Unknown Unknown Author
Title: Hizi Ndizo Sehemu Kuu Mbili Unazo Weza Kujifunza Na Kupata Uzoefu Wa Kufanya Jambo Lolote
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na Mwanamafanikio mwenzangu kupitia Mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio, Ni imani yangu kubwa kuwa nI mzima na unaendelea vem...

Habari rafiki na Mwanamafanikio mwenzangu kupitia Mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Ni imani yangu kubwa kuwa nI mzima na unaendelea vema na mapambano ili kujihakikishia kufanikiwa.

Ni chukue fursa hii kukukaribisha kwa moyo mkunjufu kwenye makala yetu ya leo,
Ambapo nitakwenda kukushirikisha maeneo mawili muhimu unayo weza kupata uzoefu mkubwa wa kufanya jambo lolote ili kuendelea kuwa washindi kwenye maisha yetu.

Mafanikio ni haki yako ya msingi ya kuzaliwa na tangu ulipo zaliwa ulisha kuwa mshindi.

Kwenye maisha ya mafanikio yapo maeneo mengi unayo weza kujifunza na kupata maarifa sahihi yanayo weza kukusaidia wewe kufanikiwa,Lakini pamoja na kuwa na maarifa hayo muhimu bado unapo anza kuchukua hatua ya kufanya jambo lolote Huo unakuwa ni mwanzo wa kujifunza jambo hilo kwa vitendo.

Unaweza kuwa umesoma vitabu vingi sana,Umeangalia video za hamasa nyingi sana na hata sehemu zote zenye maarifa sahihi lakini bado Hujajua jambo hilo kama hujafanya kwa vitendo.

Hivyo leo rafiki yangu Nakwenda kukushirikisha maeneo hayo muhimu ambayo yatakupa uhakika wa safari yako kuwa na mafanikio makubwa.

Sehemu ya kwanza ni  MAKOSA YETU WENYEWE,
Ni wazi kwamba huwezi kufanya jambo pasipo kukosea hata kidogo na kama ikitokea hivyo basi ni wazi hujafanya jambo jipya lolote.

Ili uweze kufikia mafanikio hutakiwi kuwa na kitu kimoja cha kufanya au hakuna kitu kimoja utakacho kifanya chenye uhakika wa kukufikisha kwenye mafanikio badala yake tunatakiwa kufanya mambo mengi yatakayo kuwa na mchango mkubwa wa sisi kufanikiwa.

Hivyo tunatakiwa kufanya mambo mengi tena tusiyo na uzoefu nayo na pindi tunapo kesea hapo ndipo tunajifunza na kupata uzoefu mkubwa wa kufanya mambo hayo,
Huwezi kufanya jambo kwa usahihi kabisa kama jambo hilo ni jipya kwako ila Unapo kosea ndipo unapo jifunza.

Mambo mapya na tusiyo na uzoefu nayo ndiyo yenye mchango mkubwa kwetu kufanya makosa na kujifunza kupitia makosa hayo.

Njia hii ya kupata uzoefu kupitia makosa yetu wenyewe ghalama yake ni kubwa sana na inahitaji muda mwingi,
Ghalama ya njia hii ni kupata hasa au hata kupoteza muda lakini kupitia makosa yanayo tughalimu wenyewe tunapata uzoefu na hata kuto rudia makosa yaliyo tughalimu mwanzoni.

Hivyo huwezi kujifunza wala kupata uzoefu wa kufanya jambo lolote pasipo kulifanya jambo lenyewe,
Pia huwezi kukosea ikiwa utafanya mambo ambayo umesha zoea kufanya ni lazima ufanye mambo mapya ili kujifunza na kupata uzoefu zaidi.

Sehemu ya pili ni MAKOSA NA UZOEFU  WA WATU WENGINE,
Dunia tuliyopo wakati huu huwezi kufanya jambo jipya kwako na likawa jipya kwa watu wote,
Huwezi kufanya jambo ambalo halija wai kabisa kufanywa na hata ikitokea hivyo bado yapo mambo ambayo yanafanana na jambo unalo taka kufanya.

Uzoefu wa watu wengine ni fursa kubwa sana kwetu kujifunza na kupata uzoefu wa kufanya mambo yetu binafsi ambayo yatakuwa na mchango wa sisi kufikia mafanikio yetu,
Makosa ya watu wengine yana nafasi kubwa sana ya kutufundisha na kuhakikisha hatuyarudii makosa ambayo yaliwa ghalimu watu wengine.

Je unajifunza kitu gani unapo ona mtu mwingine anapata hasara kwenye biashara yake na makosa yaliyo tengeneza hasara hiyo una yatambua?
Je unachukua hatua gani kuhakikisha hurudii makosa hayo?
Bila shaka utachukua hatua sahihi na kuhakikisha unayakwepa makosa hayo yasijirudie wala kuyafanya tena kwenye maisha yako.

Ni muhimu sana kushirikiana na watu wengine kwenye safari yetu ya mafanikio ili kupata nafasi ya kutambua na kuyajua mambo mbalimbali wanayo fanya kwenye maisha yao,
Fursa ya kuyajua mambo hayo ni wazi sisi tunakuwa tunajifunza na kupata uzoefu mkubwa utakao tusaidia kwenye maisha.

Kwenye hatua hii ya kupata uzoefu kutoka kwa watu wengine Tunaweza Chagua marafiki wachache wenye mitizamo inayo endana na yetu ambapo tutashirikiana kwa karibu na hivyo inaturahisishia sisi kujifunza.

Ni muhimu sana kutumia makosa ya wengine kama sehemu ya kujifunza na kupata uzoefu wa kufanya.
Njia hii ni rahisi na haina ghalama kubwa kujifunza na kupata uzoefu wa sisi kuwa bora zaidi kwenye maeneo yetu.

Kwenye hatua hii pia unaweza kuchagua watu wachache watakao kuwa viongozi wa maisha yetu nasi tukawalipa ghalama lakini watu hawa wanatakiwa kuwa ni watu wanao fanya kwa vitendo.

Hivyo rafiki hizi ni njia mbili nilizo kuandalia rafiki yangu kwa siku hii ya leo,
Tumia maarifa hayo kuboresha maisha yako na kuweza kuepuka makosa yanayo weza kutughalimu zaidi kwenye maisha na hivyo kuwa kizuizi cha sisi kuto fanikiwa.

Kila la kheri rafiki yangu,
Nikutakie siku njema na yenye mafanikio zaidi.

Na wako Ernest lwilla.
Ushauri na maaoni Tuma ujumbe kwenda 0715222989/errynine6@gmail.com.

Karibu sana.

Sehemu mbili unazo weza kupata uzoefu wa kufanya jambo lolote
@Makosa yetu wenyewe*uzoefu huu unaghalama kubwa na unahitaji mud mwingi sana
@ Uzoefu wa wengine

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top