Unknown Unknown Author
Title: Tumia Sheria Hii Muhimu Kila Unapo Hitaji Kufanya Mambo Makubwa Kwenye Maisha Yako Ya Baadae.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na msomaji wetu kupitia  mtando wetu huu wa Ufunguo Wa Mafanikio, Niimani yangu kubwa kuwa ni mzima wa Afya njema na Unaendel...

Habari rafiki na msomaji wetu kupitia  mtando wetu huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Niimani yangu kubwa kuwa ni mzima wa Afya njema na Unaendelea vema na kazi zako za kila siku ambapo ndipo unapo weka Akili,Nguvu na Maarifa ili kupata matokeo yaliyo bora na makubwa zaidi.

Nitumie fursa hii muhimu sana kukuarika ili tuweze kushirikishana yale yaliyo muhimu katika maisha ya mafanikio na hatimae kufikia hatua kubwa zaidi kimafanikio,
Kwa siku hii ya leo nitaenda kukushirikisha Sheria moja muhimu unayo paswa kuitumia kila unapo taka kufanya jambo lolote lililo kubwa kwa mafanikio yako ya baadae.

Kunamsukumo na nguvu kubwa sana ambayo ndiyo huwazuia watu wengi kutofikia hatua ya kufanya mambo yaliyo makubwa kwenye maisha yao ya mafanikio na hivyo muda mwingi hujikuta wanaweka juhudi kubwa lakini juhudi hizi haziwa fikishi kwenye nafasi ya kufikia mafanikio makubwa na hivyo kuendelea kuishi maisha yaliyo ya kawaida kila siku za maisha yao.
Mafanikio makubwa Au mambo makubwa yote yana miiko na sheria ili uweze kuyafikia na ikiwa utakuwa tayari kuishi na kufanya mambo ya kawaida ambayo yanafanya uonekane na wewe ni miongoni mwawatu wanao ishi machaguo sahihi ya maisha yao basi huwezi kufikia mafanikio yaliyo makubwa zaidi kwenye maisha.
Nifuatilie

Mafanikio makubwa yanasheria moja iliyo kubwa na hii ndiyo inayo wafikisha watu wengi kwenye mafanikio makubwa,
Sheria hii ni Neno HAPANA KWENYE MAMBO YOTE YA KAWAIDA.

Ndio,Yapo mambo mengi unayo takiwa kuachana nayo pindi unapo kuwa unajambo kubwa unalo taka kulifanya Au kulikamilisha ndani ya kipindi fulani,
Nahapo unahitaji kuweka juhudi kubwa zaidi na kuelekeza nguvu zako zote kwenye jambo hilo moja.

Huwezi kukamilisha jambo lolote lililo kubwa ikiwa utakuwa na mambo mengi yanayo vujisha kipato chako,
Ni lazima uweke juhudi kubwa na nguvu huku ukiwa unafanya mambo ya kawaida kawaida ambayo kwa kiasi kikubwa yanakurudisha nyuma.
Mfano:Unahitaji kufungua kampuni kubwa itakayo hitaji uwekezaji wa fedha nyingi huwezi kukamilisha hilo ikiwa utaendelea kufanya mambo madogo madogo ambayo kwa sehemu kubwa yanakurudisha nyuma kufikia mpango wako huo.

Upo kwenye mpango huo na unahitaji kisibadilike chochote kwenye mfumo wa maisha yako ya kawaida yaani kama ulikuwa nasafari zisizo za msingi,Uendelee kutumia fedha kwa anasa,Uendelee kunywa pombe kwa kiwango kile kile,Kuvaa nguo za ghalama nk,
Huwezi kukamilisha mpango huo kirahisi vinginevyo lazima uwe na mifereji Minngi inayo ianayo kuzalisha kipato kitakacho elekezwa kwenye shughuli hiyo.

Sheria hii ya HAPANA utatakiwa kuitumia kwenye maeneo yote ya maisha yako,
Na sehemu zingine zote zinazo hitaji utoe fedha zako hata kama ni kidogo kiasi gani.

Kwa kutumia sheria hii itakulazimu kubadili mfumo mzima wa maisha yako na kufanya uendane na sheria hii yaani uwe tayari kubadilika wewe,
Utalazimika kuacha mambo yote uliyo kuwa unayafanya kwa mazoea,
Utalazimika kuweka juhudi kubwa na matokeo yote ya juhudi hizo kuya elekeze kwenye jambo hilo lililo kubwa na lenye manufaa kwa maisha yako ya baadae,
Utalazimika kuwa tayari kwa dhihaka kutoka kwa watu wako wa karibu maana kila mtu atasema mambo yake wakati wewe ukiwa kwenye matumizi ya sheria hii,
Usiogope kuonekana unaishi maisha yaliyo chini ya kiwango chako yaani maisha yasiyo na hadhi ya juu.

Sheria hii inaweza kuleta mabadiliko makubwa sana ukianzia ndani yako,Marafiki,Ndugu na jamaa ambapo inaweza kukutenganisha nao na hata kufikia hatua ya kuonekana upo tofauti na jamii inayo kuzunguka,
Kutokana na hilo pia utajikuta kuwa na maisha magumu,Maisha yasiyo endana na juhudi unazo weka kwa wakati huo,
Utajikuta familia yako inaelemewa na maisha ambayo haikuya zoea.

Rafiki njia pekee ya kuishinda hali hiyo ni kuangalia lilejambo kubwa unalo taka kulifanya,
Angalia umefikia hatua gani na bado kiasi gani kufikia lengo lako kisha ongeza bidii na usiiache sheria hii.
Kwa kufanya hivyo haitoshi ni lazima ujihamasishe ndani yako na kuona kama tayari umesha kamilisha jambo hilo na tayari unanufaika nalo.
Hupaswi kabisa kuangalia wengine wanafanya nini?
Hupaswi kuona wengine wanaishije maisha yao zaidi angalia wamefanya makubwa gani kwenye maisha yao na hiyo itakupa nguvu zaidi ya kuendelea kuweka juhudi zaidi.

Rafiki ni muhimu sana kuitumia sheria hii ya HAPANA ingawa unatakiwa kuwa tayari na kuwasehemu ya mabadiliko yoyote yatakayo tokea kwako.
Nasema hivi kwa sababu kuitumia sheria hii inahitaji roho ngumu,
Roho ya kuachana na mambo yote yasiyo na muhimu kwako.

Hivyo rafiki tumia sheria hii kila unapo kuwa katika kukamilisha jambo lolote lililo kubwa na lenye manufaa ya maisha yako ya baadae,
Tumia Sheria hii na uiishi maisha yako yote ya mafanikio.

Ikiwa unamaoni,Changamoto na hata ushauri tafadhari acha maoni yako kwenye kisanduku cha maoni hapo chini Au 0715222989/errynine6@gmail.com.

Kila la kheri rafiki yangu,
Fanyia kazi somo hili litakusaidia sana.
Na wako Mjasiriamali & Mwandishi wako

Ernest Lwilla.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top