Unknown Unknown Author
Title: Fanya Kitu Hiki (1) Kumfanya Mteja Awe Wa Kudumu Kwenye Biashara Yako
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na msomaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio, Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima wa afya njema kabisa kama ilivyo kwangu...

Habari rafiki na msomaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima wa afya njema kabisa kama ilivyo kwangu na hivyo kuendelea na mapambano ya kufikia mafanikio yako makubwa.

Nitumie fursa hii kukukaribisha kwenye makala yetu ya leo ambapo tutaenda kushirikishana jambo moja lililo na thamani kubwa kwa mteja wako na kumfanya mteja arudi mala zote kufuata huduma,
Kimsingi yapo mambo mengi yanayo wavutia wateja kwenye biashara zetu na hatmae kuwa wateja wa kudumu kwenye biashara zetu.

Lakini lipo jambo moja linalo saulika na hivyo linapo mtokea mteja au mnunuzi wa huduma yako kuto rudi tena kufuata huduma,
Jambo hili linafanya biashara nyingi kuwa na wateja wengi lakini wasio wa kudumu kwenye uteja,
Kiasi ambacho kila siku unakuwa na wateja wapya ambao bado hawajaujua mfumo wa biashara yako.

Karibu na unifuatilie,
Jambo hili ni WEWE KUWA SEHEMU YA HASARA AU CHANGAMOTO ANAZO PITIA MTEJA WAKO,
Je unahusika vipi na hasara anayo ipata mteja wako hasa inapo kuwa imechangiwa na mfumo wa biashara kwa ujumla??
Je unato mchango gani pindi mteja anapo kutana na changamoto zinazo changiwa na mfumo wa biashara??,

Rafiki hakuna jambo ambalo halikuhusu kwenye biashara unayo ifanya,
Na ukiwa na mtizamo huo ujue hujaamua kuwa sehemu ya hasara au changamoto ya mteja wako.

Wateja wengi wanakata mguu wa kufuata huduma zako pindi wanapo pata hasara inayo jirudia kwenye biashara ambayo wewe unawasambazia au kuwafikishia walipo,
Wateja wengi wanakata mguu wa kufuata biashara yako pindi wanapo kutana na changamoto nyingi na wanapo kushirikisha unakuwa huna mchango wowote kwao.

Mfano mkubwa ni kwa wale watoa huduma/Wafanya biashara wa vyakula,Au huduma zinazo haribika,

Mfano,Mimi ninatoa huduma za kusambazo mayai mji mzima, Ambapo mteja anaweza kununua trey 50 na kwenye kila trey unakuta kuna mayai 5 yameharibika eitha kwa kukaa mda mrefu na hivyo mteja anapo rudisha mrejesho wa hasara ya mayai 25 kwenye trey 50.
Nimekuwa nikiifidia hasara hiyo kwa kugawana nae kiasi cha hasara,
Pia nimekuwa ninapo agiza mzigo nawapo taarifa waweke na fidia yahasara inayo patikana kwa mnunuzi wa mwisho au mteja wangu.

Kwa kufanya hivyo nimekuwa na wateja wengi sana na wanao rudisha mrejesho na maendeleo ya biashara zao na hata changamoto wanazo kitana nazo na kisha tunapata muda wa kuzijadili pamoja.

Mfano mwingine ni kwa Mama ntilie au Wauza huduma za vyakula,
Changamoto kubwa mala nyingi uwa inakuwa ni kwenye maandalizi ya chakula au huduma,
Malalamiko makubwa yanatolewa na mteja ambaye ndiye mlaji wa mwisho wa huduma yako.

Sasa mala nyingi mteja anapo toa maoni au ushauri wa huduma aliyo ipata inakuwa na matokeo ya tofauti kwa mtoa huduma,
Watoa huduma wengi wamekuwa wakisimamia kitu wanacho kiamini na sio kie anacho shauri mteja au mlaji wa huduma yao.

Mfano wa Mwisho,
Ni kwa watu wanao uza au zalisha mbegu ambapo mteja anakuwa amenunua na kafuata maelezo vizuri na kwa bahati nzuri au mbaya hajapata matokeo rafiki kama alivyo tegemea,
Ni lazima mtoa huduma uone ni kwa jinsi gani utakuwa sehemu ya hasara au changamoto ya mteja wako.
Kwa kufanya hivyo utakuwa umetengeneza Wateja/mabalozi imara wa biashara yako kwa watu wengine ambao huwezi kuwa fikia wote kwa wakati mmoja.

Rafiki yangu kwa namna hiyo huwezi.kuwa na wateja wa kudumu na wamao penda kuona ukiendelea kutoa huduma yako,
Huwezi kuwa na wateja kwa njia ya kuto msikiliza mteja wako,Kero wala ushauri anao toa maana yeye ndie mfaidika nambari moja wa huduma unayo itoa sasa kama huto mpa nafasi hawezi kujua kama wateja wako unawapa kilicho bora.

Mwisho kabisa,
Nikusii rafiki yangu juu ya kuwa sehemu ya hasara na changamoto anazo zipitia mteja wako,
Sikiliza ushauri wake,Sikiliza kero yake na ifanyie kazi ili kumfanya mteja arudi tena na kwa kufanya hivyo tu utakuwa na wateja wengi na walio sahihi na rafiki kwa biashara yako.

Kila la kheri rafiki yangu,
Na wako Mwandishi/Mjasiriamali na Mwamasishaji
Ernest Lwilla

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top