Uhali gani Rafiki na msomaji wa mtando huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu.
Ikiwa ni siku nyingine nzuri kwetu ni nafasi ya pekee kwetu kwenda kuweka nguvu kubwa ili tuweze kupata matokeo yaliyo Makubwa na Bora zaidi.
Ni kukaribishe kwa moyo mkunjufu kwenye makala yetu ya leo ambapo nitaenda kukushirikisha jambo na uamzi wa kuchukua kabla hujafanya maamuzi yoyote kwenye maisha yako ya mafanikio.
Wapo watu wengi wanao umia sana kwa kufanya mambo yao pasipo kuona nafasi ya jambo muhimu nalo kwenda kukushirikisha leo,
Kutokana na hilo basi wamejikuta kwenye maumivu makubwa na kurudishwa nyuma kila wanapo piga hatua kwenda mbele.
Kumbuka haya ni nayo kushirikisha ni yale ni nayo jifunza na kuyaishi kwenye maisha yangu.
Tatizo kubwa la watu wengi wanao ogopa GHALAMA,
Tatizo lingine ni USIRI(UBINAFSI).
Matatizo hayo hapo juu ni kikwazo kikubwa kwa watu wengi na hivyo muda mwingi wanajikuta wakiangukia kwenye maeneo ya hasara na kutapeliwa.
Watu wengi wamekuwa waoga wa kutoa ghalama za maisha ya kila siku kwenye mafanikio yao,
Watu wengi ni waoga wa kutoa ghalama za kufanya uchunguzi wa kina ,
Watu wengi ni waoga wa kutoa ghalama za kuwapa usalama wa hatua za mafanikio yao.
Watu hao hufanya hayo yote wakidhani wana epuka ghalama na hivyo ghalama hizo zinakuwa zinawasaidia kusonga mbele kumbe ndiyo wanajipoteza.
Kundi lingine ni watu ambao wanafanya na kuendesha mambo yao pasipo kushirikisha watu wengine,
Watu hawa mala nyingi huogopa kulipa ghalama za kuwashirikisha watu wengine na hivyo kufanya mambo yao kimya kimya,
Wapo watu wanao fanya hayo kwa kusudi na wengine ni asili yao kufanya mambo kwa usiri lakini jambo la kushangaza USIRI huo umekuwa ukiwa umiza wao wenyewe hasa pale mambo yanapo kwenda tofauti.
Rafiki kuepuka matokeo mabaya ya mambo hayo hapo juu yote nitaenda kukushirikisha jambo muhimu unalo paswa kufanya ili kuendelea kuwa salama siku zote za maisha yako.
Jambo la kwanza ni wewe KUSHIRIKISHA BUSARA ZA WATU,
Sio kila mtu ni sahihi kwako kushirikisha lakini ni muhimu kushirikisha busara za watu hao utakao wachagua,
Ukiwa kama mwanamafanikio ni muhimu sana kuwa na watu wachache wenye busara na hao ndio uwashirikishe hatua zako za mafanikio.
Hakikisha unapo fikiria kufanya jambo lolote kwenye mafanikio yao unawashirikisha na kusikiliza maoni na mitizamo yao hii ni kwa sababu maamuzi yako pekee yanaweza kuwa sio sahihi na hivyo kukuingiza ghalama au hasara kubwa.
Unapo chagua kikundi hiki ni muhimu kuzingatia ufahamu wao juu ya mambo utakayo kuwa unafanya wewe,
Ni muhimu pia kuzingatia wao wamefanya nini kwenye maisha yao ya mafanikio.
Mfano:Unafikiri kufanya uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali ya uwekezaji Eg.Kwenye mashamba,Majengo na hata Hisa ni muhimu kabla hujafikia kununua au kuwekeza chochote kuwashirikisha watu wako walio na busara na kuona mitizamo na maoni yao juu ya hatua hiyo.
Usifanyame maamuzi yoyote ukiwa pekee yako kwa sababu itakuwa rahisi kupoteza,
Ikiwa unahitaji kununua shamba shirikisha watu wako wa busara na kufuata hatua za ushauri wao.
Ikiwa unahitaji kuwekeza kwenye majengo washirikishe watu wako na kisha kufuata hatua za ushauri wao.
Hii itakuwa salama kwako
Lakini ukiwa katika hatua hizo zote usikwepe ghalama na hivyo kufanya mambo kwa mkato au kwa kuto washirikisha watu wenye busara utajikuta unasonga mbele kidogo huku kurudishwa nyuma kukiwa kwingi sana.
Hivyo rafiki yangu kila siku zingatia kufuata hatua hizo hapo juu,
Washirikishe watu wenye busara na Usikwepe Ghalama kwa kufanya mambo kwa mkato.
Kila la kheri rafiki yangu,
Na wako rafiki Ernest Lwilla
Kwamaoni na ushauri 0715222989/errynine6@gmail.com.
Karibu sana.
Chapisha Maoni