Unknown Unknown Author
Title: Soma Hapa Umuhimu Wa Kugusa Maisha Ya Wengine,Hapo Ndipo Chanzo Cha Utajiri Kilipo.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Hongera rafiki kwa siku hii njema, Karibu na endelea kutembelea na kujifunza zaidi kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa mafanikio, Natumaini ...

Hongera rafiki kwa siku hii njema,
Karibu na endelea kutembelea na kujifunza zaidi kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa mafanikio,
Natumaini huto toka mtupu kama ulivyo ingia hapa.

Karibu tujadimu faida na umuhimu mkubwa wa kuwa msaada kwa maisha ya watu wengine na namna unavyo weza kunufaika kutokana na hali hiyo.

Siri kubwa ya matajiri wa kubwa Duniani ipo hapa kwenye kugusa maisha ya watu wengine,
Siri kubwa ya kupata wazo bora la biashara ni kugusa maisha ya watu wengine,
Siri ya mtu yeyote kuwa maarufu hapa duniani ni kugusa maisha ya watu kwa namna yoyote ile.

Wapo watu ukiwa sikia wakiongea juu ya utajiri utadhani ni kitu kidogo sana na nikitendo cha kulala na kuamka tu,
Lakini ukweli ni kwamba ni ngumu sana kufikia mafanikio yako kama huta weza kugusa maisha ya wahitaji,
Utasikia Kutengeneza pesa kwenye mtandao mkubwa wa Internet lakini kama huna namna ya kuwagusa watu kwenye maisha yao utaishia kuwa laumu watu juu ya jambo hilo.

Nateta na wewe rafiki,
Ukiona mkutano mkubwa wa matajiri wakubwa umeketi mahara ujue mada kubwa itakayo jadiliwa hapo ni CHANGAMOTO ZA MAISHA YA WATU NA UTATUZI WAKE.
Hii ni kwa sababu ni ngumu sana kwenda kuchukua pesa kwa wahitaji wa jambo fulani pasipo kuwasaidia au kutatua changamoto inayo wakabili.

Ona hapa ukisha ona changamoto ya jamii fulani na kuchukua jukumu la kuwasaidia hapo unakuwa sawa na kupitisha daftari la mchango wa hiyari kukuchangia utajiri wewe maana hapo kila mmoja ataona namna ya kupata huduma yako ili aepukane na changamoto husika.

Mfano:Ipo shida kubwa ya Mwanga vijijini Je unadhani makampuni yaliyo liona hilo na kupeleka huduma ya mwanga wanatengeneza pesa kiasi gani?
Eg:Solataa & M_Kopa na makampuni mengine mengi.

Je walio tambua fursa ya kupeleka masomo ya semina za ujasiriamali mikoani wametengeneza shilingi ngapi?
Je walio ona fursa ya kutoa mafunzo mbalimbali kwa njia ya internet wanatengeneza shilingi ngapi?
Je walio ona uhaba wa mayai ya kienyeji na kuona namna ya kuzalisha mayai ya kisasa ambayo ndo yanayo tumika kwa sehemu kubwa sasa wanatengeneza kiasi gani cha fedha?
Rafiki hi ni mifano michache tu niliyo kupa lakini ipo mingi sana.

Rafiki Utajiri mkubwa upo kwenye matatizo ya watu wa jamii fulani tena hii ni kwakila mmoja kwenye nafasi yake ya utafutaji watu wanamatatizo lukuki na hawana namna ya kuyatatua Je unaonaje  kuchukua hatua ya utatuzi??

Ikiwa utayaogopa matatizo ya watu basi huwezi kufikia hatua unayo itaka wewe,
Ikiwa huto ona namna ya kutatua matatizo ya watu wa jamii yako basi huwezi kufika lengo lako kwa kiwango cha ukubwa wa ndoto yako.

Ninacho kushauri hapa ona namna ya kugusa maisha ya wahitaji kwa njia ya namna yoyote ile,
Ona namna ambayo utaanza kuweka thamani kwenye maisha ya watu na watu hao wakinufaika na mchango wako watakuwa tayari kutoa ghalama kwako.
Rafiki wazo ili liwe bora ni lazima liweze kutatua tatizo la watu wanao kuzunguka au jamii ya watu fulani.

Tambua kuwa kila hitaji unalo lifurahia sasa ujue ni mawazo ya watu fulani walio tumia muda wao na kuona namna ya kuweka thamani kwenye maisha ya wengine,
Hivyo nawe ona namna utakavyo gusa maisha ya watu wengine.

Tuma ujumbe Big key of successfully2017 kwenda 0715222989/Email.errynine6@gmail.com
Uunganishwe na gproup la WhatsApp BURE.

Rafiki nikutakie wasaa mwema na kutafakari utafanya lipi kuyapa thamani maisha ya wahitaji.
Na wako rafiki katika somo hili.

Ernest Lwilla

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top