Habari rafiki na mwanamafanikio mwenzangu kupitia Mtandao wa UFUNGUO WA MAFANIKIO?
Hongera sana kwa kuendelea kuwa karibu na maandiko haya Muhimu ni kuyafanyia kazi ili uweze kuona matokeo mazuri.
Ikiwa ni siku nyingine nzuri sana kwetu ni Fursa ya pekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa zaidi ili kuweza kupata matokeo yaliyo mazuri na makubwa zaidi.
Nichukue nafasi hii ya pekee kukukaribisha kwenye makala hii tuongozane mpaka mwisho.
Ahsanteni kwa wote mlio weza kuniuliza maswali juu ya sehemu sahihi ya kuweza kuweka fedha zetu za Akiba na Malengo mbalimbali,
Mala zote jibu langu lilikuwa SEHEMU ZOTE NI SAHIHI UKIWA NA NIDHAMU BINAFSI,
Lakini jibu hili hali kuwa tiba kwa wengi kutokana na kukosa nidhamu binafsi na hivyo imeendelea kuwa changamoto kubwa kwa wengi na hivyo leo nimekuandalia somo litakalo kuwa na suluhisho la kweli kwenye kufikia mipango yako ya kifedha.
Watu wengi wamekuwa wakifungua Account kwenye mabank wakiamini njia hii itawasaidia kufikia mipango yao ya kifedha lakini bado imekuwa haina msaada kwao hii ni kutokana na kukosa nidhamu binafsi lakini pia kuto elewa matumizi sahihi ya fedha zao za akiba.
Na wengine wamekuwa wakiweka fedha kwenye account zao za simu lakini bado imekuwa changamoto kubwa na hivyo kujikuta wakitoa fedha hizo pasipo mipango iliyo wafanya kuanzisha akiba hizo,
Hivyo rafiki Nakwenda kukufungua juu ya gereza unalo takiwa kuzifungia fedha zako ili kuweza kufikia mipango yako ya kifedha.
Gereza hili ni AKAUNTI ZA MIPANGO AU MALENGO,
Hili ndilo Gereza Unalo takiwa kuzifungia fedha zako.
Account hii haikuruhusu kutoa fedha mpaka pale unatakapo fika muda ulio jiwekea wewe Mfano:Unaweza kufungua acciunt utakayo weka fedha pasipo kutoa hata kidogo kwa miaka mitano mfululizo na hivyo hutapewa card ya acount hiyo mpaka muda huo utakapo fika.
Ni kweli zipo changamoto nyingi sana hasa linapo kuja swala la fedha,
Unaweza kufungua acount leo na kuweka akiba kwa muda mrefu lakini linapo kuja jambo fulani hata kama sio muhimu basi akili inakuwa rahisi kulitolea maamuzi tena yaliyo ya hovyo na kutoa akiba hizo kwa kufanyia mambo yasiyo muhimu kwako,
Sasa ili uweze kufikia mpango wako ni lazima ujitoe kikamilifu na kuweka nidhamu kubwa sana kwenye fedha na inapo tokea huwezi basi Chukua hatua hii kufungua jera kwa ajiri ya fedha zako.
Unapo chukua hatua hii hakikisha unafungua account inayo toa riba nzuri kwa kipindi utakacho kuwa umeamua kuweka fedha zako.
Hii Itakuepusha na changamoto mbalimbali za kifedha ambazo wenda zimekuwa zikikuzuia kupiga hatua kwa muda mrefu.
Pia unapo chukua hatua hii ni muhimu kutambua Kusudi la kufungua account hii na kujiwekea kiwango cha muda ulio jiwekea kuhakikisha unafikia lengo lako,
Yaani Mfano,Lengo lako ni kukusanya fedha kiasi cha Milioni 10 kwa mwaka mzima,
Unacho takiwa kufahamu ni kiasi unacho takiwa kukusanya kwa Mwezi,Wiki na kisha Siku kisha anza kufanyia kazi mpango huo na kiasi hicho kukiweka kwenye acount hii ya mpango wako ambayo huto ruhusiwa kutoa fedha mpaka mwaka uishe ndipo utatoa fedha zako.
Karibu sana na chukua hatua sasa kufanyia kazi somo hili ikiwa kweli umeshindwa kabisa kujiwekea nidhamu kwenye maisha yako ya mafanikio,
Ni imani yangu kubwa kuwa njia hii itakusaidia kwa 100% Ikiwa utaweka nidhamu ya kufanyia kazi mpango wako na hata kuweka akiba hizo kila siku.
Kila la kheri rafiki yangu,
Nikutakie safari njema kuelekea mafanikio yako.
Kwa ushauri na maoni kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yako.
Tuma ujumbe kwenda 0715222989/errynine6@gmail.com
Kisha ntakujibu na kukushauri kwa ukaribu sana na kuhakikisha ushauri ninao kupa unakusaidia.
Karibu sana na wako rafiki ERNEST LWILLA,
Chapisha Maoni