Habari rafiki na mwanamafanikio mwenzangu kupitia ukulasa huu wa Ufunguo wa mafanikio,Nitumaini langu kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu,
Rafiki ni siku nyingine nzuri sana kwetu sote zaidi tunatakiwa kuongeza juhudi zaidi ili kuufanya mwakaa huu kuwa mkubwa zaidi kimafanikio kwetu sote,Nikukaribishe kwa moyo mkunjufu na tujifunze pamoja kupitia makala hii somo letu zaidi litajikita kujua kosa kubwa zaidi linalo fanywa na wafanya biashara kupitia biashara ya mtandao yaani NetworkMarketing!
Nikiwa mmoja kati yao ambae nimefanya biashara hii kwa zaidi ya miaka 2 pasipo kufanikiwa kwa mafanikio yanayo onekana zaidi ya kujifunza kupitia changamoto zinazo ikabili biashara hii na wafanyabiashara wenyewe kwa ujumla wao.
Kosa nililo jifunza hapa ni Wafanya biashara wenyewe kuzungumzia mafanikio makubwa ambayo wao binafsi hawana na wanaamini yapo kwenye biashara hii pia muda wote wana fundisha zaidi mafanikio ambayo huonyesha kupatikana bila changamoto jambo ambalo sio la kweli.
Wafanya biashara wengi huonyesha mafanikio makubwa zaidi yanayo patikana kutokana na fursa au biashara hiyo ikiwa wao wenyewe hawayaishi mafanikio hayo kwa maana hiyo hutumia zaidi mifano ya video kuliko uhalisia wao wenyewe kwenye biashara,
Hii pia inapelekea kwa wafanya biashara hawa kutoa taarifa za wongo ili kufanya watu waamini uwepo wa biashara hii ya mtandao lakini inakuwa ngumu sana mtu kuchukua uamzi wa kujiunga kwani hawaamini kuwa biashara hii ni halali na inawanufaisha watu.
Rafiki ukweli biashara ya mtandao ni biashara kubwa na nzuri sana na inayo wanufaisha wengi lakini sio kwa urahisi unao hadisiwa na wafanyabiashara wengi ambapo inaonekana ukisha ingia kwenye mfumo huu unakuwa tayari umesha fanikiwa,Rafiki hupaswi kumdanganya mtu juu ya mafanikio yanayo patikana kwenye biashara ya mtandao zaidi mtu ndiye aamue kujiunga zaidi akijua atatakiwa kutumia muda,Pesa na hata maarifa makubwa zaidi ili kujenga biashara yake iliyo kubwa na itakayo mlipa lakini usimdanganye kwa kumwonyesha mafanikio yaliyo makubwa zaidi kirahisi rahisi.
Rafiki huna sababu ya kudanganya chochote kwani utajenga timu inayo amini mafanikio kwenye biashara ya mtandao ni rahisi kumbe sio kweli kiasi mtu anaingia na kukaa kusubili mafanikio pasipo kufanya kazi jambo ambalo sio kweli,
Tengeneza timu iliyo imara na inayo jua wajibu wake katika kutafuta mafanikio katika kujifunza na kufanya kwa vitendo vinavyo obgozana na juhudi,Nini hasa kisudi la wewe kudanganya kama nilivyo tumia muda mwingi mimi kuwadanganya wengine kama milivyo danganywa mimi pasipo kujua vizuri nini kusudi la mimi kuingia kwenye biashara ya mtabdao,
Mwisho tumia muda wako kusababisha watu wajue nini maana ya biashara ya mtanda kisha wafundishe wafanye kama unavyo fanya na uwape tumaini la mafanikio baada ya kufanya kazi kwa juhudi na sio kutumia mbinu za udanganyifu ambapo utajenga tibu iliyo dhaifu katkika biashara yako.
Rafiki ni kutakie mafanikio zaidi katika kujifunza na endelea kufuatilia makala hizi zaidi nikukaribishe kwenye group letu la WhatsApp
Tuna ujumbe BIG KEY OF SUCCESSFULL2017 kwenda namba 0715222989 Email:errynine6@gmail.com
Uunganishwe na uendelee kupata mafunzo zaidi BURE.
Karibu nimechagua kusafiri na wewe katika mafanikio yangu.
Chapisha Maoni