Habari rafiki na mwanamafanikio mwenzangu kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa Mafanikio ni tumaini langu ni mzima kama ilivyo kwangu,
Rafiki ni siku nyingine tena nzuri sana kwetu ambayo nimuhimu kuzitambua na kuzikwepa tabia ambazo zitakuwa kikwazo katika uchumi wetu ikiwa tutashindwa kuzjkwepa kwenye safari ya mafanikio.
Rafiki Tabia ni nguzo mama katika safari ya mafanikio uliyo nayo na hata unaoyo tegemea kuyapata yanategemea tabia yako.
Rafiki ni muhimu kutambua aina ya tabia ulizo nazo na kuona kama zitakusaidia kwenye safari yako ya mafanikio kwani tabia ni taa ya mafanikio yako, Watu wengi hukwamishwa kufikia mafanikio yao kutokana na baadhi ya tabia zao na kujikuta ndoto zao na maono yao yanakufa,
Rafiki tabia hizo ni hizi hizi ambazo unatakiwa kuwa makini nazo na kuzikwepa katika safari yako ya mafanikio,
Rafikifi tabia hizi nikama zifuatazo;
1.Uvivu,
Rafiki uvivu ni tabia ambayo usipo weza kuikwepa wakati wa ujana wako inakughalimu sana wakati wa uzee wako,Rafiki uvivu si lazima tu uwe ule wa kufanya mambo ila ni pamoja na kujiwekea tumalengo tudogo tudogo,uvivu wa kufikilia mambo makubwa,uvivu wa kutoboresha huduma yako na mengine mengi hii itapelekea kipato chako kuzidi kuwa kudogo siku hadi siku kwenye safari yako.
2.Kukata tamaa mapema
Rafiki kati ya tabia ambayo unatakiwa kikwepa kwa nguvu zako zoto ni pamoja na kukata tama mapema baada tuu yakushindwa kwa jambo Fulani ambalo ulitegemea lingeweza kukupa hatua fulani katika maisha yako na hii hutokea pale mtu unapo amua kufanya jambo ukiwa unategemea matokeo chanya pekee pindi utakapo pata matokeo tofauti na uliyo tarajia tayali unajikuta kukata tamaa na kuona kama hutoweza tena,
Rafiki nimuhimu kutambua lengo lako kabla hujaanza kufanya ili hata inapo tokea utofauti malengo yako ndiyo yakufanye kuendelea kupambana zaidi kutokana na lengo.
3.Visingizio,
Rafiki pindi upatapo wazo au lengo la kufanya jambo fulani huo ndo muda sahihi wa kuanza pasipo kujipa visingizio ambavyo vitakufanya usifanye mfano wa visingizio hivyo inaweza kuwa Sina muda,Sina mtaji,Fulani alifanya akashindwa rafiki ikiwa utajipa visingizio kamwe huto kuja kufanya maamuzi magumu yatakayo fanya usonge mbele kimafanikio.
4.Matumizo ovyo ya pesa,
Rafiki hapa ndo kwenye tatizo na kikwazo cha kutofanikiwa watu wengi huona pesa ndogo ndogo ndo zakutumia ovyo wakati sivyo,Watu wengi hufikili mafanikio pasipo kupangilia matumizi ya pesa zao wanazo zalisha,Rafiki ni muhimu kuitambua thamani ya pesa kubwa na ndogo mfano:Vodacom wanakukopesha shiling 500 kwa liba ya shilingi 100 yaani pesa wanayo kupa nikubwa kuliko liba unayo walipa wao wamesha tambua thamani ya pesa hiyo kwa watu kumi itakuwa sawa na Tsh 1000,
Unapo fanya malipo kwenye makampuni makubwa mfano mzigo wako ni wa Tsh 1,709,980 rafiki ikiwa huto lipa sh 80 mzigo wote utazuiliwa rafiki ni muhimu kutambua thamani ya pasa yako na kuiepusha na matumizi ya hovyo.
5.Kulizika,
Ndugu muda mwingi na kwatu wengi huhangaikia sana hitaji husika na wengine kuona wanacho kipata kinatosha na hivyo kuona hakuna haja ya kuwa na mkondo mwingine wa kuinhiza kipato kwa kujiambia MAISHA NI HAYA HAYA,TAJILI NITAKUWA MIMI KAMA FULANI AMESHINDWA,TUMIA PESA IKUZOEE kujiambia huku kutamfanya mtu kuwa pale pale,Lakini pia kianhaika kwa ajili ya wazo fulani mala tu utakapo litimiza jambo hilo unaona umesha maliza kila kitu,Kunawatu akisha jenga nyumba vyumba vitatu amesha maliza kuja kukumbuka nyumba haitoshi ni baada tu ya uzao wake kustawi yaani asha anza kupata wajuku.
6.Ulevi wa kwenye mitando ya kijamii,
Rafiki wakati watu wengine wakiona uwepo wa tekinolojia hii na fursa kwao kibiashara na kujijenga kiuchumi kuna watu wengi hasa umri wa 18_35 huona mitandao hiyo ipo kwa ajili ya wao kuuza sura na kuonyesha uwezo wao wa kimavazi na mengine mengi,Rafiki unatakiwa kujua kwamba hakuna jambo lisilo na hasara ikiwa utalitumia vibaya Mf: Wewe ni binti unae tumia muda mwingi kupost picha zako za uchi kwenye mitandao unajua nani atakuja kuibeba dhamana ya aibu yako kwenye maisha ya ndoa?
Rafiki badilika mapema kwani itakuletea shida baadae.
Mwisho,Rafiki ni muhimu muda wote kuwa na tabia chanya zitakazo kisaidika katika safari yako ya mafanikio,Rafiki kama nawe ni miongoni mwa watu wenye tabia hizo jua mafanikio kwako ni ndoto ya mchana huku ukiwa macho
Tafadhali badilisha tabia kwa matokeo na mafanikio yako makubwa 2017
Tuma ujumbe mfupi BIG KEY OF SUCCESSFULL 2017 kwenda 0715222989 au Email errynine6@gmail.com
Uunganishe na group la WhatsApp kwa mafunzo zaidi BURE.
Pia unaweza kulike page yetu Facebook. UFUNGUO WA MAFANIKIO.
Karibu sana na nikutakie siku njema
Wako rafiki katika mafanikio
Ernest Lwilla.
Chapisha Maoni