Unknown Unknown Author
Title: Mambo 5 Muhimu Niliyo Jifunza Kwenye Semina Ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA (KISIMA CHA MAARIFA).
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na mwanamafanikio mwenzangu kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa Mafanikio, Niimani yangu kubwa kuwa ni mzima wa afya njema kama...

Habari rafiki na mwanamafanikio mwenzangu kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa Mafanikio,
Niimani yangu kubwa kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu.
Ninafasi ya pekee kwetu kwenda kuweka juhudi zaidi ili tuweze kupata mafanikio yaliyzaifi ya hayo
Rafiki,
Yapo mambo mengi sana niliyo pata kujifunza kwenye semina niliyo shiriki KISIMA CHA MAARIFA,
Semina hii ili fundishwa na Kocha wa Mafanikio Amani Makirita iliyo kuwa na Kichwa kikuu ELIMU YA MSINGI YA FEDHA ndani yake ikiwa na masomo kumi.

Kwa siku hii ya leo nitaenda kukushirikisha mambo matano ikiwa ni pamoja na hatua jilizo kwisha zichukua mpaka sasa,
Karibu nikushirikishe.

Jambo la kwanza Maana halisi ya FEDHA ,UTAJIRI NA UHURU WA KIFEDHA,

Fedha ni nini?
Fedha ni njia ya kubadilishana dhamani,
Fedha ni njia iliyo kubalika kubadilishana thamani kwa dhana hii unapo fikiri kupata fedha ni muhimu kufikiri kwanza ni thamani ipi utakayo toa ili uweze kulipwa au kupata fedha,
Uwepo fedha umerahisisha mabadilishano hayo ya thamani Mfano:Unapo hitaji shiringi 10000 ni lazima uwe na kitu chenye thamani sawa na shilingi 10000 ambacho kinahitaji na mtu mwingine au kutatua tatizo la mtu mwingine.
  Utajiri,
Ni kuwa na kiasi kilicho pitiliza hata kiasi ambacho mtu anahitaji kuendesha amisha yake.
  Uhuru wa kifedha,
Ni hali ambapo mtu anakuwa amefikia na kuto kuwa na hofu yoyote kuhusu fedha,
Hatua hii mtu anakuwa na uwezo wa kuishi maisha anayo yataka bila wasiwasi hata asipo fanya kazi moja kwa moja.

Jambo la pili KIPATO & NJIA ZA KUONGEZA KIPATO  ZAIDI,

Kipato,Ni ile fedha unayo lipwa kutokana na kufanya au kuwezesha kitu fulani kufanikiwa,
Kipato kinaweza kutokana na kazi ambayo unakuwa umeifanya wewe mfano kuuza bidhaa au huduma unazo weza kutoa kwa wengine ambaonwanahitaji.
Muhimu kufahamu kuwa zipo aina mbili za kipato ambapo ni kama ifuatavyo
i/Active Income.
Hiki ni kipato kinacho kuhitaji wewe uwepo moja kwa moja kwenye shughuli au uzalishaji.
ii/Passive Income.
Hiki ni kipato unacho weza kutengeneza pasipo uwepo wako moja kwa moja.

Ili kutengeneza na kuongeza kipato zaidi ni muhimu kurejea kwenye maana halisi ya fedha ambayo ni Thamani,
Ili kutengeneza fedha zaidi ni muhimu kuongeza thamani zaidi pia wingi au uchache wa
Kipato ni kiashiria cha thamani unayo toa zaidi kwa wengne Mfano:
Kuwapa watu Elimu,Huduma za afya,Kuuza bidhaa n.k,

Mifereji ya kipato,
Bahari daima huwa haikauki kwa sababu ya uwepo wa mifeji mingi inayo peleka maji kwenye bahari moja.
Hivi ndivyo ilivyo kwenye vipato vyetu,Kama unahitaji kuongeza kipato zaidi badi ni muhimu kuongeza na kuwa na mifereji mingi zaidi ya kupato.
Muhimu zaidi kufahamu hitaji nambari moja lakufikia utajiri na hata uhuru wa kifedha ni kuwa na mifereji mingi ya kipato.

