Unknown Unknown Author
Title: Unapaswa Kuyafahamu Mambo Haya (2) Muhimu Na Msingi Kuhusu Dunia.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio, Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima wa afya njema na un...

Habari rafiki na msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima wa afya njema na unaendelea vema na kuwa bora zaidi hasa kwenye kazi ulizo chagua kuwa bora.
Kwa kuamua kuwa bora na tofauti tu hapo ndipo lilipo chumbuko la mafanikio ya watu wengi.

Ikiwa ni siku nyingine muhimu kwetu nitumie nafasi hii ya pekee kukukaribisha kwenye makala yetu ya leo ambapo tutaenda kujifunza mambo mawili muhimu tunayo takiwa kuya fahamu hasa kuhusu Dunia na Binadamu,
Dunia na Binadamu ni vitu viwili tofauti na utofauti huu una nafasi moja muhimu kwetu ya kujifunza zaidi.

Jambo la kwanza Dunia haiko Fair yaani Dunia haina huruma,Haina aibu,Haina chenga wala ubabaishaji.
Watu wengi wamekuwa wakitumia nguvu nyingi sana kuhakikisha wanaenda sambamba na dunia lakini jambo la kushangaza Dunia imekuwa ikiwa angamiza wao,
Unapo kuwa na wazo lolote la kushindana na Dunia sawa na kuingia vitani huku ukiwa na motokeo ya kushindwa na unapo kuwa umeshindwa maana yake unapotezwa kabisa hii ndio maana nasema Dunia haiko fair.

Wapo watu wanao tumia nguvu kubwa sana kuhakikisha wanaidanganya Dunia na kujipatia mafanikio kwa njia za ujanja ujanja lakini huwa haipiti muda mrefu Dunia inachukua jukumu kubwa la kuwapa Adhabu kali,
Mfano:Watu wengi hutafuta njia za mkato zitakazo wafikisha haraka kwenye mafanikio ambapo watu huanza Ujambazi,Utapeli,Udanganyifu nk Dunia huchukua jukumu zito lisilo na huruma la kuwaadhibu watu wa aina hiyo.

Wapo watu wanajidanganya wao wenyewe huku wakidhani wanaidanganya Dunia baada ya muda kidogo kupita Dunia huchukua jukumu lake kama kawaida kuwapa adhabu kali,
Mfano:Upo wakati watu hudai wanakula Bata na kufanya mambo mabaya yanayo enda kinyume na misingi ya maisha yao inaweza kuwa Kufanya Umalaya,Kunywa pombe kwa kuzidisha,Kutumia Madawa ya kulevya nk Dunia jukumu lake ni Moja ni kuwaadhibu hapo huwa haipiti muda mrefu Watu hawa wanapotezwa zaidi.

Pia wapo watu ambao huamini wanafanya mambo ya siri kwa kujidanganya huko huamini kwamba wapo salama na baada ya mda mambo huwa yanakuwa hadharani na dunia inawapa haki wanayo stahili,
Mfano,Watu wengi wamekuwa wakifanya biashara za magendo,Biashara halamu na kujitengenezea faida kubwa sana lakini huwa haipiti muda Dunia inachukua jukumu lake na baadae kupoteza kila kitu kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuliko faida walio itengeneza kwa kipindi chote cha biashhara hiyo.

Jambo moja unalo takiwa kulitambua ni kwamba Dunia haiko fair na kwa namna hiyo hakuna jambo utakalo itadanganya Dunia na ikakuvumilia uendelee kuidanganya ni lazima itakuadhibu kwa namna yoyote,
Wapo watu ambao huamni kwamba Wanaidanganya Dunia lakini hakika ya dunia ni kwamba haidanganyiki hata kidogo hivyo chukua hatua na kujenga mtizamo sahihi juu ya dunia.

