Habari rafiki yangu na msomaji wa makala hizi kupitia Errynine Tz nimatumaini yangu nimzima wa afya njema.
Nisiku nyingine tena tuliyo ipata na niwajibu wetu kwenda kuweka jitiada kubwa zaidi katika shughuli zetu za kila siku ambazo tunaamini ni sehemu sahihi kwa mafanikio yetu.
Rafiki yangu awali yayote nichukue nafasi hii kujitambulisha kwako naitwa Ernest N Lwilla mimi nikijana mwenye umri wa miaka 25 nimesha fanya shughuri nyingi sana.
Nimesha wai kufanya biashara ya Mazao kwa zaidi ya misimu miwili yaani nilikuwa na nunua Mpunga na Ufuta kiukweli biashara hizi hazikuwa na matokeo mazuri kwangu kama nilivo kuwa nikiambiwa na watu wanao fanya biashara hizo kuwa zinafaida kubwa na mala zote nilikuwa kiaanza biashara kwa hamasa kubwa sana lakini haikuwa vile kama nilivo tegemea HAKIKA MAFANIKIO SIO AJALI.
Rafiki mwanzoni mwamwaka 2013 nilianza rasmi mafunzo ya kuandaa Muziki yaani Producer hapo nilijifunza pamoja na kutengeza Video,Mwishoni mwamwaka huo huo Baba mzazi alinifungulia studio iliyo kuwa ikishughulika na Muziki & Video.
Nilianza kwa kasi kubwa nikishilikiana na mwalimu wangu lakini bado picha niliyo kuwa nayo wakati naanza ilipotezwa sana na changamoto zilizo kuwa nyingi kuliko mafanikio,Sikuwa na uvumilivu nikaamua kuuza vifaa nakisha kuendele na shughuri zingine za uzalishaji mali nikiwa bado nipo na Baba rafiki yangu kipenzi.
Wakati huo baba akiamini Mimi bado nimdogo na ninastili kuendelea kuwa mikononi mwake akihofia zaidi kunipoteza kwenye dimbwi lisilo sahihi kulingana na umri wangu.
FIKRA CHANYA zilianza baada ya kuanza kujishughulisha na vitu vidogo vidogo sana Nakumbuka mtaani kwetu palikuwa na kituo kidogo cha kuuza vinywaji yaani Depo ambapo nilikuwa na shusha vinywaji kila siku na kila nikishusha nilikuwa nalipwa Tsh 1000 au 1500, Baada ya mda kidogo kituo hicho kilipanua uwigo wa mauzo kwa Kuanza kusambaza na Bia ambapo awali nilikuwa nisoda pekee,Hakika ukawa fursa nakwangu pia kujiongezea kipato ambapo nilikuwa kila nikishusha Bia nalipwa 2000 hadi 3000 hapo ilitegemea idadi.
Hakika kipato kikaboreka zaidi nikaanza udalali wa simu kubwa yaani Smartphone ambapo nilikuwa nikinunua simu kwa Tsh 70,000 na ninauza kutokana na mteja wangu alivo kuja mala nyingi nilipata faida kwanzia 10000 hadi 15000 kwa mfano umekutana na mtu ambaye nimgeni na amesikiliza kelele za wengi juu ya Smartphone.
Hakika Baada ya muda mfupi nilikuwa napesa yakutosha sana lakini Baba yangu kipenzi nafasi yake ilikuwa pale pale,Ikatokea bahati zuri Kunampangaji wa Mama nilie kuwa namshushia vinywa ameshindwa ofisi yake ya Kufua na kunyosha Nguo yaani DOBI nami ikawa ni Fulsa nzuri kwangu nikakinunua kile chumba kwa 300,000 lakini nikiwa nadharau kubwa sana juu ya shughuli aliyo kuwa akiifanya ofisini hapo.
Nilijipa maswali ya kipuuzi tu Ivi ntaweza kufanya kazi ya kufua,Watu watanichuliaje,Nakumbeka nilianza kwa kumtafuta binti wa kazi ambaye nilidumu nae kwa mwezi moja yaani kwanzia 4/2014 hadi mwezi wa tano,Kwa kipindi nilicho kuwa na mfanya kazi wangu Ofisi iliniingizia Tsh 210,000 Haaa eti nami nikaanza kukamata mkwanja mrefumrefu.
Siku chache baada ya kumlipa posho yake yule binti aliniomba kuacha kazi Nadhani nikwa sababu zile zile nizo jipa mimi nikamruhusu wakati huo bado naendelea kushusha vinywaji na biashara yangu ya simu ikiwa inaendelea.
