Unknown Unknown Author
Title: KUWA SABABU YA MAFANIKIO KWA WENGINE NAWE UFANIKIWE ZAIDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
   Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa Mafanikio,Rafiki ni tumaini langu kuwa ni mzima wa afya njema k...

   Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa Mafanikio,Rafiki ni tumaini langu kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu,
   Rafiki siku nyingine nzuri sana kwangu na kwako pia kama mpambanaji ni nafasi nzuri kwetu kuongeza juhudi na Maarifa zaidi kwenye shughuli zetu zitakazo tufikisha kilele cha mafanikio.

  Ili upate kitu lazima utoe kitu,Ili ufanikiwe lazima ushindwe mala kadha ndo ufanikiwe wapo watu ambao ni wabinafsi na kuweka siri ya mafanikio yao katika jamii,
  Ukweli ikiwa utautumia muda mwingi kusaidia wengine ili waweze kufanikiwa una kuwa unatengeneza nafasi kubwa ya wewe kufanikiwa.

  Kuwa sababu ya mafanikio kwa wengine ndipo nawe ufanikiwe zaidi hii imaana unapo wasaidia watu na kufanikiwa kutokana na wewe nao wataona nafasi yako katika mafanikio yao na kisha kukupa malipo ya mafanikio yao,Siku chache kabla sijapata mwanga wa kujifunza kupitia makala siku wai kufikilia kulipa ghalama ya kujifunza lakini baada ya kuona mafanikio ya kujifunza mwenyewe nilijikuta kununua Vitabu kwa wale wanao nifundisha,Nikaanza kulipia ghalama za semina Online na mengine mengi,Je unadhani hawa walimu wange kaa na ujuzi wao pasipo kunisaidia wange chukua kwa mfumo gani pesa yangu?Kujitoa kwao na kutushika mkono ndo kunako pelekea wao kufanikiwa kifedha nami nikifanikiwa kimaarifa zaidi na baadae kivitendo.

   Rafiki ni kitu gani unaweza kukifanya na kikamsaidia mtu mwingine kwenye nafasi ya mafanikio yake na kuona umuhimu wa kulipia ghalama ya huduma au msaada ulio mpa,Kila binadamu ana kitu ndani yake kinacho weza kumsaidia mtu mwingine ili aweza kufanikiwa,
   
   Mwalimu wangu wa Fursa 101 Geofrey Tenganamba ali wai kusema WEWE NI SABABU YA MAFANIKIO YANGU,NAMI NI SABABU YA MAFANIKIO YAKO,
Akiwa na maana alicho nacho kinatakiwa kuwa sababu ya mafanikio yangu lakini sio bure lazima nitoe ghalama ya kujifunza kitu hicho,Wapo watu wengi wakisikia kutoa ghalama au kulipia huduma Fulani ambayo haina faida ya moja kwa moja kama ilivyo Biashara zingine huingia mitini na kuona bora kuendeshwa na ujinga kuliko kulipia ghalama za kuwa toa kwenye dimbi hilo la ujinga,
  
Rafiki fanya chochote kitakacho kuwa na matokeo chanya ya kimafanikio kwa wengine ndipo nawe ufanikiwe zaidi kwenye maisha yako,Wapo watu wana liskia neno Fursa na kuli kurupikia bila kujua nini unatakiwa ufanye ndipo Fursa hiyo ikulipe au ikuingizie pesa ni lazima imefanikishe mtu kwenye jambo Fulani ndo atoe ghalama za huduma hiyo ndipo neno Fursa ligeuke kwako na kukuingizia kipato.

   Ikiwa utakuwa mbinafsi katika mafanikio yako ujue hata ikitokea changamoto ambayo ipo nje ya uwezo wako na ipo ndani ya uwezo wa watu wengine lazima ikurudishe nyuma kwa sababu huna ushirikiano wala msaada kwa wengine,Kama wewe unauwezo kiuchumi fanya watu wengine wafanikiwe ili uchumi wako ukue zaidi,Kama unakipaji cha kufundisha basi fanya juhudi ya kufundisha ndipo uingize kipato kutokana na uwezo wako wa kufundisha,Kama ni mwandishi andika kitabu kitakacho kuwa suluhisho la matatizo ya wengine ndipo uingize kipato kupitia kutatua kero zao ,Rafiki kuwa sababu ya mafanikio kwa wengine ili ufanikiwe zaidi,
   Katika Biashara lazima ukubali Biashara yako iwasaidie wengine au itatue kero za wengine ndipo ipate wateja na kukuingizia faida kubwa mmiliki wa biashara hiyo.

   Rafiki ni muhimu kuwa na subila kubwa zaidi katika kuhakikisha unawasaidia wengi yaani usitegemee uwasaidie leo kesho wakulipe lazima waone  kitu ndani yao ndipo wasukumwe kulipia ghalama hiyo.
   Rafiki Mimi ni sababu ya mafanikio yako kwenye chochote nacho kifanya nawe unatakiwa kuwa sababu ya mafanikio yangu.

   Tuma ujumbe BIG KEY OF SUCCESSFULL2017 Kwenda 0715222989/Email:errynine6 @gmail.com Uunganishe na group la WhatsApp kwa mafunzo zaidi BURE.
   Pia unaweza kulike page yetu ya Facebook UFUNGU WA MAFANIKIO kwa makala zaidi.

  Nikutakie siku njema na yenye mafanikio zaidi ya jana.
Ni wako rafiki katika mafanikio
       Ernest Lwilla.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top