Unknown Unknown Author
Title: Hii Ndiyo Tiba Ya Kushinda Vizuizi Na Kila Sababu Za Kuto Chukua Hatua Kwenye Maisha Yako
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na msomaji wa masomo yetu kupitia mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio, Niimani yangu kubwa kuwa ni mzima wa afya njema na Una...

Habari rafiki na msomaji wa masomo yetu kupitia mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Niimani yangu kubwa kuwa ni mzima wa afya njema na Unaendelea vema na kazi ulizo chagua kuzifanya kwa ubora ili kufikia mafanikio makubwa.

Ikiwa ni siku nyingine nzuri sana kwetu ni Fursa ya pekee kwenda kwenda Akili,Nguvu na Maarifa zaidi ili tuweze kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yetu,
Ni chukue nafasi hii ya pekee kukukaribisha kwenye makala yetu ya leo ambapo nitaenda kukushirikisha Mwarobaini wa kila aina ya sababu na vizuizi vinavyo kuzuia kuchukua hatua dhidi ya maisha yako.

Idadi ndogo sana ya watu Duniani ndiyo inayo fikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao na hatmae kuwa Msaada kwa maisha ya wengine,
Watu hawa ndiyo walio achana na kila aina ya sababu inayo kuwa kizuizi kwa watu wengine kuto chukua hatua dhidi ya kuboresha maisha yao.
Kila unapo wauliza watu ambao hawajachukua hatua huwezi kukosa sababu ambayo yeye anaona ndicho kizuizi cha yeye kuto chukua hatua.
Mfano:1
Anna kwanini hufanyi Biashara?
Jibu:Sina mta.
Mtaji Sh ngapi?
Jibu:Ni pesa nyingi.
Mfano:2
John kwanini umeshindwa kwenye Interview yako?
Jibu:Sina bahati.
Hivyo walio shinda ni wenye bahati pekee?
Ndiyo hata hivyo upendeleo ulikuwa mwingi sana.

Hivyo ndivyo watu wengi wanavyo jizuia kuchukua hatua dhidi ya maisha yao na kwa namna hiyo hawawezi kuchukua hatua wala kujishughulisha na chochote na hivyo kuendelea kuwa mizigo kwa watu wengine hasa Wazazi,Marafiki na Ndugu wengine,
Ili kuweza kuzishinda hofu hizi na kila sababu zinazo wazuia watu kuchukua nitaenda kukupa tiba itakayo kufanya uachane na sababu zote na uchukue hatua sasa.

Tiba hii ni NDIYO.......KWA HIYO?
Hii ndiyo tiba unayo paswa kuitumia kila unapo jipa sababu zinazo onyesha kukuzuia kuchukua hatua,
Mfano sababu nyingi sana zinazo wazuia watu wengi kuchukua hatua ni kama
Sina mtaji,Sina bahati,Nimezaliwa kwenye familia ya kimasikini,Wazazi wangu ndiyo wanao changia kuendelea kuto chukua hatua.
Ukweli mtu pekee mwenye jukumu kubwa na kuwajibika juu ya maisha yako ni wewe mwenyewe kwa msingi huo unakuwa huna sababu ya kulaumu watu wengine kama sababu ya wewe kuto chukua hatua ya kuboresha maisha yako badala yake kila unapo Pata kizuizi tumia tiba hii NDIYO.....KWA HIYO? kuzivuka na kuendelea kuboresha maisha yako hasa ukizingatia wewe ndie mwenye jukumu la kuwajibika dhidi ya maisha yako.

Matumizi ya sheria hii ni kama ifuatavyo,
Niwazi wewe ndiyo mtu pekee mwenye jukumu la kuwajibika kuchukua hatua hivyo kila unapo jipa sababu ujue umejizuia wewe mwenyewe,
Sasa badala ya kujizuia maenyewe tumia sheria hii.
Mfano: Unapo kosa kianzio au mtaji yaani Sina Mtaji NDIYO....huna mtaji KWAHIYO unafanje?
Sina bahati NDIYO...huna bahati KWAHIYO unafanyaje?
Nimezaliwa kwenye familia ya kimasikini NDIYO...KWAHIYO unafanyaje?
Sina watu wakunisaidia NDIYO...huna msaada NDIYO KWAHIYO unafanyaje?

Hivyo ndiyo unavyo weza kuzishinda sababu zote na kila aina ya hofu zinazo kuzuia kuchukua hatua,
Kila unapo jipa sababu Jipe swali hilo pia na majibu ya swali hilo ndio hatua unayo paswa kuchukua ikiwa mtu pekee mwenye jukumu la maisha yako ni wewe huna sababu tena ya kujizuia.

Maisha yako ni jukumu lako namba moja hivyo kwa namna yoyote unatakiwa kuwajibika wewe kwa kuona ni njia gani unaweza kuzitumia kutoka hapo ulipo sasa,
Na ikiwa utachagua kujipa sababu bila majibu ya kukufanya uchukue hatua ujue umechagua fungu lisilo jema kwenye maisha yako,
Fungu la kuendelea kutafuta sababu na kuona wengine wakipiga hatua kwenye maisha yao.

Ukiwa kama rafiki yangu,Mwanamafanikio mwenzangu,Mpambanaji mwenzangu Hupaswi kuwa na aina yoyote Ile ya sababu zenye kukuzuia kuchukua hatua kubwa kwenye maisha yako,
Nasema hivyo kwa sababu umechagua kuwa Mwanamafanikio na mafanikio haya letwi kwa kujipa sababu bali kwa kuchukua hatua tena zilizo kubwa kwenye maisha yako,
Hatua hizi ndizo zitakazo kupa matokeo makubwa na maisha yaliyo bora zaidi.

Ikiwa umechagua kujipa sababu naweza ku kwambia huna sababu ya kuendelea kupoteza muda wako na kusoma masomo haya.
Ni lazima uwe tofauti na watu wengine ambao hawajaweza kupata masomo yangu.

Hivyo rafiki chukua hatua sasa achana na sababu zote zinazo onekana kuwa ni kizuizi kwako kuto chukua hatua,
Unapo chagua maisha ya ushindi maana yake umesha achana na sababu zote zinazo wazuia wengine kuchukua hatua.
Unaweza kuniachia Maoni yako,Changamoto yako Na Ushauri wako hapo chini kwenye sanduku la maoni au kwa kutumia 0715222989/errynine6@gmail.com.

Kila la kheri rafiki yangu,
Nikutakie mafanikio mema kwako.
Na wako Mjasiriamali na Mwandishi

Ernest Lwilla

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top