Habari na hongera ndugu msomaji wa masomo haya kupitia mtandao huu wa ufunguo wa mafanikio,
Niimani yangu kubwa unaendelea vema na kazi zako ukizisimamia zaidi kwa kutumia maarifa mbali mbali unayo yapata hapa na mahali pengine yanapo patikana maarifa kama haya.
Karibu tena nakukaribisha kwa moyo mkunjufu uweze kuitumia fursa hii kupata maarifa ambayo yataenda kuwa na mchango mkubwa sana kwenye biashara na hata kazi zako za kila siku,
Kwa siku hii ya leo nitaenda kukushirikisha kosa kubwa linalo fanywa na watu wengi sana hasa wanapo anza kuona namna wanavyo weza kuongeza mifereji mingine ya kuongeza pato lao.
Kwa kipindi cha awali watu wengi huanza biashara zao kwa umakini sana na hata kuzifuatilia kwa ukaribu sana ikiwa ni pamoja na wao wenyewe kuwajibika kwa 100%,
Kwa kipindi hiki chote biashara nyingi huwa zinakuwa sio kubwa na hata faida inayo zalishwa huwa ni kidogo sana
Hivyo watu wengi hutumia muda wao kuzikuza biashara zao mpaka biashara hizi zinapo anza kutengeneza faida.
Jambo kubwa sana ni pale biashara hizi zinapo kuwa zimesimama na hapo wamiliki wengi huanza kuona fursa zingine za kuweza kuboresha kipato chao ikiwa ni pamoja na kuanzisha miladi mipya kwao,
Sasa kila wanapo ongeza mradi wamekuwa wakitumia muda mwingi kuisimamia miladi mipya na kusahau kuwa juhudi hizo zinatkiwa kuelekezwa kwenye miladi yao yote.
Kwenye hatua hii kubwa watu huanza kuona namna wao wanavyo weza kuajiri watu wengine ili kuhakikisha shughuli za uzalisha zinakuwa bora zaidi kwao,
Kwa kufanya hivyo huona wamesha maliza uwajibikaji wao kwenye miladi ya awali na hivyo wanaendelea kufungua miladi mingine ambapo ndio huweka nguvu kubwa huko.
Watu hawa wanaamini kufanya hivyo ndio kufikia mafanikio kwa urahisi zaidi lakini sio kweli kwasababu hii,
Wanapo waachia wafanya kazi uendeshaji wa shughuli zote wafanya kazi hao huwa hawafanyi hivyo badala yake wanaanza kufanya mambo hivyo hovyo na mwishoni mambo yanabadilika kuwa hasara kwenye biashara zao.
Kwenye hatua hii biashara nyingi huwa hazizalishi kiwango cha fedha ambacho kingezalishwa na wamiliki wa biashara hizo,
Matokeo yake makubwa ni kudorola kwa uzalishaji wa miladi hiyo,Kuwa na miladi mingi ambayo haizalishi kipato,Hasara kubwa ya uendeshaji miladi isiyo zalisha mfano kulipa kodi mbalimbali.
Mathara hayo huwa makubwa zaidi kulingana na muda ambao uzembe umeanza kutokea na muda mwingine hutokea kupotea kwa wamiliki wa biashara hizo.
Mfano:
Mmiliki anapo kuwa na miladi anayo ipa muda wa kutosha na mingine muda unakuwa mdogo zaidi madhara makubwa huwa ni kupoteza miladi yote,
Yaani wanapo gundua miladi mingine haizalishi wataanza kurudi kwenye miladi ya awali ili kuipa misingi ya kuzalisha hali hiyo itapelekea ile miladi mipya kukosa usimamizi mzuri kwa sababu inakuwa bado haija anza kuzalisha faida.
Ushauri wangu juu ya hali hii,
Ni kuwa karibu sana na miladi yako yote,
Kushiriki kikamilifu kwenye usimamizi na hata kufanya kazi kwa baathi ya muda kulingana na ratiba yako.
Hii itawafanya wasaifizi hao kuwa makini lakini pia linapo tokea tatizo lolote inakuwa rahisi kulitambua na kulichukulia hatua za udhibithi.
Hali hii imenisumbua sana siku za nyuma ambapo muda mwingi niliwaachia kazi zangu wasaidizi kiasi ambacho wasaidizi hao wanafanya kazi chini ya kiwango na kwa kuto jituma matokeo yake yalikuwa ni kuwafukuza wateja wote,
Ambapo wateja wengi wakifika ofisini walikuwa wananiulizia na wanapo kuta sipo hawaachi kazi licha ya kuwa kipindi cha nyumba waliacha.
Rafiki hutakiwi kustaafu kuwajibika kila sehemu uliyo weka kipato chako hata ingekuwa unazalisha fedha kidogo kidogo,
Unatakiwa kuwa karibu muda wote tena ukiwa kama mfanyaji na sio Boss au msimamizi,
Kwa kufanya hivyo utatambua madhaifu mengi sana yaliyo kwa vijana au wasaidi wako kwa njia hii wafanyazi hawawezinkuleta uzembe wa aina yoyote kwenye kazi.
Kumbuka kufanya kazi kama boss itakughalimu kiasi cha kushuka na kuanzia kwenye hatua iliyo mbaya zaidi,
Usipo ziba ufa utajenga ukuta na hivyo unatakiwa kufahamu ikiwa utashindwa kusimamia kwa ukari biashara zako itakughalimu kuzipoteza biashara hizo.
Anza kushirikiana kwa ukaribu na kutambua mfumo mzima kama unafuatwa na wasaidizi wako.
Kila la kheri rafiki yangu.
Na wako rafiki na Mjasirimali mwenzako.
Ernest Lwilla
Kwa ushauri zaidi wa Biashara nitafute
errynine6@gmail.com/0715222989
Chapisha Maoni