Unknown Unknown Author
Title: Mambo 5 Muhimu Unayo Takiwa Kuacha Ili Ufikie Mafanikio Makubwa
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na mpenzi msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa Mafanikio,Nitumaini langu unaendelea vema na unayafanyia ka...

Habari rafiki na mpenzi msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa Mafanikio,Nitumaini langu unaendelea vema na unayafanyia kazi masomo haya ili kuwa msaada wa kweli kwenye safari yako ya mafanikio.

Karibu tushirikishane mambo yaliyo muhimu zaidi kwenye maisha yetu ili kufikia hatua tunazo zitamani kimafanikio,
Kwa awali Binadamu wengi tumekuwa tukikwamishwa au kujikwamosha kwa mambo ambayo sio ya lazima wala sio muhimu kwetu.
Hii imekuwa ikipelekea watu wengi kuto piga hatia kimafanikio,
Hii leo nimekuandalia mambo ambayo ukiamua leo hii kuyafanyia kazi lazima upige hatua kwa namna yoyote ile kimafanikio.
Nifuatilie

1.Acha Kuahirisha mambo,Hii ni moja ya sababu kubwa kati ya zilizo nyingi zimazo wafanya watu wengi kuto piga hatua zaidi kimafanikio,
Rafiki kama na wewe ni miongoni mwa watu wanao ahirisha kufanya mambo basi kufanikiwa inaweza kuwa kazi ngumu kwako kama ilivyo rahosi kuahirisha mala nyingi.

Mf:Kunamambo ambayo ulijiambia utayafanya muda fulani lakini unapo fika muda huo haufanyi lile na badala yake ubafanya jambo jingine tofauti na lengo lako,
Ulipanga kukamilisha jambo fulani lakini unapo fika muda huo haufanya na kusogeza muda mbele yaani muda wote unakuwa huna dedline iliyo ya kweli kwenye maamuzuzi yako.
Hivyo huwezi kufanikiwa ikiwa utakosa msimamo na heshima ya mambo uliyo jipangia mwenyewe ni lazima uheshimu jambo lolote na ulifanye kwa mda mwafaka.

2.Acha Uvivu,Uvivu ni kikwazo kingine kinacho warudisha watu nyuma yaani watu wengi hawapendi kufanya kazi huku wakitaka matokeo makubwa na yaliyo bora,
Pia wengine huanza kwa juhudi kubwa na wakijituma zaidi lakini wanapo fikia hatua inayo wawezasha kujikimu hupunguza juhudi na wengine kulizika kabisa na kuona hakuna mafanikio zaidi ya pale,
Wengi hujiambia kuwa nipumzike maana maana nilipo toka ni mbali na mazoea yakisha jenga tabia Uvuvi kwake inakuwa na kawaida hapo wengi hutengeneza heshima ya kuwaonuesha wanamafanikio makubwa,Rafiki ili ufikie  kwenye mafanikio makubwa ni lazima uwe na juhudi kama ndo kwanza una anza leo kutafuta,
Rafiki ukitaka mafanikio yakufuate ni lazima uache Uvivu,Acha uvivu na fanya kazi kwa juhudi.

3.Acha Matumizi mabaya ya Fedha,Wengi huweza kujibana na wakijaribu kiweka vitega uchumi vya kila namna vitakavyo ongeza pato lao lakini baada ya muda fulani Wanaanza kupunguza ari na kuanza kutumia ovyo fedha zao huku wakitumia misemo inayo watia moyo Mf:Tunakula ujana,Maisha yenyewe ndo haya haya,Wakufanikiwa zaidi nitakuwa mimi,
Kwa mfumo huu mtu anakuwa hana tena machungu wala kukumbuka maumivu aliyo yapitia kabla hajaipata fedha anayo itumia hovyo kwa wakati huo.
Lakini pia wapo watu ambao bado hawana fedha lakini matumizi yao ni Ovyo Utawasikia siwezi kujibana wakati fedha za kula ninazo,Maisha yenyewe ni haya,Tunaishi mala moja
Kwa kauli hizo mtu anakuwa amesha jikatia tamaa mapema na haoni tena faida ya kuweka akiba wala kuwekeza kwa mafanikio ya baadae.
Rafiki tumia vizuri fedha zako.

