Habari rafiki na msomaji wa makala hii kupitia mtandao huu wa Errynine Tz,Nitumaini langu ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu.
Rafiki nsiku nyingine tena ambayo tunatakiwa kwenda kupambana zaidi ili kuepuka kutegemea wahisani katika safari yetu ya mafanikio.
Rafiki imekuwa ni kawaida sana kwa Taifa,Taasisi binafsi,Mtu mmoja mmoja kuendesha maisha yake kwa msaada wa kutoka sehemu fulani,
Bila shaka umewai kuyasikia sana maneno haya Kwa hisani ya Vodacom,Kwa hisani ya Marekani ,Kwa hisani ya China na mengine mengi sana .
Rafiki Mungu alimuumba mwanadamu na akili akiwa na kusudi lake na kwamba mwadamu huyu atumie akili kuendesha maisha yake binafsi,Ingawa imekuwa nitofauti kidogo na watu wengi kutotumia uwezo huo badala yake wanawategemea watu wengine ili kuendesha maisha yao,
Rafiki yangu kuendesha maisha kwa kutegemea mtu fulani wakiwemo ndugu rafiki na jamaa kunahasala nyingi sana tofauti na Unapo kuwa muhisani mwenyewe wa maisha yako yaani Dreva wa maisha yako ni mwenyewe.
Rafiki mala ngapi umeahidiwa kitu na ndugu,rafiki na jamaa na baada ya mda mchache unajikuta umekwamishwa kwa kusubili msaada kutoka kwa mtu mwingine,Rafiki ni vizuri kujitegemea mwenyewe ambapo unapo panga jambo unakuwa na uhakika na hata inapo tokea umekwama unakuwa unatambua kitu gani kimekukwamisha .
Rafiki kuwa muhisani mwenyewe wa safari yako ya mafanikio yako mwenye kwani hauna sababu ya kumtegemea mtu nwingine kwani unakila sifa za kuto mtegea mtu kwani una
Akili,Nguvu,Muda,Watu,Maarifa n.k
Rafiki kama ni miongoni wa watu wanaotegemea msaada tafadhali badilika na ujitegemee mwenyewe kwani utakuwa na uhakika zaidi katika safari yako.
Mwisho kila jambo linawezekana ikiwa utaamua liwezekane kikubwa fanya maamuzi sahihi kwa faida ya uhakika wa safari yako.
Nikutakie siku njema na yenye mafanikio
Usisahau kutuma ujumbe mfupi BIG KEY OF SUCCESSFUL 2017 kwenda 0715222989/errynine6@gmail.com
Uunganishwe na group la WhatsApp kwa mafunzo zaidi.
Wako rafiki katika mafanikio
Ernest Lwilla
Chapisha Maoni