Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa mafanikio,Nitumaini langu kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu,
Rafiki ni siku nyingine nzuri sana kwangu na kwako pia ikiwa tutaitumia vizuri siku hii has a kwakuweka juhudi zaidi katika shughuli zetu za kila siku.
Rafiki mafanikio huja kwa kuweka juhudi lakini hata ukipata mafanikio pasipo kujitambua ni kazi bure maana hayo mafanikio kwako yatapita kama njia,
Kujitambua ndo njia peke itakayo kupa mafanikio yaliyo ya kweli na ili uweze kujitambua lazima ujiulize mwenyewe maswali kadha katika nafsi,Maswali hayo nikama yafuatayo.
1. Wewe ni nani?
Hata ikitokea leo kama zali la umepata pesa kama hujajielewa wewe ni nani kuzipoteza ni sekunde kama ulivyo zipata,Swali hili ni mfano wa kalama au zawadi uliyo nayo ndani yako ambayo na unaitumiaje kwa wengine,Wewe ni nani? Na kwanini uwe wewe? Na unautofauti gani unao kutofautisha wewe na wengine yaani kalama uliyo nayo ndo inayo kutofautisha na wengine Jitambue Wewe ni nani?
2. Umetokea wapi?
Muda mwingine kipimo sahihi cha wewe ni pale ulipo toka,Kwakutazama ulipo toka na kupata picha halisi ya ulipo toka unaweza kujiweka tofauti na wengine Mfano:Umetokea katika Familia duni kiuchumi kamwe huwezi kuendelea kufanya mambo yanayo zidi kukuweka ulipo zaidi utafanya juhudi zaidi ya kusinga zaidi,Rafiki jiulize wewe ni nani Umetokea wapi? Hii itakupa feature nzuri zaidi ufanye nini cha kukutofautisha na ulipo toka.
3. Unaelekea wapi?
Ikiwa tayari umesha jijua wewe ni nani? Umetokea wapi basi ni rahisi zaidi kujua unaelekea wapi na kutengeneza mfumo sahihi utakao kufikisha hapo unapo taka kuelekea,Ni lazima na ni muhimu kuwa na picha sahihi ya wapi unakwenda maana huwezi kupoteza na kelele za wengine ambazo kwa kiasi kikubwa zinaweza kukukwamisha kuto fika unapo elekea.
4. Umefika wapi?
Muda mwingine ni muhimu kuwa na kumbukumbu ya kila hatua unayo pitia katika maisha yako maana pasipo kulijua hilo unaweza kuhisi unasogea hatua nyingine kumbe umeganda palepale ulipo kuwa na kwa mda mrefu,
Rafiki muda mwingine uwa najitafakari mwenyewe kwa Mfano ninapo anza mwaka mpya maswali nayo jiulizaga nikama Nilianza mwaka na nini na ninafunza mwaka ma nini?
Je nimepiga hatua au nimerudi nyuma kwa kufanya ivo uwa najua nilipo fikia,
5. Natakiwa nifanye nini?
Safari ya maisha kuelekea Mafanikio ama chochote kile unachokihitaji, huanzia katika kujitambua ikiwa utajitambua niwazi utakuwa na vingi sana vya kufanya ingawa unatakiwa kuwa na vitu vichacha na kuvifanya kwa ufasaa na ubora wa hali ya juu,Muda mwingine ni vizuri kujua wajibu wako na ukajua ni wapi edhamilia kufika kwa kujiwekea mwisho wa muda,
Rafiki pasipo kujipa maswali wala majibu ya maswali hayo ujue bado hujajitambua na hivyo unahitaji kujipa muda na kuchukua hatima ya maisha yako mwenyewe.
Tuma neno BIG KEY OF SUCCESSFULL 2017 Kwenda 0715222989/Email;errynine6@gmail.com
Uunganishwe na group la WhatsApp kwa mafunzo zaidi BURE
Pia unaweza kulike page yetu Facebook UFUNGUO WA MAFANIKIO kwa mafunzo zaidi
Wako rafiki katika mafanikio
Ernest Lwilla.
Chapisha Maoni