Unknown Unknown Author
Title: Hii Ndiyo Kanuni Unayo Takiwa Kuitumia Kila Unapo Tenga Fedha Ya Akiba
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari ya leo Rafiki yangu? Ni tumaini langu kuwa ni mzima wa afya njema na Unaendelea na mapambano kuhakikisha una boresha zaidi maisha ya...

Habari ya leo Rafiki yangu?

Ni tumaini langu kuwa ni mzima wa afya njema na Unaendelea na mapambano kuhakikisha una boresha zaidi maisha yako.
Ikiwa ni siku nyinginE nzuri kwetu ni Fursa ya pekee kwetu kwenda kutumia Akili,Nguvu na Maarifa tuliyo nayo kwenye kazi tulizo chagua kufanya ili kuweza kupata matokeo makubwa na yaliyo bora sana.

Ni chukue nafasi hii ya pekee kukukaribisha kwenye makala yetu ya leo kupitia mtandao huu wa UFUNGUO WA MAFANIKIO ambapo ninakwenda kukushirikisha njia bora unayo paswa kutumia kila unapo tenga sehemu ya kipato chako ambacho unaweka akiba.

Changamoto kubwa sana kwa watu ni Elimu juu ya Fedha na Hata Umuhimu wa akiba kwenye maisha yao,
Lakini changamoto nyingine kubwa sana ni namna ya kutenga kipato kwa ajili ya akiba zao na Baadhi hata kutambua matumizi sahihi ya akiba zao.

Nimekuwa nikipata maswali mengi sana kutoka kwa watu wanao fuatilia masomo yangu Mfano:Nitumie njia gani kutenga akiba yangu?
Je ni matumizi yapi sahihi kwa fedha ninayo weka akiba?
Je njia ipi ni sahihi kwangu kuweka Akiba?
Na hivyo rafiki leo nita jibu swali la kwanza hapo juu na makala zitakazo fuata nitajibu  maswali mengine yote.

Watu wengi wapo kwenye changamoto hii ya kuto tambua njia ya kuweka akiba kila wanapo pata kipato chao na Hivyo wamekuwa wakifanya makosa makubwa sana ambayo yamekuwa yakiwa potezea sana muda pasipo kufikia malengo yao ya kuweka akiba.

Moja ya makosa hayo makubwa ni pamoja na   PATO,MATUMIZI,AKIBA,
Hili ndilo kosa linalo waghalimu watu wengi na baadae kujikuta kipato chao chote kimeishia kwenye matumizi na hivyo kukosa pesa ya kuweka akiba,
Kosa hili ni kwa watu wengi sana na hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya kipato chao kina kuwa kimesha tumika hata kabla hawana pesa mkononi.

Rafiki hilo ni kosa na hivyo unatakiwa kuliepuka na kuanza kutumia kanuni hii ninayo kwenda kukushirikisha hapa.

Kanuni hii ni KIPATO,AKIBA,MATUMIZI,
Hii ndiyo siri kubwa inayo weza kukupa uhakika wa kuweka akiba pasipo wasisi wala kutoa sababu,
Muhimu sana kutambua kipato chako kisha kutambua asilimia utakazo tenga kwenye kipato chako kwa ajiri ya akiba kisha kufanya matumizi hii ni kwa sababu Muda mwingine unaweza kuwa na matumizi makubwa yanayo zidi kipato chako na hivyo kwa sababu kuweka akiba hijajijengea tabia hiyo basi ni rahisi kutumia kipato chote bila kuweka akiba.

Mfano:Kipato changu kwa upande wa faida pekee ni Tsh 500,000,Hivyo nimejiwekea utaratibu wa kuweka akiba 10% za kipato hicho ambayo sawa na Tsh 50000%,
Hivyo kabla sija anza kuigawa fedha yangu kwenye makundi mengine na hakikisha nimesha tenga fungu hili la akiba.

Kwa namna hii nimekuwa nikiweka nidhamu kubwa sana kwenye hii kwa sababu muda mwingine nitakuwa na mambo mengi ya kufanya ambayo hadi kipato changu hakitoshi.

Hivyo rafiki yangu,
Ni imani yangu kubwa kuwa huto rudia makosa ambayo umekuwa ukifanya kila ulipo hitaji kuweka akiba ambapo Ulitumia Kanuni inayo kupa uwezekano mdogo wa kuweka akiba tena kwa kiwango kisicho sahihi.

Tumia kanuni hiyo niliyo kushirikisha hapo juu ili kuwa na uhakika wa kuweka akiba kila mwezi na kila mwaka ambapo akiba hizo utazitumia baadae kwa ajiri ya kuboresha maisha yako ya mafanikio.

Chukua hatua sasa na uweze kubadilisha maisha yako.

Nikukaribishe kwenye tovuti hii uweze kupata masomo mengine kila siku www.ufunguowamafanikio.blogspot.com
Pia kwa changamoto na Ushauri zaidi wasiliana nami moja kwa moja kwa simu 0715222989 WhatsApp,07429620158 Talk/errynine6@gmail.com

Kila la kheri na karibu sana rafiki yangu.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top