,
Rafiki mtu yeyote asiye kuwa na malengo 80% ya pesa anayo pata matumizi yake niya hovyo hovyo daima na hapo hutumia asilimia chache sana kuwekeza,
Wakati huo huo mtu mwenye malengo makubwa 80% ya pesa yoyote anayo ipata hutumia zaidi kuwekeza ili atimize malengo yako kwa wakati sahihi.
2.Malengo makubwa yatakufanya uwe mbunifu zaidi kwenye biashara yako.
Ndiyo,Malengo makubwa yanaongeza ubunifu mdogo mdogo ambao utaboresha biashara yako ili kuwa na wateja wengi zaidi watakao ongeza kipato chako hatimae kufikia malengo uliyo jiwekea.
3.Malengo makubwa yatakufanya uongeze juhudi zaidi katika biashara yako,
Mfano wewe nimvivu wa kupindukia,unapenda kuzunguka zunguka,Muda wote unapenda kuangalia filamu n.k
Rafiki malengo makubwa yatakufanya kuacha mambo yote yasiyo yamsingi katika biashara yako,Malengo makubwa yatakufanya muda wote uwepo kwenye biashara yako.
Nahivyo kuboresha zaidi kipato chako.
4.Malengo makubwa yatakuongezea marafiki chanya zaidi kwenye biashara yako.
Rafiki malengo makubwa yatakufanya uwe karibu zaidi na watu wanafikili mambo makubwa hata zaidi ya uwezo wao kwani kupitia picha sahihi ya malengo yako itakuepusha na watu wote wosio chanya kwako.
5.Malengo makubwa yatakufanya uwe mpambanaji zaidi unapo kutana na changamoto.
Rafiki malengo yako ndo yatakayo kupa hamasa zaidi ya kuendelea kufanya jambo hata unapo kutana na changamoto kubwa,Ndo maana kuna muda mwingine unakuwa unataka kukata tamaa lakini utakapo tizama malengo yako yatakufanya usalie ukipambana na changamo mpaka utakapo zishinda.
Mwisho Rafiki ni muhimu zaidi kuweka malengo makubwa hata inapo tokea hujayakamilisha utafika hatua ambayo usinge weza kuifikia kama usinge weka malengo.
Kwamfano malengo yako kwa mwaka yalikuwa lazim ununue uwanja na kuanza msingi lakini kutoka na sababu ambazo zinakuwa ni njee ya uwezo wako,Unafikia hatua ya kununua uwanja na kumwaga tofari hapo hatua itakayo fuaya itakuwa nikusimamisha msingi.
Rafiki nikusi sana kama bado hujapanga malengo yako bado nimapema sana ,kaa andika malengo kisha anza kupambana kuyakamilisha.
Nikutakie siku njema na yenye mafanikio zaidi kwako.
Tuma ujumbe mfupi BIG KEY OF SUCCESSFUL 2017 kwenda 0715222989/Email. errynine6@gmail.com
Uunganishe na group la WhatsApp kwa mafunzo zaidi.
Karibu.
Wako rafiki katika mafanikio
Ernest Lwilla
Chapisha Maoni