Unknown Unknown Author
Title: STOP COMPLAIN PART 1
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Stop Camplain,HILI GAME HALIHITAJI HARAKA WALA HASIRA. Habari Mwanamafanikio mwenzangu? Na msomaji wa ukulasa huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,...

Stop Camplain,HILI GAME HALIHITAJI HARAKA WALA HASIRA.

Habari Mwanamafanikio mwenzangu?
Na msomaji wa ukulasa huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Imani yangu unaendelea vizuri na unaendelea kuongeza juhudi zaidi ili upate matokeo bora.

Karibu kwenye makala hii sehemu ya kwanza.

My Experience
Watu wengi wana haraka na mafanikio wanayo yataka na cha kushangaza mambo uwa yanakuwa tofauti na mipango yao.
Mipango mala zote haijawai kuwa migumu,Ugumu unakuja kwenye utekelezaji hapo ndipo mambo huanza kubadilika mpaka unahisi kunawatu wanakuchora kwenye kazi zako na hivyo wanaharibu kila chanel unayo set.

Fursa Ya Biashara
Fursa hii ni Pana sana na inaboresha na kubadili maisha ya watu wengi sana lakini sio LAHISI,
Biashara ni sawa na maisha ya binadamu,
Maisha ya binadamu yamebebwa na uhai wake ambao unamisingi yake ili uweze kuendelea kuwa hai unahitaji Mzunguko wa dumu usisimame hata DK 1 huku Ukipewa virutubisho muhimu vinavyo fanya afya kuwa bora zaidi.

Hivi ndivyo ilivyo biashara yoyote,
Inapo tokea misingi yake imevunjika basi biashara hii itakufa.
Biashara ili iweze kuwa hai inajitaji Mzunguko wa fedha uwe mzuri na inapo tokea mzunguko wa fedha kusua sua basi biashara hii inaweza kufa zisipo chukuliwa hatua za haraka.
Moyo wa biashara ni Mauzo na mauzo yanapo kuwa madogo basi biashara hii haiwezi kuendelea kuwa hai pia kumbuka wingi wa mauzo au uchache wa mauzo unategemea sana MZUNGUKO WA FEDHA.

Upo wakati Mzunguko wa fedha unapo kuwa mzuri Biashara nyingi mauzo yake yanakuwa makubwa na hivyo kutengeneza faida kubwa sana,
Kwenye kipindi hiki watu wengi hufanya manunuzi ya bidhaa kutokana na mzunguko wake na hata mitaji ya wengi hukua kwenye kipindi hiki.

Lakini watu wengi kwa kuto Lifahamu hili,
Imepelekea kufunguliwa kwa biashara nyingi sana ambazo kipindi cha kudumu kwake kina kuwa kifupi sana na hata ikidumu basi itakuwa ni biashara isiyo kua.
Yaani ni zile biashara za kununua bidhaa,kuuza kupata faida na kutumia fullstop.

Wakati huo huo biashara nyingine zinakuwa ni zile  za kuongeza mtaji kila baada ya miezi sita baada ya muda huo kuisha na fedha walizo weka zinakuwa zimesha isha,
Muda mwingi biashara hizi hata wafanya biashara wenyewe wanakuwa hawaelewi fedha hizi zinaenda wapi?
Lakini wanaongeza fedha zingine kuficha aibu ya kuonekana biashara zao zimekufa.

Ukweli biashara inahitaji virutubisho ili iweze kukua vizuri,
Virutubisho hivi ni mzunguko mzuri wa fedha unapokua mzuri mauzo  yana kuwa makubwa na hivyo kutengeneza faida kubwa.
Hivyo virutubisho hivi msingi wake unatakiwa kutoka kwenye sehemu ya faida,
Yaani biashara inapotengeneza faida kubwa sehemu ya Faida hii inatakiwa kurudi kwenye ununuzi wa bidhaa na hivyo biashara kuendelea kutengeneza faida kubwa zaidi.

Sasa wapo watu mzunguko wa fedha unapo kuwa mdogo kwenye biashara wanataka matumizi yao yaendelee kuwa makubwa kama kipindi mzunguko wa fedha unapo kwa mkubwa ambapo faida inakuwa kubwa na matokeo yake biashara nyingi za mfumo huu zinakufa ndani ya kipindi kisicho zidi miaka miwili.

Tutaendelea sehemu ya pili ya Fursa ya biashara.
Na wako Rafiki
Ernest Lwilla
0715222989/errynine6@gmail.com

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top