Habari rafiki yangu na msomaji wa makala hii kupitia ukulasa huu wa Errynine Tz nimatumaini yangu u mzima wa afya njema.
Mpendwa rafiki kila wazo linahitaji misingi imara ilikulifanikisha kwa wakati mwafaka,
Leo tujifunze zaidi misingi mitatu ya kutimiza malengo yetu tunayo kuwa tumejiwekea wenyewe ili kupata kitu fulani katika maisha.
Zifuatazo ni nguzo 3 za kutimiza malengo yetu.
1/JITAMBUE
Awaki ya yote unatakiwa kujitambua mwenyewe, wewe ni nani?Upo duniani kwa kusudi gani?Unataka nini?Na kwa wakati gani?
Baada ya kupata majibu ya maswali hayo muhimu utahitaji muda zaidi wakutafakari njia sahihi za kutimiza lengo lako,Ikiwa nipamoja na kuandika mpango maalumu utakao kufikisha hapo mapema.
Rafiki katika kujitambua kwako utahitaji muda mwingi zaidi kutafakari mipangilio sahihi ya lengo lako.
2/MUDA & JUHUDI.
Bila shaka ulisha wahi kusikia msemo huu MUDA NI MALI lakini huku tilia maanani yoyote juu ya muda wako.
Ndio muda ndo utajili mkubwa zaidi ikiwa utautumia vizuri hii itakupa faida ya kufanya mambo mengi zaidi yatakayo kuongezea thamani ya kipato chako.
Hapo utahitaji pia kuongeza kiungo kingine ambacho ni JUHUDI kama ulikuwa unafanya kazi kwa masaa 7 ongeza juhud katika masa hayo 7 na hata ikiwezekana fanya kitu kingine cha ziaada njee ya masaa hayo 7 yaani unaweza kubuni mladi mwingine utakao ufanya kwa masaa 5 na kuwa jumla ya masaa 12 unayo yatumia kwa siku. baada ya mwaka mmoja utakuwa umepiga hatua kubwa zaidi kimafanikio.
3.NIDHAMU;
Nidham iwe ndo ngao kubwa zaidi kwako katika kutimiza malengo yako,
Unahitaji nidhamu kubwa zaidi Kwajamii inayo kuzunguka,Shughuri zako unazo zifanya,Unahitaji nidhamu katika kipato chako na hapo ndo panahitaji nidhamu kubwa zaidi ilikufikia malengo yako unatakiwa kuwa na nidhamu kubwa kwenye MAPATO NA MATUMIZI YA PESA YAKO.
Sasa utakuta mtu amejiwekea malengo yake mazuri na makubwa sana alafu ikija kwenye nidhamu ya mapato na matumizi ni zero yaani Mapato yake kwa siku ni 30,000 alafu anatumia 25000 inayobaki 5000 ndo yakukamilishia malengo yake.
Hapo usipo badilika utaishia kuona mafanikio ya watu wengine nasi kwako.
Rafiki yangu kitu pekee kinacho mtofautisha mtu alie fanikiwa na asie fanikiwa ni nidhamu ya mapato na matumizi ya kipato chake hakuna kingine.
Mwisho kabisa ili ukamilishe malengo yako nilazima kwanza UJITAMBUE,TUMIA VIZURI MUDA NA JUHUDI KUBWA,KUWA NA NIDHAMU hapo ndani ya mda mfupi utaanza kunyoshewa mikono.
Karibu sana tujifunze pamoja.
Pia unaweza kutuma ujumbe BIG KEY OF SUCCESSFULLY 2017 kwenda 0715222989 uunganishwe kwenye group la WhatsApp kwa masomo zaidi
Wako katika mafanikio
Ernest Lwilla.
Chapisha Maoni