Habari rafiki yangu mpendwa nimatumaini yangu tunaendelea kujifunza maarifa mapya kila kukicha ili maarifa haya yawe Dira nzuri ya mafanikio yetu ikiwa tutayafanyia kazi.
Rafiki Maarifa ni nguzo kubwa zaidi katika kufikia mafanikio yako na ili uweze kujifunza lazima uwekeze muda katika kujifunza kila siku.
Zingatia misingi ifuatayo kuhakikisha unapata maarifa mapya kila siku na kila wasaa.
1.USIJIFANYE MJUAJI.
Ili uweze kujifunza inakubidi kujishusha na hata kuipa akili yako nafasi ya kujifunza mambo mengi zaidi kwani hata kama unajua huwezi kuyajua yote,
Kuna watu wao hujipa nafasi katika kuyajua mambo yote jambo ambalo haliwezekani ili uweze kujifunza lazima ujipe nafasi ya kujifunza pasipo kujifanya mjuaji wakati wowote.
2.INAFAA KUWA MJUAJI.
Rafiki nivizuri kujifunza na hata kutumia maarifa unayo jifunza pale yanapo hitajika mfano Unaplani kufanya jambo ambalo linahitaji maarifa ambayo tayari umekwisha kujifunza hapo tumia maarifa hayo ili yakuongoze katika jambo hilo Eg,
a)Biashara tumimia maarifa uliyo nayo ili kuanza na kukuza zaidi biashara yako.
b)Ufugaji hali kazalika kama unaelimu juu ya ufugaji tumia elimu hiyo kufanya ufugaji wako kuwa wa tofauti zaidi kutokana na elimu hiyo.
c)Kilimo pia katika kilimo tumia maarifa uliyo nayo ili kufanya kilimo chenye tija na faida kubwa kutokana na maarifa uliyo nayo katika kilimo.
3.USIJE UKAJUA KWA WAJUAJI:
Ingawa nivizuri kuwa mjuaji kwa vile unavyo vijua na usivyo vijua jifunze zaidi kwa wanao jua kwani ukijifanya mjuaji huto weza kujua mengine ambayo huyajui, kumbuka kujifunza kila siku ndo njia pekee ya kujua mengi.
Rafiki mwisho usije ukawa na maarifa mengi zaidi pasipo kuyatumia hayo maarifa sawa na mtu asie jua,Muda mwingine tumia muda wako kuwafundisha wenzako unavyo vijua ili ujifunze usivyo vijua.
Nikutakie siku njema na yenye mafanikio zaidi.
Tuma ujumbe BIG KEY OF SUCCESSFUL 2017 kwenda namba 0715222989 kuunganishwa na kundi la WhatsApp kwa mafunzo zaidi.
Wako katika mafanikio,
Ernest Lwilla.
Chapisha Maoni