Unknown Unknown Author
Title: Hili Ndo Vazi Unalo Takiwa Kuvaa Wakati Wa Mapambano Na Hata Baada Ya Kuwa Mshindi.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na Mwanamafanikio mwenzangu kupitia Mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio, Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima na Unaendelea vem...

Habari rafiki na Mwanamafanikio mwenzangu kupitia Mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima na Unaendelea vema na mapambano ili kujihakikishia ushindi wa kufanikiwa kwenye maisha yako.

Hii ni Siku nyingine na iliyo ya pekee kwetu,
Ni Fursa ya sisi kwenda kuweka Nguvu kubwa ili tuweze kupata matokeo yaliyo bora,
Pia ni nafsi ya pekee kwetu kwenda kuitumia fursa ya kuwa hai ambapo wapo wengi ambao hawajafanikiwa kuiona siku hii ya leo hivyo ni muhimu kwenda kuweka alama ya wewe kuwa hai leo.

Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye makala yetu ya leo na tuongozane pamoja mpaka mwisho wa somo letu,
Ambapo nitakwenda kukushirikisha jambo muhimu tunalo paswa kuwa nalo mwanzo mpaka mwisho wa safari yetu ya mafanikio.

Dunia inaendesha mambo yake kiasili,
Binadamu tunaendesha mambo yetu kwa namna ya hatua ambazo tumesha piga kwenye maisha yetu hii ni kwa hatua zetu binafsi na hata za watu wengine.

Dunia,
Pamoja na kujiendesha kiasili bado kunasheria ambazo inatumia kutuongoza kiasili binadamu ambazo tukizifuata maisha yetu yatakuwa bora zaidi na hakuna mtu anae weza kuvunja sheria hizi na akawa salama.

Nisikuchoshe rafiki,
Nikukaribishe kwenye somo letu ambapo Nakwenda kukushirikisha Vazi unalo takiwa kuliva wakati wa mapambano yako na hata baada ya wewe kuwa mshindi yaani kufikia kusudi lako.

Vazi hili rafiki ni UJASIRI kwenye maisha ya mafanikio hakuna hatua wala jambo ambalo linaweza kuja kirahisi hata ingekuwa jambo tunalo fanya ni rahisi,
Hii ni Sheria ya asili ya Dunia.

Ikiwa utakuwa mwoga au mnyonge kwenye hatua za  mapambano yako kuelekea mafanikio ya maisha yako ni wazi huwezi kufanikiwa,
Badala yake utakuwa nyenzo ya watu wengine kufanikiwa kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yao huku wewe ukiendelea kuwa na hali isiyo na matumaini ya kufanikiwa.

Tizama hata wanyama wa wapo porini mnyama anae kosa ujasiri na kuto jiamini ndie anae onewa mala zote huku wanyama wenye ujasiri wakiendelea kuishi maisha mazuri.

Hii inamaana gani rafiki?
Ikiwa utakosa ujasiri wa kuchukua hatua kwenye maisha yako na kusimama Imara kwenye mapambano sio rahisi kupata unacho kitafuta badala yake watabata watu walio jasiri,
Kwa namna hii hata baada ya kufikia mafanikio makubwa watu wengi huendelea kuwa jasiri na wenye kujiamini kwa sababu ikiwa watakuwa wanyonge watapoteza hata mafanikio waliyo kuwa nayo.

Rafiki hakuna jambo ambalo utalifanya leo kilelemama na likakufikisha kwenye mafanikio makubwa na kuendelea kuwa na mafanikio pasipo kuwa na ijasiri,
Angalia watu wenye mafanikio makubwa kwenye jamii zetu ni watu wanao jituma,Ni watu wanao jiamini,Ni watu wanao jitoa kwa kiasi kikubwa hii ni ishara kwamba mafanikio yanataka uwe jasiri ndipo uweze kufanikiwa kwenye jambo lolote.

Ujasiri huo unatakiwa kuwa nao kwenye maeneo yote ya maisha yako iwe ni biashara,Kazi,Ajira,Uwekezaji nk ni lazima uwe jasiri ndipo upate matokeo mazuri,
Ikiwa huto kuwa jasiri huto weza kupiga hatua kwa sababu utakuwa ni mtu wa kuonewa daima kwenye maisha yako yote.

Hivyo rafiki yangu tambua kuwa ujasiri ndio ushindi unao takiwa kuuvaa mwanzo mpaka mwisho wa safari yako ya maisha ya hapa duniani,
Kwa kuwa jasiri ni Fursa ya wewe kuwa mshindi kwenye kila jambo yaani UTATAWALA na sio KUTAWALIWA.

Je umesha vaa ujasiri kiasi gani utakao kupa ushindi kwenye maisha ya mapambano mpaka wewe kufikia ushindi mkubwa na wenye alama isiyo futika hapa Dunini?
Chukua hatua sasa na Anza kujijengea tabia ya kuwa jasiri kwenye kila hatua ya maisha yako,Ujasiri huo utakupa matokeo unayo yataka wewe hata ukiwa na changamoto kiasi gani bado ujasiri huo utakuwa nguzo kwako na kuto yumbishwa mpaka mwisho wa safari yako.

Kila la kheri rafiki yangu,
Nikutakie safari njema kuelekea mafanikio yako ambapo huwezi kuwa mshindi bila kuwa jasiri.

Karibu sana kwa ushauri na maoni yako Tuma kupitia 0715222989/errynine6@gmail.com
au Tuma Ujumbe WhatsApp BIG KEY OF SUCCESSFULL2017 uweze kuungana na wanamafanikio wengine BURE.

Ni wako MJasiriamali & Mwandishi

Ernest Lwilla.
0715222989.




About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top