Habari rafiki na msomaji wa mtando huu wa Ufunguo wa mafanikio,
Nitumaini langu kuwa u mzima wa afya njema kabisa,
Karibu rafiki siku hii ya leo nimependa zaidi tushirikishane na tujifunze pamoja juu ya sifa kuu mbili (2) za changamoto katika maisha yetu ya kila siku na usipo zifahamu vizuri huwezi kupiga hatua yoyote kimafanikio,
Nasema hivi kwa sababu jamii zetu kwa sehemu kubwa changamoto wanaziona kama sumu kwenye kazi zao na hivyo mala zote wanafanya juhudi kubwa namna ya kuzikwepa jambo ambalo ni hatari zaidi.
Rafiki changamoto ni DARAJA,
Changamoto ni DARASA lakini ni kwa namna ambayo changamoto itakufikia na utakavyo ichukulia mbaya zaidi unatakiwa kufahamu kuwa changamoto mala zote zinabisha hodi kwa mambo madogo madogo ambayo mala zote uwa yana puuzwa mpaka pale lita kapo kuwa jambo kubwa ndipo kuona kama tatizo,
USIPO ZIBA UFA UTA JENGA UKUTA.
Rafiki sipendi nikuchoshe lakini hiyo ndiyo hali halisi tunayo kutana nayo kwenye mafanikio yetu.
Changamoto zina sifa nying sana lakini hii leo nitakushirikisha mbili tu,
Ambazo mimi binafsi nimejiona na kujifunza kupitia uwepo wake.
1.Changamoto Zinafundisha na kukufikirisha kwa usahihi.
Jambo ambalo ungeamua kwenda darasani ukatoe ghalama za kujifunza tena kwa muda mrefu basi kupitia Changamoto utajifundisha pasipo malipo ila kwa kukufikirisha zaidi,
Yaani pindi ukutanapo na changamoto na ile hatua ya kufikiri njia sahihi ya kutatua ile changamoto unakuwa tayari Umefikirishwa na Kujifundisha mwenyewe na kuijua kazi kazi unayo fanya,
Kivipi?
Fahamu kuwa bila changamoto usinge fikiri chochote na kwa maana hiyo ungekuwa hujaongeza kitu chochote cha kukifahamu kwenye hiyo kazi yako.
Changamoto ndiye mwalimu bora kuliko wote duniani kwa sababu ukiwa katika shughuli yako hapo ndipo changamoto inapo tokea,
Kwa maana hiyo ukiwa huna kitu cha kufanya huwezi ukajifunza maana huna kitu cha kukupa changamoto ili zikufindiahe.
2,Changamoto ndiyo inayo kutoa kwenye hatua ndogo kwenda kubwa zaidi (Changamoto ni Daraja).
Ukiwa unaendelea na shughuli zako na hujakutana na changamoto yoyote basi hapo utafanananishwa na mtu alie katika usingizi mzito,
Hivyo anahitaji mtu mwingine aje amwamshe na ndipo atambue anaelekea wapi??
Ukiona mtu amepiga hatua kwenye chochote anacho fanya basi ujue changamoto ndiyo iliyo mvusha hivyo isinge kuwa changamoto isinge kuwa rahisi kuenda hatua kubwa zaidi.
Amani Makirita anaizungumzia changamoto kama sehemu ya mafanikio makubwa kwa mtu yeyote kwenye kazi zake lakini ni pale atakapo weza kuipatia njia sahihi ya kutatua
"Anazungumza" Changamoto ndiyo mafanikio kwa sababu amejifunza mengi na kufikia hatua kubwa zaidi kwani mafanikio yote aliyo nayo ni matokeo ya kuzipita changamoto.
Je unadhani kuzikwepa changamoto ndiyo njia sahihi kufikia mafanikio yako??
Je nini thamani ya changamoto kwenye mafanikio yako??
Mabilionea wote unao wafahamu na wengine unao wasikia ni watu walio pambana na kuzishinda changamoto hapo ndipo chanzo cha wewe kuwa fahamu na wasinge pambana basi hata wewe usinge wafahamu,
Haitoshi mpaka sasa bado wanakutana na changamoto kubwa zaidi ambapo kama wasipo weza kuzieewa na kuzifurahia basi mafanikio hayo yasinge baki kwao.
Mwisho rafiki unatakiwa uwa chanya zaidi kwa kufikiri njia sahihi ya kutatua changamoto hata kabla hujafikiri kuzikwepa kwa namna yoyote,
Maana kama utazikwepa changamoto basi utafanya mambo mengi sana pasipo kufikia hatua ubayo tamani kufika.
Changamoto ni uamsho wako katika kuendelea kuwa makini dhidi ya jambo unalo lifanya.
Tuma ujumbe mfupi Big Key Of Successfull2017 kwenda 0715222989/Email:errynine6@gmail.com
Uunganishwe na group la WhatsApp BURE.
Rafiki nikutakie siku njema na yenye mafanikio zaidi.
Na wako rafiki katika mafanikio
Ernest Lwilla.
Chapisha Maoni