Jambo la Tatu MADENI NA NAMNA YA KUONDOKA KWENYE MADENI,

Madeni ni utumwa.
Hii nikauli inayo umiza lakini yenye ukweli mkubwa ndani yake na wengi hawapendi kuisikia kwa sababu wengi wapo kwenye dimbwi hilo la madeni,
Madeni ni utumwa kwa sababu zifuatazo
i/Madeni yananyima uhuru,
ii/Madeni ni utumwa kwa sababu anae kudai anakuwa na usimanizi wa karibu zaidi na fedha anayo kudai,
iii/Madeni ni utumwa kwa sababu unakuwa unafanyia kazi wengine,
Madeni haya yanaweza kuwa ni utumwa zaidi kwako ukilinganisha na aina ya madeni utakayo daiwa kwa sababu kuna madeni aina mbili
Madeni mabaya ja madeni mazuri hivyo inategemea wewe unamadeni yaliyo upande upi.

Ili kuondoka kwenye madeni unatakiwa kufanya mambo yafuatayo.
1:Jua ni kiasi gani unadaiwa,
2:Tengeneza mpangilio mpya wa kipato chako utakao husisha na kulipa madeni hayo.
3:Kipaumbele cha kulipa madeni
4:Jiandae kwa kipindi kigumu cha kulipa madeni yako,
Kuondoka kwenye madeni sawa na vita ya kutafuta uhuru hivyo unahitajinkuwa tayari kwa kipindi kigumu utakacho kipitia wakati unalipa madeni hayo.

Jambo la Nne UWEKEZAJI,DHANA YA COMPOUND INTEREST & RULE OF 72.

  Uhuru wa kifedha pale maisha yako yanapo weza kwenda kama kawaida hata kama umelala au hufanyi kazi moja kwa moja,
Hivyo hatuwezi kufikia hatua ya Utajiri na  Uhuru wa kifedha kwa kuweka akiba pekee kwa sababu akiba pekee huwa inaisha baada ya muda fulani hata ikiwa nyingi kiasi gani hivyo tunapaswa kuifanya fedha kutufanyia kazi sisi pasipo kuhusika moja kwa moja na njia pekee ya fedha kutufanyia kazi ni kupitia uwekezaji mbali mbali.

Maana ya uwekezaji,
Uwekezaji,Ni pale fedha yako inaponkuwa inakufanyia kazi badala ya wewe kuifanyia kazi fedha,
Kwenye uwekezaji fedha yako inawekwa kwenye shughuli ambazo wewe huto husika moja kwa moja na usimamizi wake lakini Unakuwa unalipwa sehemu ya faida inayo tokana na uwekezaji ulio ufanya.

Jambo muhimu unalo takiwa kulifahamu kwenye uwekezaji ni
i/Anza mapema
ii/Wekeza kila muda.
Unapo anza mapema maana yake unakuwa na.muda wa kutosha kufanya uwekezaji wako,
Pia unapo wekeza kila muda unanufaika zaidi kiuchumi kuliko kuwekeza mala moja Mfano:Kununua hisa za milioni moja mala moja kwa mwaka kwa njia hii unaweza kuwa uanpoteza thamani ya fedha yako,
Hivyo muhimu kuwekeza kila wakati na kwa kiasi kidogo kidogo.

Dhana ya Compound Interest & Rule of 72=
Uwekezaji unadhana kuu mbili tunazo paswa kuzifahamu ili kunufaika na uwekezaji tunao weza kuufanya.
i/Compound interest(Riba mkusanyo),
Hii ndiyo dhana kuu inayo fanya uwekezaji kuwa kitu muhimu katika maisha.
ii/Rule of 72 (Sheria ya 72)
Hii ni dhana inayo tuonyesha muda ambao unahitajika ukuaji wa uwekezaji wako,
Kwa sheria hii unaweza kujua inachukua muda gani kwa uwekezaji wako kukua mala mbili.

Rafiki sito weka mifano hapa namna dhana hizi zinavyo fanya kazi na kuweka uwekezaji kuwa kitu muhimu sana,
Ila kumbuka somo hili linamambo mazito ambayo jamii yetu kubwa haiyajui hata kidogo hivyo
kwa ufupisho huo unapaswa kuzingatia mambo haya muhimu  kwenye uwekezaji,
1:Anza kuwekeza mapema uwezavyo,
2:Usitoe fedha kwenye uwekezaji kwa ajiri ya matumiazi
3:Tawanya uwekezaji wako
4:Jifunze zaidi kuhusu uwekezaji
5:Epuka watu wanao tabili hali ya uwekezaji.

