KHERI YA KUZALIWA KWANGU!
Desember 23,Siku ya Jumanne saa 10:Usiku Mwaka 1992 katika hospitali ya Ikonda hapo ndipo nilipo zaliwa mimi nikiwa kijana wa kwanza kwa Baba na Mama Yangu.
Sifa na Utukufu kwa Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na Nchi,ambae pia ndio muumba wa kila kilicho hai Ulimwenguni pote,Ahsante sana Wazazi wangu,Ndugu,rafiki na jamaa pia,
Tangu Mwaka 1992 mpaka sasa nimesha kuwa na watu tofauti tofauti kwa vipindi tofautitofauti na kwa mazingira tofauti tofauti tukishirikiana katika majukumu tofauti tofauti Ahsanteni sana kila mmoja ana nafasi na mchango mkubwa sana wa mimi kufikia hapa.
Kwa siku hii ya leo ambayo ni maalum kwangu,
Napenda kukushirikisha mambo machache (3) ambayo nitapenda kila mmoja wetu aweze kuyatafakari kwa nafasi ya pumzi yake kwa siku hii ya leo.
Hii ikiwa na maana ya kwamba kila kiumbe kilicho hai maisha yake yana nafasi kubwa kwa kiumbe kingine kujifunza ikiwa kiumbe hicho kitaamua kushirikisha jambo hilo,
Hivyo pia Ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu binadamu kwenye kila siku tunayo pewa nafasi ya kuwa hai.
Karibu sana Rafiki yangu nikushirikishe mambo haya matatu na tuweze kujifunza sote.
Jambo la kwanza KILA PUMZI NI NAFASI MPYA YA MAPAMBANO,
Tangu tunapo zaliwa siku ya kwanza tunasajiliwa rasmi kwenye vita ya mapambano dhidi ya matumizi ya uhai tulio pewa,Ambapo tangu siku ya kwanza tunaziishi changamoto kila siku na kadri tunavyo zishinda changamoto hizo ndivyo tunavyo zidi kukua na Umri wetu kuongezeka zaidi.
Kila kiumbe hususani binadamu tunafanya mambo mengi sana kila siku ya uhai wetu kwanzia utoto wetu mpaka sasa,Mambo mengi tunayo pata mala nyingi hupelekea maumivu makubwa lakini bado kesho yake Unalazimika kuchukua hatua ya kufanya jambo jingine litakalo kupa changamoto na maumivu na unapo yashinda ndivyo unavyo pewa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai.
Maisha yetu yanakamilika kwa kufanya mambo mengi sana yanayo tupa neema,maumivu,changamoto n.k lakini matokeo hao huwa ni kichocheo cha sisi kuendelea kuishi,
Ni mambo mangapi umejifunza na kufanya kwa vitendo tangu ulipo zaliwa?
Ni mambo mangapi yalikupa matokeo uliyo yataka?
Ni mambo mangapi yalikupa Maumivu makubwa?
Ni mambo mangapi yalikughalimu mpaka ukajuta?
Lakini matokeo hayo ndiyo mwisho wa kufanya? Bila shaka ni HAPANA.
Hii inamaana kila siku,Kila sekunde,Kila dakika ni nafasi nyingine ya mapambano pasipo kujali ni jambo jipya au ni jambo ulilo zoea kulifanya,Litakupa Neema au Maumivu lakini ili upate nafasi ya uhai wa kuishi kesho ni lazima ufanye leo.
Hivyo rafiki yangu kila siku ni Nafasi ya kuishinda kwa kufanya jambo jingine pasipo kuangalia jana yake lakini Matokeo bora ya leo yatategemea matokeo yako ya jana iwapo ulishinda utapata hamasa ya kufanya jambo jingine leo,Iwapo ulishindwa utapata fundisho la kuiendea leo kwa mafanikio.
