Unknown Unknown Author
Title: TEMBELEA SEHEMU HIZI TATU MUHIMU KUELEWA ZAIDI MAANA YA MAISHA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
   Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa Ufungu wa mafanikio ni tumaini langu kuwa ni mzima wa afya njema kama iliv...

   Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa Ufungu wa mafanikio ni tumaini langu kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu,
   Ni siku nyingine nzuri sana kwetu sote kama wanamabadiliko makubwa ya kiuchumi ambayo yanahitaji juhudi ya Kujifunza kuliko ambatana na vitendo zaidi.

   Maisha ya kiumbe chochote chini ya jua yana tafsiri na maana kubwa sana ambayo ni ngumu sana kuielewa kama utatizama upande mmoja ambao wewe umehiari kutizama,
  Mala zote upande wenye mvuto wa kutizamwa ni upande wenye maisha mazuri yasiyo na misuko suko ya aina yoyote,Maana ya maisha kamwe haiwezi kutimia kimaana kama utatizama sehemu moja lazima utembelee na kutizama sehemu nyingine ambayo wewe haupo,
  
     Sehemu hizi zinaweza kuwa ni sehem 3  ambazo ni

              HOSPITALINI
Hii sehemu inayo fananishwa na  mfano wa Gereji ambapo huduma za uboreshaji na urekebishaji wa afya za magari na vingine vingi hufanyika.Binadamu miili yetu inachakaa na inapo hitaji marekebisho hupelekwa Hospitalini ambapo haina maana kwenda hospitalini ni lazima uwe unaumwa,
  
    Ni muhimu kutembelea hospitalini na kuiona ni sehemu ya maisha yetu kwani kunawakati utahitaji huduma au kuhudumia ,Lakini pia kutoka na kutembelea huko kutakupa ni dhamu kubwa ya kutunza afya yako na kuheshimu afya kama mtaji namba moja ya mafanikio.

                GEREZANI
  Ukiwa unauhuru wa kufanya mengi na kijiona wewe ndo wewe kumbuka wakati huo huo kuna watu wapo chini ya ulinzi wanalindwa na Uhuru wao upo mikononi mwa wanyang'anyi wa haki,
   Ni uhuru tu ndo kitu unacho jivunia nacho kwa sababu unafanya chochote popote ambacho ni halali kuelekea mafanikio yako Je una pata picha gani kwa mtu ambae hana uhuru wakati huo.
    Ni muhimu sana kutembelea Magerezani ili kujua vitu unavyo vifaidi unapo kuwa na uhuru na hata kuwapa imani walio poteza uhuru wao na kuona nao ni sehemu ya jamii pia utaji funza matumizi sahihi ya muda na uhuru ulio nao kuelekea mafanikio yako.

                 MAKABULINI.
Uweli ni kwamba kifo ndo risk kubwa sana na isiyo kwepeka kwenye maisha ya kiumbe chochote ususani binadamu,Muda mwingine jaribu kutafuta takwimu za watu wanao zaliwa na hata wanao kufa kila siku na kila saa ukiweza zaidi lisaa na hata dakika na sekunde,
  Unagundua nafasi yako kuwa hai sio bure ila ni kwakusudi maalumu la kufanya kitu kwa wengine na kuweka alama ya ukumbusho wako,Na utakipo gundua kila sekunde kuna watu wanao fariki basi ni nafasi ya kila sekunde kufanya kitu kitakacho badilisha maisha yako na kuweka alama imara ya uhai wako.

    Pia ni vema kufahamu chochote kilicho na mwanzo lazima kiwe ma mwisho na kama kuna mwisho,Jiulize mwisho wako utakuwaje?Utakuwa umesha wagusa wangapi?
Chukua hatua kubwa kuelekea mafanikio yako.

   Tuma neno BIG KEY OF SUCVESSFULL 2017 kwenda 0715222989/Email.errynine6@gmail.com
Uunganishe na group la WhatsApp kwa kujifunza zaidi BURE

Pia unaweza kulike page ya Facebook UFUNGUO WA MAFANIKIO.

Nikutakie siku njema na yenye mafanikio tele.
     Wako rafiki katika mafanikio
Ernest Lwilla.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top