Unknown Unknown Author
Title: Fanya Kitu Hiki Mara Kwa Mara Ili Kuendelea Kuwa Bora Kila Siku
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari Mwanamafanikio Mwenzangu kupitia Mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio? Ni yangu imani kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu....

Habari Mwanamafanikio Mwenzangu kupitia Mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio?
Ni yangu imani kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu.

Ni nafasi nyingine nzuri na yapekee kwetu sote kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuendelea kutengeneza nafasi ya kufikia mafanikio yaliyo makubwa.

Nichukue nafsi hii kukukaribisha kwa moyo mkunjufu kwenye makala yetu ya leo ambapo Nakwenda kukushirikisha jambo muhimu litakalo kufanya kuwa na hamasa muda wote na hata kuendelea kuwa bora katika kujifunza kila siku ya maisha yako,
Zaidi utakuwa umetoa mchango mkubwa kwa wengine katika kubadilisha maisha yao.

Yapo mambo mengi  na njia nyingi unazo weza kufanya kwenye maisha ya kila siku na ukaweza kuendelea kuwa bora na kuwa na hamasa kubwa ya kufanya jambo ulilo amua mufanya,
Lakini changamoto ya njia hizo ni kwamba unakuwa unajiamulia wewe na hata usipo fanya bado hakuna anae weza kukulaumu au kukulazimisha.

Njia hii ninayo kwenda kukushirikisha leo Utafanya kwa upendo wako huku ukiendelea kuwa bora kwa jambo lolote na kuwa na hamasa za kuendelea kufanya jambo lolote hata unapo kutana na ugumu.

Jambo hili ni KUTOA ELIMU NA HAMAISHA KWA WENGINE,
Hii ndiyo njia bora ya wewe kuelewa vizuri kila jambo unalo jifunza,Kufanyia kazi mambo unayo jifunza na hata kuendelea kuwa na hamasa muda wote.

Maisha yetu yanabadilishwa na mafundisho kutoka kwa wengine nasi tuna nafasi ya kubadilisha maisha ya wengine kwa njia ya wao kujifunza kupitia sisi,
Maisha yetu ni Darasa kubwa sana kwa watu wengine ikiwa tutaamua kuwafundiaha yale tunayo jifunza na kufanyia kazi na hata uzoefu tunao upata baada ya kufanyia kazi yale tunayo jifunza.

Kuna mambo mengi tunayo jifunza kupitia hatua zetu na hata kupitia hatua za watu wa karibu yetu,
Pia tunajifunza mambo mengi ambayo muda mwingine usipo ya shirikisha kwa wengi hata wewe mwenyewe huwezi kunufaika nayo.

Njia unayo takiwa kuitumia ili kuweza kuwa shirikisha wengine yale unayo jifunza na hata Uzoefu wako ni kupitia mitandao ya kijamii au njia nyingine.

Mfano;Kwa kufungua kulasa maalumu Eg,Twitter,Facebook,Istagram za kuwashirikisha wengine hatua zako za kila jambo unalo fanya au kujifunza,Kuwa na kundi la WhatsApp ambapo unaweza kuwa na watu wa chache ambao kila siku utawashirikisha  yale uliyo jifunza na hata Uliyo Na uzoefu nayo,
Pia kwa kufungua blogu kama hii ya Ufunguo Wa Mafanikio na kisha kuwa shirikisha watu yale unayo jifunza na kufanya wewe.

Kwa njia hii muda wote unakuwa ni mtu wa kujifunza na kufanyia kazi yale unayo jifunza,
Pia kwa njia hii inakuwa na hamasa muda wote kwa sababu Unakuwa tayari umesha tengeneza watu wenye mtizamo kama wako na wanao amini katika juhudi zako.

Njia hizi zote zinakufanya kuendelea kuweka juhudi na kupambana ili kupata matokeo bora hata mambo yanapo kuwa magumu sana kwako,
Pia mambo yanapo kuwa magumu zaidi kwako na kuyatatua ndivyo unavyo zidi kupata mambo mengi ya kuwa shirikiksha wengine.

Hivyo rafiki chukua hatua sasa na Anza kubadilisha maisha ya wengine kwa kuwa shirikisha hatua za maisha yako,
Hakikisha makosa unayo fanya wewe na kukighalimu wewe yasiwa ghalimu na wengine kupitia wewe kuwa fundisha.

Chukua hatua sasa rafiki yangu,
Nikutakie kila la kheri rafiki yangu katika kujipa jukumu hilo ambalo halita kuwa rahisi kwako hasa kwa siku za mwanzoni.

Na wako rafiki katika maisha ya mafanikio,
Ernest Lwilla,
Kwa ushauri na maoni
Wasiliana nami kwa 0715222989/Errynine6@gmail.com

Karibu sana rafiki yangu.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top