Nikaona sio mbaya nikamruhusu yule binti akaondoka nikachukua nafasi ile pasipo kuzingatia maswali ya kijinga niliyo jipa mwanzoni yote nikwasababu tu nilikuwa nimegundua siri ya biashara hiyo,Nikaendelea mwenyewe mwezi nilio anza kusimamia mimi mauzo yalipanda hadi kufikia 300,000 hapo nimekula nimelipa kodi ya chumba na mengine mengi.
Hapo nilianza nami kupanua uwingo wa kipato changu nikawa pale pale ofisini nweka na nguo za mitumba
Hakika biashara ilienda vizuri
Nkawa nawateja wengi sana.
KELELE ZIKA TANDA
Mwaka 2015 mwezi wa 7 nilikutana nakelele tena nakunirudisha nyuma tena ambapo nilipata wazo jipya la biashara ya Samaki nakwamba inalipa sana yaani ni pasupasu,Nikalitendea kazi lile wazo cash nilikuwa kama na Tsh 1.2m ilipo fika mwezi wa 8 nikatafuta kijana akabaki ofisini nami nikanyanyua unyayo kuelekea mawindoni Ziwa Rukwa nilifika salama na shughuli zikaendelea baada ya siku chache sana Samaki waliaadimika sana kiasi Mvuvi alie kuwa akitoka na Samaki 2000 alitoka na Samaki 700 hapo ni kiwango cha juu nao niwale wanao vulia ndani sana wengine wote ilkuwa nikwanzia 150 hadi 200 mwisho.
Mfumo ulio tumika katika ununuzi wa Samaki ni ule wakumpa mvuvi pesa kisha aanze kukupa Samaki kwa kipindi hicho hali ilizidi kuwa ngumu sana kutokana na mgomo huo wasamaki nami nimesha wapa pesa zote wavuvi.
Rafiki nilisota na hali hiyo kwa zaidi ya mwezi na nikiwa kule polini hakukuwa na mawasiliano yoyote na hata unapo hitaji mawasiliano ilikubidi usafili kufata mawasiliano kumbuka wakati naenda huko siku mwaga Baba kwani nilijua atanizuia nami nataka nifanikiwe haraka.
Nilipo pata nafasi yakufata mawasiliano niliweza kuongea na Baba,Mama mwenye nyumba ambaye alinikumbusha juu ya pango la nyumba ofisini kuwa muda umeisha hivyo nahitaji kulipia MWANAUME NJIA PANDA hapo mfukoni nilikuwa nimebakiwa na Tsh 70,000 tu.
Nilifikili kwa muda nakumfata rafiki yangu ambae yeye ni mzoefu na ndiye nilie ongoza nae wakati wa kwenda Samaki nilizo kuwa nimesha pata niza shilingi 100,000 Hapo niliipa selikali ya kichwa changu kuchukua maamuzi magumu zaidi,Nilimwambia yule rafiki yangu juu ya maamuzi hayo kuwa Kesho naondoka alinisii sana niwe mvumilivu katika hali hiyo ngumu sikuweza kumwelewa hata sekunde Aliniuliza juu ya pesa nyingi nayo wadai wavuvi nilimwambia ACHANA NAYO nakama utaweza kuidai basi idai iwe yako.
Siku hiyo hiyo muda wa saa tisha hivi nikaanza safari yangu toka ziwani hadi kijiji jilani ambapo ilini chukua masaa 3 kufika hapo.
Saa 11 jua la mchechemo nilianza safari yakuto kijiji hapo kuelekea sehemu ambayo magari uwa yanaishia ambapo ilinichukua masaa 5,Ambapo niliingia saa 5 kasoro pale kijijini magari yanapo ishia,
Giza nene nami ni mgeni kwani wakati wa kwenda hatukupata hata muda wakuzunguka hata kido wakati huo huduma za simu zilikuwa tayari zinapatikana,Nilisongea usiku ule sehemu moja ambayo watu walikuwa wanaongea niliwasalimu,Nikajitambulisha vizuri nao wanikaribisha vizuri niliweza kuuliza magari kama yamesha fika wakaniambia tayari ila natakiwa kukata tiketi.
Niliomba sehemu ya kulala nikaonyeshwa sehemu ambayo si yakulipia lakini piah kunajoto la kutosha sana na hivyo sikuwa na haja ya kujifunika chochote,Nililala mpaka mda wa magari alfajil saa 10 nikamfata Kondakta wa Gari nikapata tiketi yangu safari ikaanza ilipofika saa 12 macho yangu yalianza kuona nchi iliyo kavu ya mwezi wa 9 mwishoni na hapo nikairuhuru selikali ya akili yangu kupanga mipango maalumu nikigika ofisini ambapo nilifika nikiwa na Tsh 50,000,Nilipokewa kwa furaha sana has a baba mzazi na majilani.
