Unknown Unknown Author
Title: SUMAKU YA MAFANIKIO INAWATAKA WATU WENYE SIFA ZIFUATAZO.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
   Habari rafiki na mwanamafanikio kupitia ukula wetu Ufunguo wa Mafanikio,Ni tumaini langu kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kawaida ...

   Habari rafiki na mwanamafanikio kupitia ukula wetu Ufunguo wa Mafanikio,Ni tumaini langu kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kawaida ya kila siku.
   Rafiki ni siku nyingine nzuri sana kwangu na kwako pia siku ambayo tunajukumu kubwa zaidi la kuweka juhudi zaidi kwenye shughuli tulizo chagua kufanya.

  Rafiki ni ukweli usio fichika kuwa kila mtu ana kiu kubwa ya mafanikio,Kila mmoja anaye haingaika popote pale naimani yupo kwa sababu anatafuta kufanikiwa.Rafiki popote na kwenye chochote unacho fanya  Mafanikio yapo na kila mahali na kila sehemu ila mafanikio hayako kwa kila mtu yaani si kila anaye tafuta anamafanikio.

  Rafiki iliuweze kufanikiwa lazima uwe mtu wa tofauti kifikra na zifuatazo ni sifa zinazo mfanya mtu au watu kufanikiwa katika maisha.

1. Walio tayari kutoa kile walicho nacho kwa ajili ya wengine.
     Rafiki ili uweze kuvuna ni lazima upande na hii ndivyo ilivyo hata kwenye safari ya mafanikio ili ufanikiwe lazima utoe kitu kwa watu wengine ndipo nawe ufanikiwe lazima uguse maisha ya watu wengine ndipo ufanikiwe,
   Muda mwingi na kwa watu wengi huwa wanafikiri kutoa kwa watu wengine ni sababu kubwa ya wao kuto yafikia mafanikio yao,Hii husababisha watu wengi kubaki pale pale walipo kuwa pasipo kubadilka chochote kwasababu hawagusi maisha ya watu wengi.

    2. Walio tayari kujifunza na kufundishika.
     Rafiki kunautofauti Mkubwa wa kujifunza na kufundisha,Kujifunza ni kupokea Maarifa mapya kupitia vyanzo mbali mbali vya elimu bora ukianzia kwenye maisha ya kila siku,Kufundisha ni hali ya kutoa ulicho jifunza na kuwafanya wengine wajue kitu unacho kijua,
      Kufundisha ndo njia pekee ya kuzidi kujua zaidi tofauti na unapo baki na kile ulicho nacho katika elimu yako yaani unapo toa elimu kwa mtu mwingine inakuwa ni nafasi ya wewe kuelewa na kufanyia kazi Maarifa uliyo nayo.

    3. Walio tayari kulipa gharama za mafanikio.
    Rafiki mafanikio sio kitu cha rahisi kama wengi wanavyo dhani,Mafanikio yanahitaji ghalama ili kuya pata,Mafanikio yana hitaji kulipia maghama za kujifunza na kuwa wavumilivu zaidi katika safari ya mafanikio.
     Muda,Uvumilivu,Maarifa,Kujituma na mengine mengi ndo huleta mafanikio yaliyo ya kweli na vyote hivyo ni lazima ukubali kulipia ghalama Kwa mfano huwezi kupata shati pasipo kipia,Huwezi kupata chochote pasipo kulipia ndivyo ilivyo hata kuyapata mafanikio.

      4. Walio tayari kufuata sheria na kanuni za mafanikio.
Kila jambo lina kanuni na sheria ili uweze kulipata hata mafanikio pia yana kanuni zake na ili uya pate lazima uzifute kanuni hizo,
    Kila alie fanikiwa nyuma yake kuna historia nzito zaidi na kuna sheria alizo zifuata hata kuya fikia mafanikio yaliyo nayo ,
  Rafiki tafuta kanuni utakazo zitumia kwenye safari yako ya mafanikio pasipo kujiwekea kanuni huwezi kufikia mafanikio yako.