Usiogope kushindwa wala usiogope kupoteza kwa sababu ndio tafsiri ya maisha Ukipata leo,Jua kesho waweza kukosa lakini ni lazima ufanye.
Jambo la pili ISHI MISINGI YA NIDHAMU UANDILIFU NA KUJITUMA,
Mafanikio ya jambo lolote linategemea mtendaji wa jambo hisika na Namna alivyo lifanya ya weza kuwa ni kwa njia sahihi au kwa njia zisizo sahihi na amefikia hatua aliyo panga kufikia,
Msingi wa Nidhamu,Uandilifu na Kujituma ni msingi nilio jifunza ukubwani na nimsingi ninao weka juhudi kuishi kila siku na sio rahisi lakini msingi huu ningeujua au kufundishwa tangu nikiwa mdogo basi ningekuwa na maumivu lakini yenye msaada katika kupiga hatua kuelekea mafanikio makubwa.
Kila kitu tunacho fanya kinategemea sana NIDHAMU ya kukifanya kitu hicho kila tunapo panga kufanya,Nidhamu pekee ndiyo inayo kuongoza kufanya pasipo kuahirisha jambo ulilo panga kufanya.
UADILIFU kila jambo ili tulifanye kwa mafanikio linahitaji kulifanya kwa uadilifu yaani kwa usahihi pasipo kujali kuna watu wanao tuona au kuto onekana,
KUJITUMA hakuna jambo lolote kwenye maisha utakalo fanya pasipo kujituma alafu likakupa matokeo yaliyo bora hivyo ni kwa kujituma pekee ndipo una weza kupiga hatua kubwa sana.
Kwa watu wote walio ishi kwa misingi hii mitatu tangu wakiwa watoto bila shaka maisha yao hayapo sawa na wengine.
Hivyo ningependa kukushirikisha rafiki yangu kama ambavyo nimejifunza na kunufaika mimi nawe uweze kunufaika na misingi hii ya Nidhamu,Uadilifu na Kujituma.
Fanya kila jambo unalo kuwa umepanga kufanya,Fanya kila jambo kwa usahihi,Fanya kila jambo kwa kwenda hatua ya ziada.
Jambo la tatu ni MTAJI WA UAMINIFU NI ZAIDI YA FEDHA,
Kama kuna vitu vinavyo walipa watu wote wanao pambana dhidi ya wao kuwa hai ili waweza kuzishinda changamoto na kuwa washindi kwenye maisha yao basi UAMINIFU ni Ufunguo mkubwa sana kwa maisha ya mafanikio katika jambo lolote unalo fanya,Iwe ni kazi,biashara,ajira nk vyote vina hitaji uaminifu.
Uaminifu ndio mtaji namba moja na mkubwa katika kufanya jambo lolote kwenye maisha,
Biashara inahitaji uaminifu ndipo uweze kuifanya kwa mafanikio,Kazi pia inahitaji uaminfu,Ajira pia inahitaji uaminifu ili uweze kuifanya kwa mafanikio.
Ikiwa unafanya biashara Au kutoa huduma yoyote upo wakati fedha inaweza kukuangusha kabisa kabiasa lakini uaminifu hauwezi kukuangusha hata kwa sekunde moja,
Fedha inatafutwa lakini uaminifu ndio maisha yetu yanatakiwa kujengwa hapo.
Wafanya biashara wote wakubwa wanaongozwa na kutawala kwa Uaminfu hivyo Auminifu unalipa zaidi kuliko kitu chochote.
Hivyo rafiki nikusii sana kuwa mwamifu kwenye kila eneo la maisha yao,UAMINIFU unalipa Sana tena Sana.
Niwatakie siku njema na yenye mafanikio makubwa sana.
Kila la kheri rafiki yangu
Na wako rafiki
Ernest Lwilla
Contact:0715222989/errynine6@gmail.com
Fb:Ufunguo Wa Mafanikio
www.ufunguowamafanikio.blogspot.com
Chapisha Maoni