Unknown Unknown Author
Title: Usifikiri Ufanye Nini Ila Jiulize Kwanini Ufanye??
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari mwanamafanikio mwenzangu kupitia ukulasa huu wa Ufunguo wa mafanikio , Nitumaini langu kuwa unaendelea kuongeza juhudi na kuzidi k...

Habari mwanamafanikio mwenzangu kupitia ukulasa huu wa Ufunguo wa mafanikio,
Nitumaini langu kuwa unaendelea kuongeza juhudi na kuzidi kuwa bora zaidi ya hapo ulipo.

Rafiki ni siku nyingine iliyo njema ambapo nimepata nafasi ya kukushirikisha Maswali mawilk muhimu ambayo unatakiwa kujiuliza kabla huja chukua hatua ya kufanya unacho fikiria kufanya.

Yapo maswali mawili muhimu ambayo ukipata kujiuliza kabla huja chukua maamuzi yoyote juu ya wazo lako itakusaidia zaidi,
Maswali haya ni i
/Nifanye nini?
ii/Kwanini nifanye?

A/Nifanye Nini??
Rafiki imekuwa ni kawaida kwa watu wengi sana kuniuliza Swali hili,
Ernest Nina laki moja nifanye biashara gani??
Na majibu yangu mala zote uwa namuuliza Wewe umefikiri kufanya nini??
Hapa nimekuwa nikipata mitizamo ya watu wengi sana juu ya hatua wanazo chukua kwenye jamii zao.

Watu wengi wanatoa sababu ya kuwa mtaji huo hautoshi kufanya chochote kwenye mazingira yao,
Ukweli ukiwa na sababu ya kufanya jambo lolote lile Laki moja ni kianzio kikubwa sana,
Kwa maana ya kujua unataka ufanye nini??
Kwanini ufanye hicho?? Unanini mkononi??.

Watu wengi wanafikiri kuanza na mitaji mikubwa sana ndiyo mafanikio lakini Mafanikio ni kuwa na sababu ya kufanya chochote unacho fikiri kufanya ila usivunje sheria.

B/Kwanini ufanye hicho??
Sababu ya kufanya unacho fikiri kufanya ndiyo mwongozi mkubwa wa mafanikio yako katika hicho unacho fikiri kufanya,
Ukiwa na sababu ya kufanya jambo fulani huwezi kutoa sababu yoyote ya kuto anza kufanya eti kwasababu huna mtaji,
Nini maana ya mtaji??
Ni muhimu ujue binadamu kuwa tuna aina nyingi za mitaji Mf:Mtaji wa nguvu,Mtaji wa kipaji,Mtaji wa muda,Mtaji wa watu na Mtaji wa Fedha.

Watu wengi uwa tunafikiri tu juu ya Mtaji wa Fedha lakini kwa sehemu kubwa tunakuwa hatuna sababu ya kuwa na Mtaji wa Fedha,
Hivyo hata tunapo pana Pesa tunazipoteza bila kufanya mambo ya msingi katika maisha yetu.

Hivyo rafiki jua kusudi la kutaka kufanya hicho unacho fikiri kufanya,
Jua sababu ya kwanini ufanye hicho ndipo ujue unaanzia wapi kutokana na aina za mitaji niliyo kuorodheshea hapo juu,
Maana unaweza kuhitaji mtaji wa fedha kumbe kusudi lako linahitaji mtaji wa nguvu hivyo pesa ukaiharibu na kuipoteza pasipo kuwa na mpangilio mzuri.

Hivyo rafiki usijiulize ufanye nini?? Ila tambua kusudi la kufanya unacho fikiri kufanya,
Hapo ndipo utapata mwongozo mzuri wa kufanya na kuweka juhudi zaidi ya vile ambavyo ulifiki awali,
Zaidi utambue kuwa mtaji sio pesa tu bali inategemea kusudi lako linataka ufanye nini??
Mfanikio unayo hitaji yapo hapo ulipo ila ni lazima utambue sababu ya kufanya hicho unacho fikiri kufanya.

Bila shaka umesha pata kusudi la kutaka kufanya chochote kile na umesha tambua nini kinahitajika ili kufanikiwa kwa wazo hilo,
Je ni watu? Je ni Nguvu? Je ni muda??
Kama jibu ni pesa basi huna sababu ya kujiuliza maswali mengi ufanye nini??
Ila chukua hatua kwa kile ulicho shika mkononi mwako.
Hicho ndicho kianzio sahihi kuanza kujenga wazo lako.

Tuma ujumbe mfupi Big Key Of Sucvessfully2017 Kwenda 0715222989/Email:errynine6@gmail.com
Uunganishwe na group la WhatsApp BURE.

Rafiki nikutakie siku njema sana na yenye mafanikio.
Ulikuwa nami ragmfiki yako katika mafanikio

Ernest Lwilla

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top