Habari rafiki na msomaji wa makala hizi kupitia ukulasa huu wa Errynine Tz,
Nimatumaini yangu tunaendelea kuweka jitiada na juhudi kubwa katika shughuri zetu za kila siku.
Miaka kadha iliyo pita ilikuwa mtu ukionekana kuwa na uchumi mkubwa ni MUUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA jambo lililo ibua sura mpya kwa vijana wengi na kujikuta katika dimbwi la usambazaji na utumiaji wa mabawa ya kulevya (UNGA)
Rafiki yangu na msomaji wa makala hii unatakiwa kufahamu kuwa nyakati zimebadilika sana
MFANO;
Vijana wengi mjini wanashindana na kuona ni ufahari kumiliki Simu, Nguo,Kutumia pesa kwa anasa *kijana anaingia bar nakuiteketeza laki tano nakufananisha na shilling 5000/=
Hii ni akili tuu ya baadhi ya watu ambao kimsingi bado hawajajitambua kwani kijana yeyote alie jitambua misingi yake mikubwa nikuwekeza katika mambo mbalimbali MFONO.
1.Laki tano kwake inauwezo wa kukodi shamba ekari 13 Mpwapwa na hapo atalima matikiti maji ambayo baada ya miezi mitatu itamtengenezea faida Million 15.
2.Laki tano inweza kuendesha shuguri za kilimo cha maharage ekari 2 ambazo baada ya miezi 4 atavuna sio chini ya million 3.
3.Laki tano inaweza kulima ekari 2 za matikiti maji baada ya siku 90 atavuna faida sio chini ya milioni 2.5.
Rafiki yangu mpendwa muda mwingine sio lazima uwafurahishe watu wanao kutizama jaribu kufanya jambo litakalo kupa faida kubwa kimafanikio yako binafsi.Watu wengi wanaona niufahari kuonekana mjini kila wakati wote,Kumbe wakati huo huo wengine wapo kusota ilikutegeneza mafanikio ya baadae.
Rafiki yangu mpendwa napenda kukumbusha Swala la uwekezaji nilamsingi sana hasa kwa wewe mwenye ndoto kubwa ya kufanikiwa.
Nikutakie kazi njema na zenye kubadisha maisha yako.
Wako katika Mafanikio ya kweli.
Errynine_Tz
Email:errynine6@gmail.com
Hotline;0715222989/0742962058
Chapisha Maoni