Jambo la pili ni Binadamu wako fair lakini ni hatari zaidi kuliko Dunia,
Mafanikio yoyote yanapatikana kupitia watu wengine,Watu tutakao shirikiana nao ili kupata mafanikio,Watu ambao watachukua nafasi ya mafanikio yao na kugusa maisha ya wahitaji,Watu ambao watawagusa watu wa chini na kuwainua kwa namna hii unaona namna gani binadamu wanahuruma sana.

Hili liwe wazi kwa kila mmoja wetu,
Kwamba huwezi kupiga hatua yoyote ya kimafanikio bila kuwa na watu utakao shirikiana nao na kwamba nafasi ya watu wengine kwenye mafanikio yako ni kubwa zaidi kuliko kuliko nafasi yake mwenyewe,
Hii ndiyo siri kuu kwamba mafanikio unayo tafuta kwa nguvu kubwa yapo kwa watu wengine ili uweze kuyapata ni lazima ushirikiane vema na watu hao.

Pamoja na uzuri huo wote wa binadamu kwenye mafanikio usishangae ninapo kwenda kukwambia Binadamu ni hatari zaidi,
Binadamu wengi wana nafasi kubwa ya kukufanikisha mtu kwenye mafanikio yako lakini ni hatari zaidi usipo kuwa makini na watu hao hii ni kwa sababu zifuatazo.

Wapo watu unao weza kushirikiana nao kwanzia chini kabisa,Watu ambao utashirikiana nao vizuri na hivyo kukufahamu kwa ukaribu sana lakini usipo kuwa makini wanaweza kukurudisha nyuma au kukupoteza kabisa hapa Binadamu anaweza
Kukuchezea mchezo ilimladi akurudishe nyuma anaweza kukudhurumu,kukutapeli n.k

Wapo watu unao weza kushirikiana kwa karibu sana hasa pale unapo tafuta wapi uanzie safari yako na hapo unaweza kutafuta kazi ambayo kwako itakuwa ni hatua kubwa ya kuanza safari yako lakini kwa unae mfanyia kazi inakuwa ni fursa yaani anakutengenezea mazingira ya wewe kuendelea kuwepo kwenye kazi yake daima na hivyo utajikuta unapoteza muda wako mwingi na huoni matokeo makubwa ya juhudi zako.
Watu hawa wanaweza kuwa wema sana kwako lakini hatua ya wema huo kwako mala nyingi huwa inawategemea wao kutengeneza faida kubwa zaidi kupitia wewe

Binadamu wengi wako fair sana lakini ni hatari zaidi hasa pale wanapo weka uvumilivu wa mda mrefu na kukosa kile walichotegemea,
Binadamu wengi hufikia hatua za u katili mkubwa sana hasa wanapo onekana kupoteza ushindi na nguvu zao.

Haya ni baadhi ya mambo niliyo hitaji kukuweka wazi rafiki yangu na uwe nayo makini kwenye hatua zako za mafanikio,
Jambo la kwanza ni kuhusu dunia bila shaka nimeweza kuelezea vizuri sana hapo juu ni muhimu sana kuheshimu dunia na kuto idanganya kwa kitu chochote kile,
Tunapaswa kutambua Dunia ilikuwepo na itaendelea kuwepo,
Dunia ipo na itaendelea kuwepo daima na hivyo hakuna siri wala ujanja ujanja kuhusu Dunia na mafanikio yetu.

Jambo lingine la msingi na kubwa ni kuwa tambua binadamu kama watu muhimu sana kwenye mafanikio yetu lakini sio wote ni sahihi kwa mafanikio yetu,
Hii ni kwasababu binadamu wengi ni vigeu geu na hivyo tunapaswa  kuwa makini.
Hivyo rafiki chukua hatua na kuyafanyia kazi mambo haya mawili ili kuweza kufikia mafanikio yetu.

Kila la kheri rafiki yangu,
Na wako Mjasiriamali na Mwandishi

Ernest lwilla

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top