4.Acha kufikiri hasi,Mafanikio ya mtu yeyote ni mtizamo wake juu ya kile anacho kiamini na kukifanya kwa wakati huo,
Lakini ikiwa unahitaji kufikia mafanikio makubwa zaidi lazima akili na mawazo yako yawe chanya ufanye kazi kwa mtizamo unao uamini zaidi katika kila unacho fanya,
Mtizamo ndiyo matokeo unayo yaona kwa watu wengi na ikiwa utajiwazia mambo mengi kwa mtizamo hasi huwezi kufanikiwa kwa jambo lolote lile,
Hivyo rafiki Waza chanya,Tenda Chanya na Matokeo yatakuwa Chanya.

5.Acha kujilinganisha na wengine,Kosa lingine kubwa linalo fanywa na watu wengi ni kujilinganisha wa watu wengine,Kuona wao kama wanafanana na wengine,Kuona wao wana uwezo mdogo kuliko wengine,
Hii ni sumu inayo ua ndoto za watu wengi sana hasa mtu anapo fikiri mbona Juma alifanuya akashindwa basi na yeye anajipa matokeo ya kushindwa hata kabla hajafanya chochote kwenye maisha yake.
Rafiki unaanzaje kujifanisha na mtu mwingine,Unaanzaje kujipima uwezo wako,Unaanzaje kujipa hofu??

Mtu nambari moja anae kujua wewe ni Wewe,
Mtu nambari moja anae ya jua mapungufu yako ni Wewe hivyo ukisha jilinganisha unakuwa sawa na mtu alie amua kujiua huku anatembea anaji alafu anajipima na uwezo wa watu wengine huku akiwa ameuacha uzuri wake.

Mwisho kabisa acha kujikatisha tamaa kwa kuona huwezi chochote,
Tamaa ni marufuku kukata mpaka pale utakapo zimiwa mpumzi lakini licha ya watu kuendelea kuishi na maisha yakiendelea lipo kundi la watu kubwa linalo angamia kwa kukataa tamaa,
Inawezekana umeweka juhudi kubwa mala nyingi na juhudi hiyo haikuzaa matunda,
Inawezekana umeshindwa mala nyingi na pasipo kupata matokeo mazuri,
Inawezekana umezulumiwa mala nyingi kiasi kwamba ukaona haiwezekani tena,
Kupitia hali ya namna tofauti huwapelekea watu kukata tamaa na kuona haiwezekani tena kwao.

Lakini ukweli upo hivi Bila shaka ulisha wai kupoteza ufunguo na ukautafuta kwa mda mrefu bila kujua ulipo na mwishoni ukiwa umechoka sana Unaukuta ufunguo sehemu ambayo hukutegemea au ulisha itafuta na hukuukuta,
Unaweza kuwa umefanya mambo mengi sana na bila kupata matokeo mazuri ambayo ulitegemea kabla hujaanza jambo hilo na baadae ukaahirisha kabisa kuendelea kuumiza nguvu zako na baadae ukafanikiwa,
Hiyo yote ni kwasababu huwezi kupewa kama ulivyo fikiria,Huwezi kuthamini kama utamipata bila jasho,Huwezi kujua thamani kama huto umia,
Kitu kizuri chochote kinakuja kwa maumivu na kwa kuweka juhudi kubwa zaidi.

Rafiki bila shika umejifunza mambo mengi yatakayo kusaidia ikiwa utaamua kuyafanyia kazi kiufasaa ni lazima upige hatua.

Tuma ujumbe Big key of successfull2017 kwenda 0715222989/Email.errynine6@gmail.com
Uunganishwe na group la WhatsApp BURE.
Nikutakie kila la heri rafiki na  wako rafiki Ernest Lwilla

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top