Habari rafiki na Mwanamafanikio mwenzangu kupitia Mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Ni imani yangu kuwa ni mzima wa afya njema zaidi unaendelea kupambana zaidi ikiwa ni pamoja na kuweka juhudi kubwa ili kuweza kufikia mafanikio makubwa kupitia kazi,biashara Au ajira Unayo fanya.
Ikiwa ni siku nyingine nzuri sana kwetu hii ni Fursa ya pekee kwetu kwenda kuweka Umakini na Juhudi kubwa zaidi ili kuweza kuitumia siku hii vizuri zaidi kwa kuweka alama ya uwepo wa uzima wetu.
Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwa moyo mkunjufu ambapo leo Mimi rafiki yako nitakwenda kukushirikisha mambo mawili muhimu ya kuzingatia juu ya kipato chetu ili tuweze kufikia Utajiri na Uhuru wa kifedha,
Karibu sana rafiki tuongozane mpaka mwisho wa somo letu ambapo ninaamini itakuwa umejifunza kitu cha kwenda kufanyia kazi ili kuweza kufikia uhuru wa kifedha.
Nianze kwa kuku uliza swali hili,
Je kwanini mpaka sasa wewe sio Tajiri?
Siku chache nilikuwa nasoma kitabu cha KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIO TAJIRI ambapo baada ya kumaliza kitabu hiki niliona kosa kubwa sana ambalo limekuwa likinizuia mimi kufanikiwa na hivyo nikaweka mkakati mzuri utakao ni wezesha mimi kuwa tajiri.
Ni mambo madogo madogo ambayo tunayafanya kila siku na kwa kuwa hayana madhara ya haraka basi Tumekuwa tukiendelea kuyafanya kila siku na baadae kujikuta kwenye dimbwi kubwa la umaskini na hata kushindwa kujitoa kwenye dimbwi hili la Umasikini,
Mambo hayo yote yamejikita kwenye mambo haya mawili nitakayo kushirikisha kwa siku hii ya leo kuelekea utajiri na uhuru wa Kifedha.
Mambo haya ni MAPATO NA MATUMIZI,
Tofauti kubwa na kizuizi kikubwa cha watu wengi kuto fikia malengo yao ya kifedha ipo hapa kwenye mapato na matumizi,
Mapato na matumizi ndio mtihani mkubwa kwa watu wengi na kutokana kwa watu hao kuwa na mpangilio mzuri wa kipato chao na matimizi basi imekuwa vigumu sana kwa watu wengi kufanikiwa.
MAPATO,Hii ni fedha unayo tengeneza kutoka kwenye shughuli zako mbalimbali Mfano:Kazi,Ajira au Biashara unayo fanya,
Mapato ni eneo la kwanza na muhimu sana kwetu sote katika kufikia Utajiri na Uhuru wa kifedha.
Hutuwezi kufikia mafanikio ya aina yoyote pasipo kuwa na Mapato,Ili kuweza kufikia Utajiri na Uhuru wa kifedha ni muhimu sana eneo hili la mapato kuwa na Uzalishaji mkubwa kwetu ingawa ni muhimu kuanza na kipato tulicho nacho.
MATUMIZI,
Hili ni eneo la pili baada ya kuwa tayari na mapato sasa ni muhimu kutambua fedha zetu wapi zina kwenda,
Matumizi ni vitu vyote vinavyo chukua fedha zetu Mfano:Mahitaji muhimu ya maisha yetu na hata mahitaji mengine yasiyo ya lazima lakini ni muhimu Eg Chakula,Malazi,Mavazi n.k
Ili kuweza kufikia Utajiri na Uhuru wa kifedha ni Muhimu sana kuzingatia na kuangalia vitu vyote vinavyo chukua fedha zetu,
Hii ni kwa sababu kila mtu anatengeneza kipato lakini ni vitu gani vina chukua kipato chake hapo kila mtu ni juu yake.
Haya ndiyo mambo mawili makubwa tunayo takiwa kuyazingatia katika kufikia utajiri na uhuru wa kifedha,
Katika tulivyo pata maana tofauti za mambo hayo mawili na kwamba MAPATO ni fedha unayo zalisha na MATUMIZI ni vitu vyote vinavyo chukua fedha zetu.
Ili kuweza kufikia Utajiri na Uhuru wa Kifedha ni muhimu sana kuwa na mapato makubwa lakini bado sio kigezo kikubwa cha sisi kufikia Utajiri bali Utajiri wetu unatokana na Matumizi ya kipato chetu,
Ili tuweze kufikia Utajiri na Uhuru wa kifedha ni Muhimu zaidi kuwa na Mapato makubwa zaidi Huku tukipunguza Matumizi.
Matumizi ya kipato chetu kamwe haya takiwi kuwa makubwa kuliko kipato tunacho zalisha na kama itakuwa hivyo basi hatuwezi Kufikia Utajiri na Uhuru wa kifedha,
Matumizi yetu ndio yanayo yanayo pima Utajiri wetu.
Ili tuweze kufikia Mafanikio makubwa ni muhimu zaidi kuwa na Mapato makubwa huku tukipunguza matumizi yetu na Kuwa madogo zaidi,
Ikiwa unakuwa na matumizi yanayo zidi ukubwa wa mapato yako basi ni muhimu kuangalia mpangilio wa matumizi yako na kisha kuondoa matumizi yote yasiyo muhimu kwako.
Daima mapato yako yanatakiwa kuwa makubwa zaidi kuliko kuliko matumizi yako kwa njia hii inakuwa rahisi kwako kupiga hatua kubwa kuelekea Utajiri na Uhuru wa kifedha,
Rafiki hauto weza kupiga hatua kubwa kifedha ikiwa matumizi yako yatakuwa makubwa zaidi kuliko mapato.
Pia kila siku kazina kuongeza mapato huku ukipunguza matumizi yako zaidi.
Kila la kheri rafiki yangu na nikutakie Mafanikio mema,
Kwa maoni na Ushauri Andika maoni kwenye sanduku la maoni hapo chini au Tuma ujumbe WhatsApp kwenda 0715222989 au errynine6@gmail.com.
Karibu sana rafiki yangu na Wako rafiki
Ernest Lwilla
Chapisha Maoni