Rafiki siku iliyofata nilipokea simu toka kwa Mama mzazi akinipa taarifa juu ya Maafari ya ndogo wangu alie nifata halikuwa tatizo nikawatumia kama 30,000 nikaendelea kupambana ili nilipe Pango la nyumba ofisini na nilifanya ivo.
Mwaka huo huo nikiwa nashauku yakukamata pesa ndefu ilipo fika mwezi wa 10 nilikutana na Mwl mmoja ambaye awali alikuwa mteja wangu wa kufua na kunyosha hapo alinishirikisha mfumo mwingine wa biashara uliofahamika kama NETWORK MARKETING nilimwamini sana yule mwalimu sikuwa na maswali mengi kwake kulingana na Maelezo aliyo nipa + na ulewa wangu nikawa nimemwelewa sana.
Nacho kikumbuka zaidi katika Maelezo yake kulingana na mfumo wa biashara hii ilionekana kama Mafanikio nikitendo cha kulala na kuamka.
Siku chache alinipa mwaliko wa semina ambayo tulifanyia Hotelini (Mwankonde Hotel),Semina ilianza kwa video za hamasa kutoka kwa walimu, Kutokana na yale Maelezo niliyo pewa awali na mwenyeji wangu kwenye semina hiyo ya fursa mpya nilimaliza semina nikiwa kichwa kimepata moto mkubwa wa mafanikio yatakayo patikana kwenye biashara hiyo.
Kutokana na muda kwenda sana hatukweza kuongea chochote kuhusiana na semina hiyo siku iliyo fuata alinipigia simu ilikuwa nimwanzoni mwamwezi wa 11/2015 mazungumzo yalikuwa mazuri mno na hata nikampa ratiba ya mimi kujiunga na biashara hiyo kwanzia hapo hakukaa mbali na mimi muda wote alikuja ofisini kwangu na hata kuniulizia maendeleo ya mpango wangu.
Niliuza vitu vingi sana Lap top,Radio,Modem na vingine vingi nikiwa na uhakika wa mfumo mpya nilio tambulishwa kuwa utanilipa fasta sana.
Ilipo fika tar 23/11/2015 nilimtafuta mwalimu kumpa taarifa za kiwango cha pesa ambacho nimekipata alinitaka nikiweke kiwango hicho cha 600,000 kwenye M-Pesa siku iliyo fuata nikafanya malipo kwenye Kampuni na hapo tukapanda Gari wote na mwenyeji wangu kwenye biashara hiyo mpaka Mbeya mjini ambapo nilijaziwa fomu ya kujiunga na familia nzima ya wafanya biashara kupitia kampuni hiyo walinigurahia sana nakuniona mimi ni mpambanaji sana nami mwenyewe nilijihisi napaa kutokana na mapokeo hao.
Ongozi wa timu ulionyesha ushilikiano mkubwa kwa kipindi chote cha mimi kujifunza biashara hiyo na hata mtaani kwangu walinipokea vizuri sana ingawa ghalama ya bidhaa za kampuni hiyo ilikuwa ni ghalama sana kiasi watanzani kwa asilimia 60 hawamudu ghalama za Huduma hizo na hivyo ilihitaji elimu kubwa kwa mteja na ushawishi mkubwa,Nilipambana sana kwa wakati ule mapka nikamaliza deni la kampuni ambapo ilikuwa ni Tsh 1m,
Hapo mziki ukaanza nikawa peke yangu kuifanya biashara changamoto nazo zilikuwa nyingi sana yaani pesa iliyokuwa inatumika ninyingi kuliko faida iliyo patikana kwenye biasha hiyo,Biashara yangu ya dobi ilkuwa bado ikiniweka mjini kwa zaidi ya asilimia 99.99 ingawa mwanzoni niliidharau sana.
Ilipo fika tar 10/2016 niliacha rasmi biashara hiyo nakuendelea na biasha ya dobi kwa kipindi chote hicho nilikuwa nimejifunza mengi sana ,nimekutana na watu wengi sana,nimefanya semina nyingi sana na mengine mengi sana.
HAKIKA MAFANIKIO SIO AJALI.
Ungana nami kwenye sehemu ya pili ya makala hii HAKIKA MAFANIKIO SIO AJALI tujifunze sote.
Tuma ujumbe mfupi BIG KEY OF SUCCESSFUL 2017 kwenda 0715222989/Email:errynine6@gmail.com
Uunganishe na group la WhatsApp kwa mafunzo zaidi.
Wako rafiki katika HAKIKA MAFANIKIO SIO AJALI
Ernest Lwilla
Ahsante
Chapisha Maoni