Habari rafiki na mwanamafanikio mwenzangu?
Unaendeleaje na mapambano ya kuhakikisha maisha yako yanaendelea kuwa bora kila siku na kufanya kwa ubora wa hali ya juu kwenye chochote unachofanya sasa na hata utakacho fanya siku za mbeleni.
Nichukue nafasi ya pekee kukukaribisha kwenye makala yetu ya leo kupitia mtando huu wa Ufunguo Wa Mafanikio ambapo leo nitaenda kukushirikisha jambo moja muhimu zaidi na msingi mkubwa wa kuongeza kipato chako.
Changamoto kubwa kwa watu wengi ni kipato kuto toshereza mahitaji yao ya msingi na hii inatokana na watu wengi kuto utambua msingi muhimu wa kuongeza kipato kwenye mambo wanayo fanya,
Msingi mkubwa na unao amua wewe utengeneze kipato kiasi gani ni huu hapa:
THAMANI,
Thamani ni kitu au vitu tunavyo fanya kila siku ambavyo vinatatua changamoto au kufanya maisha ya watu wengine kuwa bora zaidi kupitia sisi.
Yaani kipato unacho lipwa na kujilipa sasa kina tegemea thamani unayo toa,Ukitoa thamani kubwa ndivyo kipato kinavo kuwa kikubwa zaidi.
Watu wengi wamekuwa wakifanya mambo mengi sana kwenye maisha yao ya kila siku ambayo yamekuwa yakiwaingizia kipato lakini mtindo na njia ya kufanya mambo hayo ndiyo imekuwa ikiamuru thamani yao,
Watu wengi wanapenda kuongeza kipato kwa kufanya mambo yale yale waliyo zoea kufanya na kwa mtindo ule ule jambo ambalo haliwezi kuongeza thamani ya kipato chao zaidi kuendelea kuwa na kipato kile kile wanacho kitengeneza.
Muhimu kufahamu kipato tunacho tengeneza au kulipwa kwenye maisha ya kila siku ni thamani tunazo toa kwa wengine.
THAMANI KUBWA=>KIPATO KIKUBWA.
THAMANI NDOGO=KIPATO KIDOGO.
Hivyo rafiki kwa mtindo huu unapo fikiri kuongeza kipato zaidi fikiri kuongeza thamani zaidi,
Pia unapo fikiri kutoa thamani kubwa tegemea kupata kipato kikubwa zaidi.
Rafiki hakuna mtu anae kuwa tayari kulipa ghalama kubwa kuliko thamani anayo pewa au huduma anayo pewa.
Popote ulipo ni muhimu kuongeza thamani zaidi ili kupata kipato zaidi ya unacho tengeneza sasa,
Ili kuongeza kipato zaidi ni muhimu kuongeza huduma zaidi zitakazo tatua matatizo ya watu wengine kisha nao kukulipa ghalama za huduma hiyo.
Chukua hatua sasa kuongeza thamani ili kuongeza kipato zaidi.
Kila la kheri rafiki yangu na nikutakie siku njema na yenye mafanikio zaidi.
Na rafiki yako
Ernest Lwilla
0715222989/errynine6@gmail.com
Karibu sana.
ONGEZA THAMANI yaani tatua changamoto.
Chapisha Maoni