Jambo la Tano KODI & BIMA

Kodi,
Ni ghalama tunayo lipa kuishi kwenye jamii iliyo staarabika,
Kupitia kodi serikali inapata nguvu yankuendelea kuwepo na kuendelea kutoa huduma kwa Wanachi wake.
Serikali haizalishi wala haina kazi inayo iingizia kipato bali inategemea kuwatoza wanachi wake kodi ili iweze kuendesha shughuli zake na kuwapa huduma wanachi wake mfano: Miundo mbinu na huduma za kijamii Eg Elimu,Maji,Afya nk,
Bila kodi ni vigumu kuishi kwenye jamii iliyo staarabika leo hii tuna vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajiri ya kodi ndizo zinawezesha vyombo hivyo kuwepo.

Tanzania tunachombo kilicho pewa jukumu la kukusanya na kusimamia kodi ambayo ni TRA,
Hapo ndio wanakusanya kodi na hatankupitia sera na sheria za kodi.

Kujenga utajiri na uhuru wa kifedha ni jambo moja na kuulinda utajiri na uhuru wa kifedha ni jambo muhimu zaidi,
Watu wengi huweka muda,kazi na nguvu kubwa kuzitafuta fedha lakini baada ya mda fulani hupoteza fedha hizo zote hata wao wenyewe bila kujua na kwakuwa hakuna anae jua keaho yake itakuwaje basi ni muhumu kujiwekea tahadhari.

Bima,
Ni kujipa uhakika wa kile ulicho nacho hata kama itatokea hatari kubwa itakayo haribu mali zako,
Kupitia bima basinunakuwa salama  kwa lolote linalo weza kutokea.

Zipo bima aina nyingi unazo weza kuwa nazo na hizi ni baadha ya bima unazo weza kuwa nazo,

i/Bima ya afya
Hii ni bima inayo kupa uhakika wa matibabu kwako na familia yako zinapo kuwa na changamoto za kiafya,
Bima hii ni muhimukuwa nayo wewe na hata familia yako.
ii/Bima ya mali
Mali yoyote uanyo miliki unapaswa kuikatia bima ili lolote linalo weza kutokea linapo tokea unakuwa an uwezo wa kulipwa mali zako.
Mali zinazo weza kukatiwa bima ni kama zifuatazo Vyombo vya usafiri,Majengo na hata biashara.
iii/Bima ya Maisha,
Hii ni bima unayo katankwa ajiri ya kulinda maisha yako dhidi ya jambo lolote linalo weza kutokea dhidi ya maisha yako binafsi Mfano:Umepata ajali iliyo pelekea kilema au Umefariki dunia, kwa bima hii wewe au ulio wajaza watalipwa kiasi cha fedha kutokana an kilichotokea.

Rafiki bima ni kitu muhimu kuwa nacho hasa kwenye safari hii ya mafanikio,
Unapo kuwa na bima hatua zako za mafanikio zinakuwa zipo salama kwa sababu muda wote unakuwa unatumia bima yako badala ya kutumia fedha zako.

Rafiki yapo mambo mengi na muhimu niliyo jifunza kwa kina kupitia semina hii Mfano:Biashara,Jinsi ya kuwapa na kuwajengea watoto wetu misingi bora ya kifedha,Aina za uwekezaji na aina ya uwekezaji unayo paswa kuufanya wewe,Tofauti ya uwekezaji mzuri na Assets.
Na hayo ni machache kati ya mengi ambayo kwa sehemu kubwa jamii yetu haitufundishi.

Rafiki ni muhimu wewe kuyapata masomo haya ya Elimu Ya Msingi Ya Fedha ili kuepukana na makosa makubwa yanayo fanwa kula siku na yanaturudisha nyuma zaidi.

Namna ya kuyapata masomo haya unapaswa kuwa mwanachama wa kisima cha maarifa kwa kulipia Ada ya Mwaka mzima ambayo ni Tsh 50000,
Kwa kufanya malipo hayo utapata masomoyo yote kumi ya semina hii zaidi utaendelea kunufaika na masomo mengine yanayo endeshwa kwenye kisima cha maarifa bure,Utapewa link ya kuingia kusoma makala zaidi ya 4000 zilizopo www.kisimachamaarifa.go.tz.
Pia unaweza kujiunga na njia ya Email list na kupata makala zote za amka myanzania Bure kwa kufuata link hii http://www.amkamtanzania.com/p/pata-habari-kwa-email.html.

Wasiliana na Kocha Amani Makirita
Kwa simu WhatsApp 0755953887/Email.Amakirita@gmail.com.
Au tembelea www.amkamtanzania.com au www.kisimachamaarifa.go.tz

Rafiki sito penda ukose masomo hayo muhimu yaliyo fundiahwa kwenye simina hii.
Kila la kheri rafiki yangu.
Na Ernest Lwilla 0715222989.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top