Unknown Unknown Author
Title: Hongera JPM Kwa Jambo Hili Muhimu Kwa Mafanikio Makubwa Ya Watanzania.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitaia mtando huu wa UFUNGUO WA MAFANIKIO, Nitumaini langu tunaendelea vema na shughuli zetu za...

Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitaia mtando huu wa UFUNGUO WA MAFANIKIO,
Nitumaini langu tunaendelea vema na shughuli zetu zaidi tukizidi kufanya makubwa  ambayo tulijiambia tutayakamirisha mwaka huu.
Rafiki hii ni siku nzuri sana na hivyo ni wajibu wetu kwenda kuweka juhudi zaidi ili kupata matokeo yaliyo bora zaidi.

Karibu tujifunze pamoja juu ya salamu zangu kwa Mh John Pombe Joseph Magufuli JPM,
Ambapo amekuwa ni Kiongozi pekee alie wapa watanzania sura mpya ya kufikiri zaidi Jambo moja ambalo ni kubwa hasa kwa Wajasiriamali,Wafanya biashara,Watumishi na makundi mengine yote.

Jambo hili ni NIDHAMU,
Sijajua kama ni nidhamu ya kweli au ni ya woga lakini kwa hili Mh anastahili pongezi,
Maana watanzania sasa wengi tumekuwa wachapa kazi hatutegemei tena maisha ya miujiza na kisha mtu uishi kwa kuto fanya kazi.

Watanzania sasa wananidhamu iliyo ndani ya mafanikio makubwa kwa wachache walio tambua nyakati na kutumia fursa hii kuzalisha,
Ingawa bado kwa baadhi ya watanzania wanalalamika Maisha yamekuwa magumu kwao.
Rafiki usiwe miongoni mwao hao wanao lalamika kutwa maisha magumu huku wakiwa wamenyoosha miguu.

Nidhamu waliyo nayo sasa Watanzania kwa sehemu kubwa ni kama zifuatazo.
Nidhamu ya Uwajibikaji,
Wengi sasa hawana visingizio tena vya kuto wajibika zaidi wanafanya kazi ndipo waingize kipato na kufanya waishi,
Kwa nyakati hizi hakuna tena Mazungumzo zaidi ya watu wengi kuchukua jukumu la maisha yao na kuwajibika kwa 100%,Hakuna uzembe wa watu katika nyanja mbali mbali za utumishi wa Uma zaidi wanafanya kazi,Hakuna tena mbada wa kuingiza kipato zaidi ya kufanya kazi ndipo uweze kuzalisha.

Nidhamu ya Fedha,
Wengi wamelazimika kujifunza na kufanya usawa wa Mapato na Matumizi,
Kwa sababu hii hakuna mtu anae chezea fedha bila utaratibu kwa sababu upatikanaji wake umekuwa ni mgumu na nilazima mtu ufanye kazi kwa juhudi hapa Utawasikia Wakisema ""Usawa wenyewe wa Magufuli huu""
Ukweli watu walijisahau kwenye habari ya mapato na matumizi maana kulikuwa na namna nyingi ya kufidia thamani ya fedha walizo poteza kwa mambo yasiyo ya ulazima.

Nidhamu ya Muda,
Watanzania wengi sasa wanatambua thamani halisi ya muda wao na hivyo hawaupotezi muda wao pasipo msingi maana ikiwa hawato tambua thamani ya muda wao hawaweza kuingiza kipato cha aina yoyote,
Watanzania sasa wanatambua misingi ya uwekezaji mkubwa kwenye muda wao.

Nidhamu ya kufanya chochote kwa ubora.
Ipo hali ya mtu kufanya jambo kwa hovyo hovyo na akaliingiza sokoni na likapata wanunuzi lakini kwa sasa hali hiyo imekuwa tofauti maana usipo zingitia ubora bmhuduma yako inakosa wanunuzi.
Na hivyo kama itakosa wanunuzi ulipaji wa kodi utakuwa mgumu kwa sababu hakuna mauzo na hivyo tiba imekuwa ni watu kufanya kwa ubora ili wapate wanunuzi.

Rafiki haya ni machache kati ya mengi ambayo yametiliwa mkazo zaidi kwenye maisha ya Watanzania na hivyo kuwa na NIDHAMU YA HALI YA JUU katika nyanja zote za maisha Hongera JPM.

Rafiki mwisho kabisa nitete kitu nawe ambae bado hujatambua mfumo unao takiwa kwenda nao ili uondokane na kulalamika maisha magumu,
Awali ya yote Maisha magumu ndiyo desturi yake kwenye maisha ya bibadamu kwa sababu sijawai kusikia watu wakisema maisha sasa yamekuwa rahisi.
Pili hali duni ya maisha inaletwa na UVIVU au Kuto kuwa na nidhamu binafsi katika mfumo wa maisha yako.
Huwezi ukategemea kuvina mazao mengi kama hujaweka juhudi katika kile unacho tegemea kuvuna.

Ninakupa siri,
Wakati baadhi ya watu wakilalamikia Hali ngumu ya maisha,
Ifanye ni fursa kwako katika kutatua matatizo yao kwasababu hawawezi kuvuna maneno pasipo kuweka juhudi ya kazi.
HAPA KAZI TUUUU!!
Lazima ufanye kazi ndipo uweze kupata unacho kitaka,
Weka kazi mbele na maneno weka kando upate matokeo unayo yataka.
Work! Work! Work!
Work hard!Work hard!Work hard!
Hiyo ndiyo kanuni ya mafanikio unayo yataka.
Hongera JPM.

Tuma ujumbe BIG KEY OF SUCCESSFULLY2017 kwenda 0715222989/Email:errynine6@gmail.com
Uunganishwe na group la WhatsApp BURE.

Nikutakie siku njema na yenye mafanikio zaidi.
Na wako rafiki katika mafanikio

      Ernest Lwilla.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top