Nitumaini langu unaendelea vema na shughuli zako za kila siku ambapo unaamini kuwa ndiyo njia sahihi itakayo kufanya upige hatua kimafanikio na hivyo ndivyo unavyo takiwa kufahamu kuwa hakuna mafanikio utakayo yapata pasipo kufanya kazi.
Karibu tujumuike pamoja kwa kujifunza mambo kadhaa muhimu juu ya kufanya baada ya matokeo makubwa kutoka Google.
Dunia ya sasa huwezi kuifananisha na dunia ya miaka ya nyuma ambapo kupata taarifa za jambo fulani ilihitaji utumie nguvu nyingi tofauti na leo ambapo kila unacho kitaka kwa wakati wowote,Popote unakipata,
Chochote unakacho taka kujifunza utajifunza tu pasipo kipingamizi chochote Hii ni kutokana kutanuka kwa Sayansi na Tekinolojia ndiyo iliyo lahisisha mambo kiasi hiki.
Kwanini nasema haya??
Leo hii ukihitaji kujua chochote kwenye kundi la watu wengi utaambiwa nenda kasearch GOOGLE,
Hivyo kwa lugha nyepesi tunaweza kusema mtando huo unamajibu ya kila kitu unacho kitaka.
Swali la kujiuliza Nani anayatoa majibu hayo kupitia mtandao huo??
Dunia imebadilika sana kiasi kwamba kila kitu kinacho fanywa na watu sehemu yoyote ile kinahifadhiwa kwa njia ya Internet hasa kupitia mitandao mbalbali zikiwemo BROG.
Watu wengi wanashirikisha mambo yao kwa njia hiyo na hatimae unapo enda Google na kutafuta chochote mtandao huo hutafuta maandiko yaliyo andikwa na watu kupitia mitandao ya jamii na blugu mbalimbali ndiyo maana inakuwa rahisi watu kukwambia nenda katafute Google.
Rafiki urahisishwaji wa matokeo ya google sio sababu ya kutosha kuyafanyia kazi moja kwa moja mafundisho hayo kwa sababu washirikishaji wapo maeneo tofauti ambapo muda mwingine masomo hayo hayawezi kukupa matokeo aliyo kupa mshirikishaji,
Inaweza kuwa mazuri au mabaya.
Unapaswa kuchukua tahadhari dhidi ya mafundisho utakayo jifunza huko kwa kuingia hatua ya kujifunza kwa watu wanao fanya kwa vitendo kitu ulicho jifunza hasa waliopo mazingira uliyopo,
Na kama utatumia matokeo moja kaa moja utatakiwa kuwa karibu na wataalamu wa hicho unacho fanya hasa waliopo maeneo ambayo wewe upo.
Sisemi matokeo ya kujifunza kupitia mtandao wa internet ni mabaya lakini lazima ufanye utafiti wa kutosha dhidi ya matokeo hayo,
Hapa unaweza kuchukua mawasiliano ya mshirikishaji wa somo husika na kufanya nae mazungumzo ya kina juu ya somo alilo kushirikisha ikiwa nipamoja na kuuliza maswali muhimu utakayo kuwa nayo.
Mfano:Umejifunza kilimo cha matikiti kupitia maandiko ya washirikishaji kupitia google nawe pasipo kufanya utafiti ukachukua kianzio/pesa zako na kuweka shambani pasipo kuwa na taarifa sahihi za kilimo hicho hasa maeneo uliyopo na mwisho mavuno yakawa tofauti na ulicho aminishwa kwenye maandiko ya Google Utamlaumu nani??
Kwa matokeo hayo utamlaumu mshirikishaji kupitia mtando huo,
Lakini ukweli Unakila sababu ya kujilaumu wewe mwenyewe au kuona matokeo hayo ni sehemu ya kujifunza kilimo hicho.
Vinginevyo tunasema umepotezwa na teknolojia yaani haijakusaidia kukupa matokeo unayo yataka wewe au uliyo yategemea na hiyo imetokana na uzembe ulio fanywa na wewe.
Rafiki nikupe siri hii,
Masomo ya kujifunza Google yawe ni sehemu ya kukufungua akili juu ya kitu chochote husika unacho taka kujifunza au kufanya.
Pia fahamu kuwa waandishi wa masomo hayo sio wote wanafanya kilimo hicho ila wengi ni wakukopi na kusambaza kwenye mitandao wanayo tumia kwa matokeo makubwa ya kupata likes,share na comments,
Hivyo unakila sababu ya kutafuta taarifa sahihi kwa watu sahihi unao amini wanafanya kitu hicho kwa usahihi na hapo ndipo utapata matokeo sahihi.
Rafiki usipotezwa na matokeo ya teknolojia inayo kuwa kila siku,
Maana utakae pata maumivu ni wewe na sio Google.
Tuma ujumbe mfupi BIG KEY OF SUCCESSFULL2017 kwenda 0715222989/Email:errynine6@gamial.com
Uunganishwe na group la WhatsApp BURE.
Rafiki nikutakie siku njema na yenye mafanikio zaidi,
Na wako rafiki katika masomo haya
Ernest Lwilla
Chapisha Maoni