STOP COMPLAIN
Tambua Kosa,Fanya marekebisho na Songa mbele
Habari Mwanamafanikio mwenzangu?
Ni imani yangu kuwa ni mzima wa afya njema na unaendelea vema na mapambano ili kuhakikisha uanakuwa na maisha bora.
Karibu tena kwenye makala yetu ya leo ambapo tutaenda kujifunza zaidi hatua zingine zitakazo tufanya kuendelea kufanikiwa kwenye kazi zetu.
Hatua hizi ni Tambua kosa,Fanya marekebisho na Kisha Songa Mbele.
My Experiences
Uhalisia huwezi kufanya jambo lolote kwa usahihi kwa kuepuka makosa yote na kweli yasitokee ni lazima ukosee na ikitokea hujakosea basi ujue wazi hakuna kimya ulicho fanya,
Lakini jambo la kushangaza ni pale mtu anapo chukua hatua na kufanya jambo kubwa na kukosea baada ya kutambua makosa anaishia pale pale au Anakataa tamaa jambo ambalo ni hatari zaidi.
Tambua Kosa
Mtu unapo fanya jambo na kukosea yapo mambo mawili yanayo pelekea kukosea,
Jambo la kwanza ni Ugeni wa jambo unalo fanya.
Hata kama ungekuwa umesoma na kikifahamu kitu nje ndani lakini unapo chukua hatua na kuanza kufanya hapo ndio rasmi unakuwa upo tayari kukijua.
Unapo kuwa umechukua hatua hata kama wewe inauwezo kiasi gani huwezi kufanya kwa usahihi pasipo kukosea,
Ni lazima ukosee na utambue kosa lililo pelekea umepata matokeo hayo hapo ndipo utakuwa umejifunza kiuhalisia na unaweza kuweka umakini usiweze kukosea tena.
Jambo la Pili ni Mazoea,
Kwa sehemu kubwa unapo kuwa umefanya kitu kwa mda mrefu kunatabia mpya inazaliwa ukiwa katika uwajibikaji wako tabia hii inatokana na kukifahamu kitu upande mmoja na hivyo muda mwingi kukifanya kwa mtindo ule ule ulio zoea ambao siku zote Unajua hauwezi kukupa matokeo zaidi ya yale uliyo yazoea.
Jambo hilo hilo siku utakayo fanya tofauti na mazoea hapo ni lazima ukosee kwa sababu umefanya pasipo mazoea.
Marekebisho
Baada ya kutambua kiini cha tatizo lako hatua inayo fuata ni kufanya marekebisho,
Unapo fanya marekebisho huwezi kurekebisha jambo pasipo kujifunza kitu chochote.
Mfano:Una fanya biashara mala kwa mala unapata hasara ambayo hata wewe mwenyewe hutambui kiini chake lakini baada ya Kujichunguza ukatambua Matumizi yako ni makubwa kuliko uzalishaji wako,
Hapo unakuwa umesha Jifunza kuwa Matumizi hayatakiwi kuwa makubwa kwenye biashara na hatua itakayo fuata ni Kupunguza matumizi yote yasiyo ya msingi kwako na hivyo kuwa na matumizi yaliyo chini ya uzalishaji wako.
Hapo ni lazima ukubali kosa lako ndipo utaweza kuweka umakini mkubwa lisitokee tena tatizo kama hilo,
Lakini kama utakuwa uankwepa tatizo hilo ni wazi hata kukifanya marekebisho haitapita mda tena unarudi kwenye mfumo ule ule ulio kupa hasara mwanzoni na hii ndiyo Asili ya akili zetu.
Kubali na kukili kosa lako hata kama ni baishara yako mwenyewe.
Songa Mbele
Baada ya kutambua Kosa lako lililo kughalimu kwenye hicho unacho fanya,
Hatua inayo fuata ni Marekebisho kupitia jambo ulilo jifunza na Baada ya hapo kinacho fuata ni kusonga mbele,
Yaani hupaswi kutumia na kupoteza muda wako mwingi kuona kiini cha tatizo badala yake unatakiwa kubeba funzo na kuendelea na hatua kubwa zaidi kwenye jambo hilo.
Hii ni kwa sababu ikiwa utatumia muda mwingi kuona kiini cha tatizo inaweza kupekea kuharibu hatua zinazo fuata,
Ambapo unaweza kujitia hofu ya kukosea tena na kuto fanya tena jambo jipya kwenye maisha yako.
Unatakiwa kutambua kuwa Marekebisho na funzO la kosa lako la kwanza ni Mwanzo la kosa lingine kwenye hatua inayo fuata kwenye hicho unacho fanya sasa.
Pia hata ukitumia muda mwingi kutizama tatizo bado haikusaidii wewe zaidi inazidi kukupotezea muda wako wanakufikia mazuri zaidi yaliyo mbele yako.
Daima tunazungumzia matokeo bora na yaliyo makubwa kamwe usitegemee matokeo bora au makubwa kama hauta chukua hatua kubwa ambazo zinaweza kuwa na hatari kubwa kwako,
Fanya mambo mapya na makubwa kila siku itakusaidia kukupa uzoefu na kujifunza zaidi.
Tutaendelea sehemu ya tatu ya makala hii wakati mwingine Muhimu zaidi ni kuchukua hatua na kushika hatamu ya maisha yako mwenyewe yaani Usiwe na wakumlaumu iwapo mambo yataenda tofauti zaidi uwe na jambo la kujifunza kisha kusonga mbele.
Kila la kheri rafiki yangu.
Na Ernest Lwilla
Contact: 0715222989/errynine6@gmail.com
Website;www.ufunguowamafanikio.blogspot.com
Chapisha Maoni