Habari ya asubuhi ya leo Mwanamafanikio mwenzangu?
Je Umesha Amka au bado unaendelea kuvuta shuka?
Ni imani yangu kuwa umesha Amka tayari kwa maandalizi ya siku hii ya leo ili kujihakikishia ushindi wako,
Na ushindi huu unaanzia asubuhi mapema kabisa.
Ikiwa ni siku nyingine ya kheri kwetu kuwa hai ni Fursa ya pekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kuweka alama ya kudumu kwenye maisha yetu kama alama ya sisi kuwa hai kwa siku hii ya leo.
Na kwa Fursa hii nitaenda kukushirikisha na kukumbusha jambo muhimu sana kwetu kwenye biashara zetu,
Sio jambo Baya ikiwa utakuwa umeaandaa mfumo mzuri lakini ni jambo hatari zaidi ikiwa utalifanya kwa mazoea mwenye biashara yako,
Wapo watu ambao wamekuwa wakifanya makosa makubwa katika kutengeneza misingi ya biashara zao hasa zinapo kuwa changa na hii hufanywa kwa namna ya kupata wanunuzi wa bidhaa mapema huku akili kwao wakiwa na Imani ya kubadilisha misingi hiyo watakapo kuwa na wateja wa kutosha kwenye biashara zao,
Lakini bahati mbaya sana baada ya kuwa na wateja huwa inakuwa ngumu sana kuivunja misingi hiyo na kuanza kutengeneza misingi mingine
Kila biashara na kwa kila mmiliki wa biashara anawajibu mkubwa wa kutengeneza misingi imara ya biashara yake ingali Changa na misingi huwa ni vizuri zaidi kusimamiwa kwa ukaribu zaidi hata biashara Inapo kuwa imekuwa ni muhimu zaidi kuisimamia misingi kwa ustawi wa biashara yako
Mala nyingi unapo vunja misingi uliyo anza nayo basi kuna watu utawapoteza na kuna watu utakwenda nao vizuri na kuna watu watakuwa wakosoaji juu ya hilo na kuona kama hujawatendea haki na kwa hakika inakuwa kweli hujawatendelea haki japo mabadiliko ni muhimu kwa biashara yoyote inayo kua.
Leo nitaenda kukushirikisha msingi mmoja ambao kwa sehemu kubwa Umekuwa Ukinighalimu mimi kwenye biashara ya ninayo ifanya sasa.
Msingi huu ni WATEJA KUCHUKUA BIDHAA PASIPO MALIPO NA BAADAE KULIPA BAADA YA KUUZA BIDHAA.
Huu ndio msingi nitakao kwenda kukushirikisha asubuhi ya leo,
Zipo njia nyingi unazo weza kutumia kwa kipindi cha awali hasa unapo Anza biashara ili tu uweze kupata wanunuzi wa bidhaa yako,
Lakini pia zipo njia nyingi utakazo zikuta zikiwa tayari zinatumiwa na watu wengine wanao fanya biashara kama unayo taka kuanza wewe na hivyo Inahitaji maamuzi magumu ambayo yatatumika kwako katika kutengeneza msingi imara wa biashara yako pasipo kuiga mifumo ambayo tayari inatumiwa na wengine
Na kwa namna ya kupata wateja kirahisi wengi huwa hatuna nafasi ya kuruhusu akili zetu kifikiri kwa kina badala yake unaingia kwa kuiga misingi inayo tumiwa na wengine tungali bado hatua uzoefu na biashara tunazo kwenda kuzianza.
Rafiki Epuka kosa la kwenda kuanza msingi kwa kuangalia wengine wanafanya nini?
Badala yake angalia wewe utafanya nini?
Msingi wa wateja kuchukua bidhaa na baadae kufanya malipo baada ya kuuza ni msingi mbovu kwa biashara changa na hata zenye muda mrefu,
Hii ni kwa sababu nyakati zinabadilika kwa wateja na wateja wenyewe wanalazimika kubadilika kutokana na mabadiliko
Kwa namna hiyo unapo kuwa umetengeneza msingi wa mteja kuchukua bidhaa na baadae kufanya malipo unakuwa kwenye hatari ya kukwamishwa hasa mambo yanapo badilika kwa wateja wako
Na inapo tokea wewe kufanya manunuzi ya bidhaa nyingine ili uweze kuwa hudumia wateja walio wachache wanao Nunua kwa fedha mkononi inakuwa ngumu kwa sababu fedha zingine zinakuwa kwa watu.
Mfano;Wateja kumi wamechukua bidhaa kila mteja amechukua bidhaa za laki 1 kwa wateja kumi sawa na Milion 1 ambapo huwezi kuipata hiyo milion moja kwa wakati mmoja,
Hii ni kwa sababu kila mtu anakuwa na soko la biashara yake
Ambao kila mmoja anarejesha kwa wakati wake na kwa mtindo wake,
Kwa namna hii unafikia hatua ya kupiga hesabu za fedha kwenye biashara yako lakini Fedha hizo huna mkononi zote zipo kwa wateja wako na unapo chukua hatua ya kuzikusanya bado mambo yatakuwa tofauti na hivyo kuangushwa kwenye biashara Au Biashara hiyo inakufa.
Hii imekuwa kiini tokea sana mimi,
Kwa sababu wateja wengi wanasura za huruma wanapo hitaji msaada wa namna hiyo lakini unapo kuwa umewapa wanabadilika au wanakutana na ugumu mkubwa ambao hauta wapa uhuru wa kufanya malipo kwa haraka.
Hivyo rafiki,
Unapo kwenda kuanza biashara yoyote ni Muhimu kusimamia misingi utakayo kwenda nayo mpaka biashara inapo kuwa inakua,
Usiingie kwenye biashara na kufuata misingi ambayo tayari kuna watu wanaitumia kwa sababu huto weza kuwa jua wateja wazuri na wabaya unao weza kwenda nao vizuri kwa misingi ambayo tayari umeikuta sokoni
Pia haita kuwa rahisi kwako kulitambua tabia za wateja wako kwa kipindi hicho cha mwanzoni na hivyo ipo hatari kubwa ya kuzulumiwa na wateja hao.
Hatua muhimu sasa kwangu na kwako ni kuuza kwa pesa mkononi,
Anza kutengeneza misingi upya itakayo wafanya wateja wote watoe pesa wafanyapo manunuzi yao,
Haita kuwa rahisi mwanzoni kwa sababu ya mfumo ulio kuwa unautumia lakini watu wakisha kuzoea na kwamba huwa hutoi bidhaa bila fedha hakuna atakae kuja kukopa kwenye biashara yako.
Kesho Nitamushirikisha juu ya nini ufanye baada ya kuvunja msingi huo wa mteja kuchukua bidhaa na kisha kufanya malipo baada ya kuuza bidhaa
Na kuanza kuuza kwa fedha ya mkononi bila kuathiri mauzo ya biashara yako.
Kila la kheri rafiki yangu,
Na wako rafiki katika mafanikio
Ernest Lwilla
Contact:0715222989/errynine6@gmail.com
Website; www.ufunguowamafanikio.blogspot.com
Karibu sana rafiki
Chapisha Maoni