Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitia blogu yetu pendwa Ufunguo wa mafanikio ni tumaini langu kuwa ni mzima wa afya njema kabisa,
Rafiki ni siku nyingine iliyo nzuri kwetu sote kama wasaka mafanikio hatuna sababu ya kutuzuia kuendelea kufanya yale tuliyo chagua kufanya kwa ubora zaidi ili kufikia mafanikio yetu.
Rafiki kila unacho kifanya ni somo ikiwa utaamua kujifunza hasa unapo pata matokeo tofauti na yale uliyo yategemea kupata,Nini hasa ninajifunza kwenye maisha ya kutafuta mafanikio wakati nikiendelea na uandishi?
Jibu!
Watu wengi huanza kufanya mambo mengi kwa kuweka nguvu ndogo,maarifa hafifu na kuto shirikisha wengine huku wakitegemea matokeo makubwa kutokana na mitizamo yao, Ukweli watu ni wavivu wa kutoa mwitikio wa kujifunza na kuchukua hatua sahihi,Watu wengi sio washirikishi yaani wanaamini wao Pekee pasipo nafasi za watu wengine kwenye mafanikio yao Je utayapataje mafanikio bila kujifunza? Pasipo kuwa na watu? Utapigaje hatu kama unakwepa kutafuta maarifa,Utapataje mafanikio pasipo kutumia pesa?
Hiki ndicho kitu nilicho jifunza hasa kutoka kwa watu wengi sana ambao wanapambana kila siku kuhakikisha wanayafikia mafanikio na hiyo ndiyo sababu inayo waweka mbali zaidi na mafanikio yao licha ya mafanikio hata hivyo wanakuwa hawana walicho jifunza kutokana na matokeo wanayo yapata mara kwa mara,Rafiki ikiwa utajifunza kitu ni lazima kuwe na mabadiliko yatakayo onyesha hatua ya kujifunza kwako na hata muda mwingine unahitaji kutumia nguvu ili kupata matokeo yaliyo bora zaidi katika hatua za mafanikio yako.
Pia kunawatu wanao tafuta mafanikio lakini hawajui ni aina gani ya mafanikio wanayo yataka yaani sawa na kutumia nguvu nyingi kuhamoisha kifusi pasipo kujua sababu ya kuhamisha kifusi hicho unataka nini? Je wanategemea nini kutokana na nguvu nyingi wanazo tumia?
Rafiki amua kufanya kitu kwa kumaanisha nini unataka,Amua kujifunza na kutumia maarifa hayo kama mwongozo wa hatua zako za mafanikio,Amua kutoa ghalama za kuwapata watu sahihi kufikia mafanikio yako
Tuma ujumbe BIG KEY OF SUCCEASFULL2017 kwenda 0715222979/Email.errynine6@gmail.com
Uungamishe na WhatsApp group kwa mafunzo zaidi BURE.
Rafiki nikutakie siku njema na yenye mafanikio zaidi.
Na wako rafiki katika mafanikio
Ernest Lwilla
Chapisha Maoni