Habari Rafiki yangu?
Ni imani yangu kubwa kuwa umekuwa unaweka juhudi kila siku ili kuendelea kutengeneza nafasi kubwa ya wewe kufikia mafanikio makubwa na kufikia kiwango cha juu cha maisha kuwa bora.
Karibu rafiki yangu kwenye makala yetu ya leo ambapo Nakwenda kukukabidhi Siraha na ngao kubwa utakayo itumia kwenye kila hali ya maisha yako hasa pale unapo kuwa Unachukua hatua kubwa zaidi.
Ni wazi kuwa kila binadamu anataka kuwa mshindi kwenye kila eneo analo weka nguvu zake,
Ni wazi kuwa kila binadamu anatamani kufanya mambo makubwa na yatakayo mpa matokeo makubwa zaidi lakini kila wanapo chukua hatua hizo mambo huenda tofauti na matarajio na kuishia kwenye ulimwengu wa kukataa tamaa.
Ipo siri na siraha kubwa inayo tumiawa na watu wengi na hata kuwa wezesha wao kufikia ushindi mkubwa kwenye kila jambo wanalo kuwa wanafanya na hata kuonekana wana bahati kwenye safari yao ya mafanikio,
Jambo hilo unatakiwa ulifahamu wewe rafiki yangu ili nawe uwe na bahati ya kufanikiwa kwenye kila jambo unalo fanya.
Watu wengi wamekuwa wakifanya Makosa makubwa kila wanapo panga kuchukua hatua dhidi ya maisha yao na makosa hayo yamekuwa yakiwapa matokeo tofauti na hata kushindwa kufikia makusudi yao yaliyo wasukuma kuchukua hatua,
Makosa hayo makubwa yamekuwa yakiwa ghalimu na hata kuwaacha kwenye hali ya majuto makubwa licha ya majuto hayo kuwaongezea maumivu zaidi.
Makosa hayo pia yamekuwa yakiwa tenga na familia zao hata kuishi mbali na watu wao wa karibu.
Karibu rafiki nikupe siri,
Siri hii ni WEWE KUWA MSHINDI KABLA HUJACHUKUA HATUA NA KUJIAMINI,
Hii ndiyo siri inayo wapa watu wengi kuwa washindi,
Washindi wengi wanachukua hatua kubwa na za hatari wakiwa tayari wana ushindi hata kabla hawaja chukua hatua.
Pia kujiamini kumekuwa ndiyo ngao imara ya washindi wengi kushinda,
Mfano;Upo wakati ambao nimekuwa nikipitia matatizo na changamoto nyingi sana lakini nimekuwa nikijiamini na kuwa mshindi hata kabla sijachukua hatua ya kukabiliana na hali hiyo na baada ya kuchukua hatua mambo kuwa magumu lakini nimekuwa nikishinda.
Upo wakati Natakiwa kufanya jambo fulani ambalo ni kubwa na muda mwingine limekuwa likinipa hofu nakuona sita weza lakini nimekuwa nikitumia siraha hii hata kabla sijachukua hatua na baada ya kuchukua hatua nimekuwa nikishinda mala zote.
Ushindi wangu umekuwa ni mdogo mdogo lakini ni wenye mapito magumu na changamoto kubwa.
Rafiki kujiamini na kuamini kuwa utashinda ni ushindi mkubwa unao takiwa kuanza nao kila unapo chukua hatua kwenye safari ya maisha yako hii itakufanya kuwa na hamasa ya kuendelea kufanya hata mambo yanapo kuwa magumu kwako,
Hii itakufanya safari yako kuwa na ushindi mkubwa wa matokeo ya kivitendo.
Rafiki usichue hatua ukiwa na wasiwasi,
Usichukue hatua ukiwa na woga,Usichukue hatua ukiwa umesha shindwa badala yake kuwa mshindi kabla hujachukua hatua na jiamini kwa kila hatua.
Epuka kabisa kujiambia siwezi kufanya hivi ila jiulize Nitawezaje kufanya hivi kisha chukua hatua,
Ukiwa utajiambia huwezi kufanya ni wazi huto weza kufanya jambo hilo bora u ache kuliko kupoteza muda hukua Unajua kwamba unashindwa.
Rafiki WEWE NI MSHINDI,
Chukua kila hatua ukiwa na ushindi mkubwa na jiamini kwa kila hatua na Utakuwa mshindi,
Tumia siraha hii kila unapo chukua hatua ili kuwa mshindi na mwenye bahati ya kushinda kwenye kila hatua za maisha yako.
Kila la kheri rafiki yangu,
Na wako rafiki katika mafanikio.
Ernest Lwilla
Contacts:0715222989/errynine6@gmail.com
Kwa ushauri na Maoni.
Karibu sana.
Chapisha Maoni