Unknown Unknown Author
Title: Mambo 3 Muhimu Unayo Paswa Kuzingatia Unapo Taka Kufungua Biashara.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na mfuatiliaji wa masomo haya kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa mafanikio , Niimani yangu kubwa kuwa unaendelea kuyafanya k...

Habari rafiki na mfuatiliaji wa masomo haya kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa mafanikio,
Niimani yangu kubwa kuwa unaendelea kuyafanya kazi mambo haya muhimu ili kufikia mafaniko yetu kwa kila eneo ambalo upo.

Nichukue fursa hii kukukaribusha kwa mikoni miwili ili tuweze kuongozana mpaka mwisho wa somo hili na kulipa kipaumbele kabla ya kuchukua hatua yoyote wakati wa kuingia kwenye Biashara.

Nimeandaa somo hili ni kwa sababu watu wengi wamekuwa wakifanya makosa makubwa kabla ya kuanza biashara zao na madhara yake yamekuwa makubwa sana kiasi kuwarudisha nyuma,
Makosa haya wapo watu wanao fanya kwa kuyajua na wengine kwa kuto yajua lakini mwisho wa siku yanawaghalimu.

Watu wengi wamekuwa wakiingia kwenye biashara kwa mihemko,Kuiga na hata kufanya tu kwa sababu ndiyo kitu pekee wanacho kiweza au walicho aminishwa kuwa kinafaida kubwa na hili ni kweli mtu kwa kufanya biashara tu anauhakika wa kutengeneza kipato kikubwa.
Lakini mambo yanaweza kuwa tofauti na mategemeo yako ikiwa huto zingatia mambo haya ninayo kwenda kukushirikisha kwenye somo hili lililo muhimu kabla hujafungua biashara.

Mambo haya matatu ni kama yafuatayo:

i/Uwepo Wa Soko,
Kabla hujaanza biashara yoyote ni lazima uone uhitaji wa kitu unacho taka kufanya au huduma unayo taka kutoa,
Ujue uhaba wa hitaji hilo na hivyo unapo toa huduma yako iwe na watumiaji watakao ifurahia thamani utakayo itoa.

Ikiwa ni biashara ambayo tayari kunawatu wanaifanya basi itakuhitaji kuona kwa kina mapungufu madogo madogo yanayo kosekana kutoka kwa wafanya biashara ambao wapo,
Na hivyo jukumu lako litakuwa ni kufanya kwa ubora zaidi na hata kuyatatua matatizo ya watu wanayo yakosa kutoka sehemu zingine.
Uwepo huu wa soko ndio kipimo cha huduma unayo paswa kutoa,
Kamwe usitoa huduma pasipo kuona uwepo wa soko au watumiaji wa huduma yako utashindwa kuiendesha biashara yako na hata ukiendesha basi itakuwa ni kwa hasara.

ii/Ukubwa Wa Soko,
Ni lazima utambue ukubwa wa soko la huduma au biashara unayo taka kutoa,
Je kunawateja wa kutosha? Ukubwa huu wasoko ndio kipimo kikubwa cha kukuonyesha kama utaendesha biashara kwa hasara au faida.
Mfano:Bila shaka ulisha wai kuona biashara nyingi zikifunguliwa kwa kiwango cha juu lakini watumiaji wa huduma hizo huwa ni wachache sana Eg BarberShop,Saluni kubwa za wanawake,SuperMarkets Nk
Watu wengi wanapenda vitu vilivyo bora lakini kwa ghalama wanayo mudu.

Hivyo Unahitaji kuwajua wateja wa biashara yako na hata kuona utaanzaje kuitoa huduma hiyo kwa uhakika wa kuuza ingawa huwezi kuanza biashara na kuanza kuuza mala moja hii ni kwasababu ni lazima utengeneze jina lako la biashara na hata kuonyesha utofauti wako na wengine ndipo uweze kuwa na wateja wa kutosha kuendesha biashara yako.
Pia unapo tizama ukubwa wa soko ni muhimu kuangalia na makundi mbalimbali ya watu,
Hakikisha biashara au huduma yako inagusa watu wa makundi yote.

iii/Umudu Wa Ghalama,
Wateja kumudu ghalama za huduma au biashara yako ni eneo muhimu linalo paswa kuzingatiwa kwa sehemu kubwa kabla hatuja anzisha biashara zetu,
Je wakazi waeneo hilo wanamudu kutoa ghalama za thamani utakayo itoa?
Hiki ni kipimo kikubwa cha kuanza biashara na nivizuri tunapo anzisha biashara ni muhimu kuweka au kutoa thamani ambayo wakazi wa eneo hilo wataweza kununua.

Jambo lolote tunalo toa kwenye maisha yetu ni thamani kwa wengine na hivyo kama hawawezi kumudu ghalama za thamani hizo haina maana tena ya sisi kuendelea kutoa thamani hizo,
Hivyo ni muhimu kutoa thamani itakayo mudu vipato vya watu wengine.
Ni vivyo hivyo kama vipato vya wakazi hao hawatamudu kununua biashara yako basi ni wazi biashara hiyo utaiendesha kwa hasara.

Rafiki ni muhimu kujua kwa kina chochote tunacho fanya ni lazima kitatue matatizo ya watu wengine lakini ni muhimu kutoa huduma amabazo watu wengine watamudu kununua maana tunafanya kwa ajiri yao,
Biashara inategemea uwepo wa soko,Ukubwa wa soko na Kumudu ghalama iwapo utaona kati ya vitu hivi kimoja wapo hakipo basi hunasababu ya kuupoteza muda wako.

Hii ndio maana wapo wataalamu wanao husika moja kwa moja na masoko,
Ambapo wazalishaji kabla hawajazalisha wanawatumia watu hao kujua Soko kama lipo,Ukubwa wa soko hilo yaani hitaji la kitu hicho linaukubwa kiasi gani?
Pia Kumudu ghalama ambazo zitakuwa ni thamani ya huduma watakazo zitoa.
Baada ya hapo ndipo hatua za uzalishaji wanaanza lakini wakiwa na uhakika wa mambo hayo muhimu.

Muhimu sana sana kuzingatia hayo mambo kwa sababu yamekuwa yakiwa ghalimu watu wengi kila wanapo chukua hatua,
Makosa haya hupaswi kuyafanya tena wewe rafiki yangu kwa sababu nimesha kushirikisha na hivyo unatakiwa kuyafanyia kaiz mambo haya kila unapo fikiri kuanza biashara au huduma.
Kwa kuzingatia mambo hayo matatu unakuwa umejihakikishia ushindi wa huduma au baishara yako.

Kila la kheri rafiki yangu,
Na wako Mwandishi na Mjasiriamali

Ernest Lwilla
Kwa maoni na ushauri wa biashara piga 0715222989/Ujumbe kupitia Email:errynine6@gmail.com

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top