Unknown Unknown Author
Title: Hii Ndiyo Siri Kuu Itakayo Kupa Hamasa Ya Kukamilisha Malengo Yako Makubwa
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na Msomaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio, Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima na Unaendelea vema kuwa bora zaidi kwen...

Habari rafiki na Msomaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima na Unaendelea vema kuwa bora zaidi kwenye kazi ulizo chagua kIfanya ili kupata matokeo makubwa kwenye maisha yako.

Ikiwa ni siku nyingine mpya na kubwa kwetu ni Fursa ya pekee kwenda kuweka Akili,Nguvu na Maarifa ili tuweze kupata matokeo bora zaidi,
Nitumie fursa hii kukukaribisha kwenye makala hii ili niweze kukushirikisha ya muhimu niliyo kuandalia siku hii ya leo.

Dunia imejaa watu wengi,
Watu hawa wote kila mmoja anapambana ili aweze kutimiza kusudi lake la kuwepo Duniani,
Lakini ni watu wachache sana wanao weka juhudi na kupata matokeo makubwa ya juhudi zao na wengine huishia njiani.

Ni watu wachache wanao zifahamu mbinu sahihi kufikia mafanikio yao,
Na wengi huishia kuweka malengo makubwa bila kuyafanikisha.
Hivyo kwa siku hii ya leo nitaenda kukushirikisha mambo mawili makubwa unayo takiwa kuyafahamu ili uweze kutimiza malengo unayo kuwa umejiwekea na hatimae kufikia Kusudi lako hapa Duniani.
Karibu.

1.Malengo yako yawe ni Deni,
Ili uweze kuyatimiza malengo yako kwa usahihi na kwa muda mwafaka ni lazima malengo yako yawe deni,
Yaani malengo yako yawe kama umekopa hivyo unatakiwa kurudisha mkopo huo.

Hii ni mbinu itakayo kufanya ujiwekee nidhamu itakayo kupa hamasa ya kufanya kazi kwa juhudi kubwa na kuelekeza kipato chako kwenye kulikamilisha lengo lako,
Katika kulikamilisha lengo lako kwa njia ya kufanya marejesho ni muhimu kutambua lengo lako linahitaji fedha kiasi gani,
Kisha kiasi hicho kukigawa kwa muda ulio panga kulikamilisha lengo hilo.
Mfano;Lengo lako ni kukusanya kiasi cha Shilingi milioni kumi kwa mwaka Kiwango hiki unakiweka kwenye mfumo wa deni,
Kisha Unagawanya kiasi hicho kwa miezi kumi na mbili na jibu hilo ndicho kiwango cha marejesho kila mwezi.

Baada ya hatua hiyo unahitaji kuweka nidhamu kubwa sana ili uweze kufanya marejesho hayo kila mwezi bila kuacha hata mwezi mmoja ili kufanikisha lengo lako,
Katika kulifanikisha lengo kwa njia hii  hutakiwi kwenda kukopa fedha kwa mtu Au taasisi za kifedha kwa sababu hautarejesha kama ulivo ichukua ni lazima itakuwa na riba ambapo utakuwa umemfanyia mtu mwingine kazi kwa kiasi fulani hivyo fanya hivyo kwa hatua kubwa ya mafanikio yako.

2.Andika malengo yako,Kuandika malengo ni hatua nyingine kubwa zaidi na  iliyo muhimu katika kufikia lengo ulilo jiwekea mwenyewe,
Watu wengi wamekuwa wakijizuia kukamilisha malengo yao kwa kuto Andika na wakiamini watakamilisha kwa kutunza kumbukumbu kichwani huu ni wongo ambao watu wengi wanajidanganya na kujipotezea muda wao na mwisho wa siku huishia kuongea bila kutekeleza,

Kuandika malengo ni hamasa kubwa tena unayo jipa mwenyewe,
Kwa kuandika malengo unakuwa utajikumbusha mala kwa mala na hivyo kuendelea kuweka juhudi kubwa kila siku.

Hatua hii ya kuandika malengo haita kupa ushindi mkubwa,
Hivyo ni lazima malengo hayo uyaweke sehemu ambayo utayaona kila muda.
Malengo yako unaweza kuyaandika vizuri na kuya bandika kwenye ukuta wa chumbani kwenye Waleti na sehemu nyingine itakayo kuwa rahisi kwako kuona kila muda.
Na unapo tizama malengo yako usitizame kama picha ni lazima upate muda wa kutafakari na kutafuta mbinu mpya zitakazo kupa hamasa ya kukamilisha malengo hayo.

Rafiki kupanga na kuweka malengo ni hatua kubwa sana lakini hatua hiyo haikupi uhakika wa moja kwa moja wewe kufanikiwa kutimiza malengo hayo,
Hivyo ni lazima uweke juhudi kubwa na unapo weka juhudi haiwezi kuwa kirahisi ni lazima utakutana na changamoto zitakazo kukatisha tamaa.

Hivyo rafiki tumia mbinu hizi mbili muhimu nilizo kushirikisha hapo juu kukamilisha malengo yako,
Weka Akili,Nguvu kubwa na Maarifa ili kufikia malengo yako.

Acha Maoni,Changamoto na ushauri kwenye sanduku la maoni hapo chini,
Au Tuma ujumbe wako kwenda 0715222989/errynine6@gmail.com

Kila la kheri rafiki yangu,
Na wako Mjasiriamali & Mwandishi
Ernest N Lwilla

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top