Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa ufunguo wa mafanikio,
Nitumaini langu kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu.
Karibu rafiki tukifunze na tushirikishane jambo hili muhimu ambalo ndo daraja kubwa tena salama kutufikisha kwenye mafanikio yetu,
Zipo njia nyingi zenye kukupa mafanikio kwa haraka lakini njia hizo sio salama zaidi ifahamike vitu vinavyo patikana kwa urahisi hata kupotea kwake ni rahisi vivyo hivyo,
Hivyo inabaki kuwa njia sahihi ni moja tu ambapo ni KUFANYA KAZI KWA BIDII,
Asiku danganye mtu kuwa kuna njia rahisi ya kufikia mafanikio yako hapo ujue utakuwa umeingizwa mjini.
Maisha yoyote wanayo ishi watu wote ni matokeo mazuri ya kufanya kazi,
Lakini upo utofauti mkubwa wa kufanya kazi na kufanya kazi kwa bidii yaani mtu anae fanya kazi anauhakika wa kuendeaha maisha pasipo wasiwasi wowote lakini Ni watu wechache wanao fanya kazi kwa juhudi na hao ndio wanao miliki uchumi mkubwa wote unao uona.
Rafiki Fanya kazi,
Lakini sio kwa kufanya kazi tu lazima ufanye kazi kwa juhudi hapo ndipo utakuwa na utofauti na wengine ambao wanafanya kazi kwa ukawaida na kupata matokeo yaliyo ya kawaida,
Ili uwe tofauti na uwe na matokeo makubwa ni lazima Ufanya kazi kwa juhudi zaidi ujifunze namna bora ya kufanya au kuifanya pesa itumike kuzalisha zaidi.
Ifanye pesa yako kuwa mtumwa wa kukuzalishia pesa zaidi ya unavyo izalisha wewe,
Ikiwa utafanya kazi kwa bidii ni lazima ujifunze namna bora ya kuikuza pesa yako ujue ni wapi unaweza kuweka pesa yako na ikazidi kuwa salama zaidi na hatmae kukua zaidi.
Yaani ona namna gani watu wataikuza biashara na pesa yako yaani kwa kuona wapi kutaupungufu nawe kuweka nguvu yako hapo.
Zipo namna nyingi za kufanya kazi kwa juhudi lakini namna iliyo bora zaidi ni KUWEKEZA,
Ambapo pesa yako itakuwa ikijizalisha kupitia uwekezaji huo hata pasipo wewe kuwepo,
Amani Makirita ana sema anauwezo wa kukopa mkopo lakini mkopo huo ni ule ambao hata urudisha yeye,
Kwa maana ya kwamba achukue mkopo na kisha kuwekeza na watu wengine wazalishe kupitia uwekezo wake.
Rafiki kufanya kazi kwa juhudi ndiyo njia peke ya kukufikisha kwenye mafanikio yako yaliyo halali na uhakika,
Tofauti na hapo hayo sio mafanikio bali ni Mwonekano wa mafanikio feki.
Rafiki kwa siku hii nilikuwa nikikushirikisha njia bora ya kukufikisha kwenye mafanikio yako njia hii ni KUFANYA KAZI KWA JUHUDI,
Rafiki fanya kazi kwa juhudi maana hakuna njia nyingine zaidi.
Tuma ujumbe mfupi BIG KEY OF SUCCESSFULLY2017 kwenda 0715222989/Email:errynine6@gmail.com
Uunganishwe na group la WhatsApp BURE.
Rafiki nikutakie siku njema zaidi na yenye mafanikio,
Ulikuwa na wako rafiki katika mafanikio
Ernest Lwilla
Chapisha Maoni