      5.Walio tayari kushirikiana na watu sahihi wenye fikra chanya na mawazo chanya kimafanikio,Rafiki ili ufanikiwe lazima wewe uwa tizame watu wenye kiu sawa na yako hata ikiwezekana walio kuzidi,
     Watu hawa ndo unaweza kushiriakiana nao na hata kuwashilikisha mipango yako katika mafanikio yako,Waepuke watu wenye fikra hasi watu ambao wanawoga juu ya vitu vikubwa ambavyo wewe unavihitaji zaidi katika mafanikio yako.

      6. Watu wawazi, wakweli na waaminifu ktk kauli na vitendo vyao.
   Rafiki sio kila mtu anakufaa kuongozana nae katika safari ya mafanikio yako,Watu wasio wasili,walio wakweli na wa aminifu ndo watu peke wanao tatikiwa kuwa nao katika safari yako ya mafanikio.

    7. Walio tayari kubadilika na kuachana na mazoea.
   Rafiki ni vizuri kuishi kwa kutengeneza histori mpya ya maisha na si kuishi kwa histori ya maisha yaliyo pita,Nasi vema kukumbuka mambo uliyo yashindwa katika maisha kwani yanakatisha sana tamaa ya kudhubutu jambo lingine kwa wakati mwingine,
   Tabia ya mazoea ndo tabia peke inayo watofautisha watu walio fanikiwa na wasio fanikiwa kimaisha rafiki epuka kuishi kwa mazoea.

      8. Walio tayari kukabiliana na changamoto na sio kuogopa cuangamoto.
    Kipimo cha mwanafunzi yeyote kuendelea na dalasa lingine ni mtiani na kama hata weza kufanya mtiani ata endelea na darasa lile lile.
    Rafiki kipimo cha mtu yeyote katika kufanya jambo kwa ubora na uimara ni Changamoto,Na kama unaziogopa Changamoto niwazi hupo tayari kuya tafuta mafanikio,MAFANIKIO sio kitu rahisi na kama Inge kuwa rahisi basi walio fanikiwa wasinge furahia na kuendelea kuimarisha misingi zaidi ya mafanikio yao,
   Rafiki zipende Changamoto,Zifurahie changamoto, Jifunze kupitia changamoto unazo kutana nazo ili ufikie mafanikio yako.           

     9. Walio tayari kushaurika na kukosolewa.
    Sasa kunawatu ukiwa kosoa wana chukia na kukutenga wao wanapenda zaidi unapo wambia wamefanya vizuri hata kama wanapotea njia,
   Watu hawa hawawafai zaidi katika maisha,Rafiki ili ufanikiwe lazima ukubali ushauri na kukosolewa pindi unapo kosea au maboresho ya kile unacho kifanya katika kazi yako.

      10.Watu walio tayari kuishi maisha yao na sio maisha ya wengine yaani wasiotaka kuishi maisha ya kuiga bali kuishi kiubunifu na  kubuni njia zao za maisha na sio za wengine.
    Rafiki kuna watu wao kazi yao ni kuangalia Fulani amefanya nini ndipo nao wa fanye sasa wanapo kutana na changamoto wa na kuwa hawana uvumilivu kwa sababu kwanza wameiga kwa kuona mtu amefanikiwa.
    Rafiki ubunifu ni kitu kikubwa sana katika safari yako ya mafanikio maana kwanza utafanya kitu unacho kipenda na kuki furahia mala zote unapo kifanya na hivyo inakuwa rahisi zaidi kufanikiwa kwako.

     Tuma ujumbe mfupi BIG KEY OF SUCCESSFULL 2017 kwenda 0715222989 / Email:errynine6@gmail.com
Uunganishwe na group la WhatsApp kwa kujifunza zaidi BURE.
Pia like page yatu ya Facebook Ufunguo wa mafanikio

Wako rafiki katika mafanikio
     Ernest Lwilla

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top