Unknown Unknown Author
Title: Epuka Kufanya Jambo Hili Kila Unapo Jikuta Kwenye Wakati Mgumu Kwenye Kila Eneo La Maisha Yako
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na hongera kwa kupata nafasi nyingine ambayo unaendelea kuweka juhudi ili kuhakikisha maisha yako yanakuwa bora zaodi, Ni ima...

Habari rafiki na hongera kwa kupata nafasi nyingine ambayo unaendelea kuweka juhudi ili kuhakikisha maisha yako yanakuwa bora zaodi,
Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu.

Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwa moyo mkunjufu  kwenye makala yetu ya leo ambapo tutakwenda kujifunza pamoja juu ya jambo moja unalo takiwa kulikwepa pindi uwapo katika wakati mgumu kwenye kila eneo la maisha yako na hata Hatua ya kuchukua ili kuondokana na hali hiyo.

Ni anze kwa kusema Safari ya maisha haijanyoka moja kwa moja,
Pia haina maana ukichukua hatua basi utakuwa na uhakika wa asilimia mia kuwa utafanikiwa.

Safari ya mafanikio inahusisha vitu vingi sana Upo wakati utapitia hali nzuri zaidi na kuifurahia hali hiyo,
Upo wakati unapitia magumu kiasi cha kukata tamaa ya kupambana lakini bado inakuwa sio njia sahihi kwako kupiga hatua kelekea mafanikio.

Changamoto ndio msingi mkubwa wa watu wengi kufikia mafanikio yao,Unapo pata changamoto unakuwa imara zaidi,Unapo pata changamoto unakuwa na uwezo mkubwa sana wa kufikiri,Unapo patwa na changamoto unakuwa tofauti na mala ya kwanza ikiwa utaitatua changamoto hiyo.

Katika kupitia hali hizo zote katika safari yako zipo namna nyingi unazo weza kutumia ili kuondoka kwenye hali hiyo,
Zipo njia zinazo ondoa tatizo kwa muda mfumo na zipo njia zinazo ondoa tatizo kwa mda mrefu lakini ni ghalama zaidi kwani ni lazima ujitoe.

Rafiki Unapo jikuta kwenye hatua yoyote ambayo sio nzuri kwako basi ni muhimu kujipa muda na kujitafakari mwenyewe na kuona namna unavyo weza kuendelea na safari pasipo kuongeza tatizo,
Unapo jikuta kwenye hali yoyote au Unapo kuwa kwenye Ugumu wowote usikimilie kutumia utatuzi wa muda mfupi badala yake tumia utatuzi wa muda mrefu zaidi.

Mfano:Unapo jikuta umepata hasara kwenye biashara yako Usikimbilie kukopa kama njia ya kutatua tatizo badala yake Kaa chini jipe muda,Utafakari na Utengeneze mkakati mzuri utakao kuwa na suluhisho la mda mrefu,
Usiendelee kuchimba shimo baada ya kujitambua upo shimoni badala yake angalia unatokaje hapo kwa njia hii utaepuka matatizo mengi ambayo yangeweza kuku ghalimu.

Mfano mwingine ni Pale Unapo jikuta kwenye Hali ngumu kimahusiano usikimbilie kuachana na mahusiano yako badala yake jipe muda na tafakari kwa kina,Tambua visababishi mpaka kufikia hatua hiyo,Ona wewe umechangia kwa kiasi gani kufikia hatua hiyo kisha tengeneza mkakati mzuri utakao kuwa na suluhisho la kudumu na sio kuchukua hatua inayo punguza tatizo na baadae kujirudia.

Muhimu zaidi ni kujitafakari na Kujiuliza maswali ambayo yatakuwa na matokeo mazuri na yaliyo ya muda mrefu katika kutatua matatizo yote tunayo yapitia,
Pia ni muhimu kutambua kuwa kila hatua tunayo pitia kwenye maisha yetu imechangiwa na sisi wenyewe kwa asilimia 100% na hivyo iwapo tumechoshwa na hali hiyo uwezo wa kujitoa kwenye Ugumu huo upo ndani yetu wenyewe.

Hivyo rafiki unapo jikuta kwenye hali yoyote isiyo nzuri kwako ni muhimu kujipa muda mzuri wa kujitafakari na kutafakari kwa kina uhusika weka katika ugumu huo kisha kuchukua hatua ya kuondokana na ugumu huo,
Uwapo katika hatua hii ya kutatua tatizo hilo usitumie njia zitakazo kuwa rahisi na zenye matokeo ya muda mfupi badala yake tumia njia sahihi ambayo itakupa matokeo bora na yatakayo dumu zaidi.

Usiendelee kuchimba shimo ujikutapo shimoni badala yake weka mkakati utakao kutoa shimoni.

Kila la kheri rafiki yangu na Mwanamafanikio mwengungu.
Kwa ushauri na maoni nitafuta moja kwa moja 0715222989 WhatsApp/errynine6@gmail.com

Pia unaweza kutuma ujumbe mfupi BIG KEY OF SUCCESSFULL2017 kwenda namna 0715222989 ili uweze kuunganishwa na kundi la WhatsApp BURE.

Karibu sana.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top