Habari Mwanamafanikio mwenzangu na Msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima na unaendelea vema na kazi ulizo chagua kufanya kwenye maisha ili kufikia mafanikio makubwa.
Leo ni siku Mpya kwetu na ni Fursa ya pekee kwetu sote kwenda kuweka juhudi kubwa zaidi ili tuweze kupata matokeo yaliyo makubwa zaidi kwenye maisha yetu,
Nichukue nafasi hii pia kukukaribisha kwenye makala hii ya leo ambapo nitaenda kukushirikisha tabia moja usiyo ijua kuhusu watumishi waliopo kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yetu.
Idadi kubwa ya watu tumegawanyika kwenye makundi mawili ya utendaji na uwajibikaji katika maisha,
Ambapo Kundi la kwanza ni watu Walio katika Ajira na Kundi la pili ni watu walio jiajiri wenyewe,
Kundi la kwanza mala zote limekuwa likionekana ni lenye maisha yenye uhakika zaidi kuliko kundi hili la pili.
Hii leo tutaenda kuigusia tabia moja ambayo kundi hili la kwanza wanaiishi kwa asilimia kubwa kwenye maisha yao,
Tabia hii kwa sehemu kubwa watumishi wengi wameshindwa kabisa kuikwepa Tabia hi ni UVIVU WA KUTO YAJUA MAENEO YOTE YA AJIRA ZAO.
Hii ndiyo tabia tutakayo enda kugusa kwa kina kupitia makala yetu ya leo,
Binafsi nimekuwa nikitembelea ofisi nyingi za uma na hata taasisi binafsi hasa zinazo shughulika na huduma muhimu za kimaisha mfano,Tasisi za kielimu,Tasisi za kifedha,Taasisi za Afya n.k
Mala nyingi sana nimekuwa nikipewa taarifa nyingi zisizo na ukweli Kutokana na tabia hii ya waajiliwa wengi kuwa wavivu wa kujua vizuri maeneo muhimu ya ajira zao.
Watumishi wengi ni wavuvu wa kujifunza zaidi kuhusu kazi wanazo fanya na hata maeneo yanayo wazunguka kwenye ajira zao,
Yaani mtu akiajiriwa kama Afisa masoko basi hawezi tena kujifunza wala kukifahamu chochote kuhusiana na campuni au tasisi iliyo mwajiri,Hawezi kujua taasisi hiyo inafaidikaje mpaka inamlipa yeye,Hawezi kujua changamoto zinazo ikabili Tasisi hiyo katika kufikisha huduma zake kwa watu wake.
Mtu ameajiriwa kama mlinzi basi hashughuliki na chochote kilicho nje na eneo lake yaani hawezi kuwa na taarifa zaidi kuhusu maeneo ya ajira yake jambo ambalo sio kweli,
Mtu yupo mapokezi basi hawezi kujua chochote kuhusu maeneo mengine ya ajira yake na wala kutafuta taarifa zozote zinazo weza kuwa muhimu zaidi kwa watu wanao wahudumia.
Watumishi wengi wamekuwa wavivu kutafuta taarifa zaidi Baada ya muda walio wajiriwa yaani muda mwingi hubaki na taarifa za muda ulio pita na hawajifunzi zaidi yanapo tokea mabadiliko hasa ya kihuduma,
Na ukiwa kama mteja usie fuatilia taarifa za tasisi hiyo kwa ukaribu basi ni hakika unaweza kupewa taarifa zisizo za kweli na kuzitumia kwa makosa na baadae zinakughalimu au kukupotezea muda zaidi.
Hivyo rafiki ni muhimu sana Unapo kuwa mteja Au Mwajiriwa wa taasisi fulani kujua na kujifunza zaidi au hata kuhoji zaidi inapo wezekana kutana na watumishi walio ngazi za juu ambao unaona wanaweza kuwa na taarifa hizo unazo hitaji wewe,
Ikiwa itashindikana hapo jaribu kuomba majarida yenye taarifa za huduma za tasisi hiyo hapo unahitaji kuomba taarifa za karibuni na sio za mda mrefu.
Ili uweze kufanya maamuzi yaliyo sahihi kwa manufaa yako binafsi,
Nimuhimu sana kuwa na taarifa muhimu tena zenye ukweli ndani yake usitumie taarifa ulizo zipata juu juu hasa kwa hawa ndugu wenye uvivu wa kujifunza zaidi ya maeneo wanao fanya kazi.
Ushauri wangu pia kwa watu hawa muhimu kwenye maeneo yetu ya maisha,
Ikiwa wewe upo kwenye maeneo ambayo watu wengine wanategemea kupata huduma ili kuboresha maisha yao basi ni miluhimu kujifunza zaidi maeneo mengine ya ajira yako,
Usiishie kwenye maeneo ya nafasi yako pekee Jifunze zaidi,
Hakikisha muda wote unakuwa na taarifa muhimu na zenye ukweli juu ya taasisi unayo fanya nayo kazi na kama huna taarifa hizo muhimu ni kutembea na vipeperushi ambapo sio rahisi kuwekwa taarifa zisizo za kweli.
Hakikisha unaelewa kwa kina mteja wako ananufaikaje na wewe unawezaje kunufaika zaidi ya mshahara.
Labda ni taasisi ya uwekezaji ikiwa utakuwa mvivu wa kutafuta taarifa zaidi huwezi kunufaika na uwekezaji hivyo ni muhimu sana kuyajua maeneo muhimu na namna unavyo weza kunufaika zaidi na kazi unazo fanya kwenye maeneo mbalimbali ya maisha ya wengine.
Mwisho kabisa Mafanikio makubwa yanakuja kwa kutoa zaidi ya unacho lipwa kama ni ajira basi weka juhudi zaidi ili kuona Fursa zingine zinazo zunguka ajira yako ambazo utazitumia kuongeza kipato chako,
Pia kama umejiajiri pia ni muhimu zaidi kuweka juhudi zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa zaidi.
Tuma maoni,changamoto na ushauri wako kwenye sanduku la maoni hapo chini Au kwa simu 0715222989/errynine6@gmail.com
Kila la kheri rafiki yangu.
Na wako Mjasiriamali & Mwandishi
Ernest Lwilla.
Chapisha Maoni