Unknown Unknown Author
Title: UNA NINI MKONONI?
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
   Habari rafiki na mwana mafanikio kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa mafanikio, Nitumaini langu kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwa...

   Habari rafiki na mwana mafanikio kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa mafanikio, Nitumaini langu kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu ,
   Rafiki ni siku nyingine nzuri sana kwako na kwangu pia ikiwa tutaitumia siku hii vizuri na kwa kuongeza juhudi zaidi kwenye shughuli zetu za kila siku.

  Rafiki karibu tujifunze pamoja somo letu UNA NINI MKONONI?,Rafiki ulicho nacho hicho ndo silaha ya wewe kurnda mbele na kufikia mafanikio yako pasipo kujali ukubwa wa malengo na ndoto yako,Rafiki anza na ulicho nacho hata pasipo kujali udogo wake maana kuna vingi ambavyo unaweza kufanya kupitia hicho ulicho nacho Mfano.

  Mkononi una shilingi 20,000 wazo rahisi sana unaweza ukaenda sokoni na ukanunua bidha zitakazo kuwezesha kuandaa unga wa lishe na ukanunua chupa na vikombe kisha ukaandaa uji wa lishe na ukauza kikombe shilingi mia 500 kwa kuwa fikishia watu wa jamii yako ambapo ni lazima uuze tu.

   Ulicho nacho ndicho unacho takiwa kuanza nacho maana kwa kupitia hapo utaweza kufikia malengo yako ya kukuza Biashara na unatakiwa kufahamu Biashara zote kubwa unazo ziona zilianza na udogo na kisha kukua.
  Rafiki hautakiwi kufikiri au kusubili kikubwa ambacho huna mkononi maana unaweza kusubili kwa muda mrefu pasipo kukipata na muda ukaendelea kusonga lakini kama utaanza na ulicho nacho ni rahisi kupata hamasa zaidi na hata kutafuta nguvu ya ziada kukuza Biashara yako

  Na hata ukichunguza kwa uzingatifu wa ndani utajua kuwa mitaji mikubwa ndiyo chanzo cha kuwa katisha tamaa watu walio na kipato kidogo,Tizama una nini mkononi kisha angalia kiasi hicho kinaweza kufanya nini kwa mfumo wa fursa ndipo utaweza kuanza Biashara itakayo kua kwa kasi.

  Rafiki sababu kubwa ya watu wengi kuto chukua hatua ya kuanza Biashara ni ukosefu wa mtaji au uhaba wa mtaji lakini huyu mtu unakuta hajafanya uchunguzi wa kina nini anataka afanye? Na anatakiwa kuwa na kianzio kiasi gani?Na atafanya kazi na nanani?
  Rafiki mtaji si pesa peke,Unatakiwa kufahamu mtaji ni pamoja na wazo la Biashara yako,Mtaji ni pamoja na nguvu zako,Watu walio kuzunguka,Muda wako,Ujuzi ulio nao na jinsi ya kutumia kama kianzio cha Biashara yako.
   Angalia jamii yako inaupungufu wa kitu gani nawe mkononi unanini na unaanzaje kutatitua kero hiyo kwa pesa ndogo uliyo nayo.

  Rafiki una nini mkononi kisha tathimini kisha chukua hatua ndogo kisha kuza ili iwe kubwa.

  Tuma neno BIG KEY OF SUCCESSFULL 2017 kwenda 0715222989/Email.errynine6@gmail.com
Uunganishwe ma group la WhatsApp kwa maarifa zaidi BURE.

Pia unaweza kulike page yetu Facebook UFUNGUO WA MAFANIKIO

Nikutakie siku njema na yenye mafanikio zaidi kwako,

   Wako rafiki katika mafanikio
         Ernest Lwilla

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top