Unknown Unknown Author
Title: MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA HUJAANZA BIASHARA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
   Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa mafanikio,Ni tumaini langu ni mzima wa afya njema kama ilivyo k...

   Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa mafanikio,Ni tumaini langu ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu
  
  Ni siku nyingine nzuri sana kwangu na kwako kama mwana mafanikio kuitumia siku hii kwa kuweka juhudi zaidi kwenye kazi tulizo chagua kuzifanya katika maisha,

    Mwanzo wa biashara yoyote ni wazo na wazo likitendewa kazi ndipo huwa katika hali ya kuonekana kwa wazo hilo.

   Rafiki biashara yoyote ambayo unategemea kuanza kuna mambo ya msingi kuya jua na yatakayo kuongoza katika hiyo biashara ili iweze kukua na pasipo kufa,Rafiki mambo hayo ni kama yafuatayo.

                TAARIFA ZA BIASHARA HUSIKA,
    Kabla hujaanza biashara ni muhimu kutafuta taarifa sahihi za biashara husika ambazo vyanzo vyake ni kutoka kwa watu ambao tayari wapo kwenye biashara hiyo au kwenye vyanzo vya mbali mbali vilivyo vya uhakika katika biashara hiyo pia unaweza kuzipata taarifa hizo kutoka mtandaoni.
   Katika kupata taarifa hizo hutakiwi kuzipata kwa mtu mmoja kwani watu wengi ni waongo na watakupa taarifa zisizo sahihi hivyo ni muhimu kukutana na watu kadhaa ambao tayari wanaifanya biashara hiyo kisha jibu litakalo jitokeza zaidi ya mala mbili hilo ndilo unatakiwa kulitumia kuanzisha biashara yako.

     JUA GHARAMA SAHIHI ZA BIASHARA HIYO.
   Watu wengi wamekuwa wakianza biashara kwa kuto jua ghalama za biashara anayo taka kuianza jambo ambalo limekiwa likileta shida na hata kuwa risk kubwa ya wao kupoteza mitaji yao kwasababu tu hawakujua ghalama za biashara zao.
     Mtu unaweza ukawa na Tsh milioni 1 ambayo ukaikadilia na kuona itaweza kuendesha biashara yako na baada ya kuanza unakuta kuna mambo mengi ambayo yanakuhiyaji ufanye tena kwa kuongeza pesa nje ya milioni moja Mfano;Usajili wa biashara,Mapato,Kitabu cha mauzo na mengine mengi  ambayo haya kuwa ndani ya milioni moja kama ilivyo kuwa umepangilia biashara yako

      JUA SOKO NA CHANGAMOTO ZA BIASHARA,
  Soko linatakiwa zaidi hasa kwa wale wanao hitaji kuanza biashara za kuzalisha na kusambaza,Ni muhimu zaidi kujua soko la bidhaa unayo taka kuzalisha na ndipo uanze kuzalisha bidhaa na hata ikiwezekana ujue wahitaji wa bidhaa hiyo ni nani,
   Pia ni muhimu kujua changamoto zaidi hasa kwa upande wa uzalishaji wa bidhaa hata hasa kwa upatikanaji wa material ambazo utazitumia kuzalisha bidhaa yako.
  Kuna mambo mengi sana yanayo husisha biashara na ni muhimu kuwa makini zaidi kabla ya kuanza biashara.
 

  Rafiki biashara nyingi sana zinaanzisha na kufungwa kwa muda usio mrefu kwa sababu ya kukulupuka kuanza na baadae matokeo  kuwa tofauti na mitizamo ya awali

   Nimuhimu kuwa na taarifa za kina za kuhusu Biashara unayo tegemea kuanza.

Tuma neno BIG KEY OF SUCCESSFULL 2017 kwenda 0715222989 au email:eryynine6@gmail.com
Uunganishe na group la WhatsApp kwa mafinzo zaidi BURE.
Au unaweza kulike page yetu Facebook UFUNGUO WA MAFANIKIO

   Nikutakie siku njema na yenye mafanikio makubwa kwako
   Niwako rafiki katika mafanikio
       Ernest Lwilla
 
  
  

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top