Unknown Unknown Author
Title: Salamu Zangu Za Kufunga Mwaka 2017 Na Kufungua Mwaka 2018 Kwako Rafiki Yangu.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Salamu zangu kwako rafiki yangu! Hatari rafiki na Msomaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio? Hongera sana rafiki kwa kuendelea kuweka...

Salamu zangu kwako rafiki yangu!

Hatari rafiki na Msomaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio?

Hongera sana rafiki kwa kuendelea kuweka juhudi kubwa zaidi kwa mwaka huu unao kwisha ambapo nina hakika yapo mambo mengi sana uliyo kwenda kufanya kwa mwaka huu 2017,
Yapo mambo uliyo fanya kwa ubora mkubwa na kwa kuweka juhudi na tumaini kubwa lakini huku pata matokeo bora ambayo ndiyo uliyo tegemea kupata,
Pia yapo mambo uliyo fanya kwa ukawaida na Ulishinda au kushindwa yote tunapaswa kujipongeza na kuona hii ni Fursa ya pekee kwako kwenda kuweka juhudi kubwa kwa 2018.

Nimekuwa na Kipindi bora sana kwangu kimafanikio na kujifunza tangu ulipo anza mwaka 2017,
Nimekutana na watu wengi sana na wa ghalama kubwa sana kwenye safari yangu ya mafanikio 2017,Nimefanya mambo mengi sana ambayo ni mazuri kwangu na kwa wengine,Yapo mambo niliyo fanikiwa na niliyo shindwa.
Pia nimekuwa na kipindi kigumu sana kwa nyakati fulani na niliendelea kuweka juhudi na kufanya kila hatua ni hatua ya kujifunza kwangu.

Katika hatua zote nilizo pitia na kuzifanya mwaka mzima wa 2017,
Nitachukua  nafasi ya kukushirikisha mambo kadhaa ambayo kwangu yamekuwa msaada mkubwa na ikiwa ni sehemu ya mafanikio makubwa niliyo vuna kwenye mwaka 2017.

1.2017 IMENIFUNDISHA KUONGEZA JUHUDI KWENYE KAZI NA BIASHARA ZOTE NILIZO FANYA,
Kwa kipindi kirefu nimekuwa nafanya kazi na biashara lakini siku wai kufanya kwa kiwango kikubwa sana,
Nilifanya kazi na biashara kwa ukawaida na hivyo iliniwezesha kuishi maisha yaliyo ya kawaida sana na muda mwingine sikuwa na utulivu katika shughuli zote nilizo fanya daima nilikuwa ni mtu wa kukimbizana na kila fursa iliyo onekana kuwa na mafanikio ya haraka,
2017 Imenifundisha mengi Sana ikiwa ni pamoja na kutambua kuwa hakuna mafanikio ya haraka kwenye maisha.

Hivyo nimetambua kuweka muda kwenye kazi,Kuweka uvumilivu kwenye kazi,Kuweka nidhamu kwenye kazi,Kujituma kwenye kazi na hata eneo lolote la maisha yangu na hii kuwa ndio nguzo kuu ya kufikia mafanikio makubwa hakuna njia ya mkato kwenye mafanikio na kwa kipindi cha mwaka mmoja tayari nimesha anza kuona matokeo yaliyo makubwa.

2.2017 IMENIFUNDISHA KUTOA GHALAMA KWENYE HATUA ZA KUJIFUNZA NA KUFANYA KWA VITENDO,
Hakuna hatua mtu anayo weza kufanikiwa bila kutoa ghalama yoyote kwa njia ya kujifunza na hata kufanya kwa vitendo,
Iwapo utatoa ghalama kubwa kuweza kujifunza itakuwa ni hatua nzuri lakini Ghalama kubwa zaidi ipo kwenye kufanya kwa vitendo.

Nimeudhuria semina nyingi nzuri na kubwa kwa mwaka 2017 ambapo maisha yangu yote siku wai kutoa ghalama kwenye kujifunza na sikujua kuwa ni muhimu kujifunza,Zipo semina nilizo toa ghalama na zipo semina nilizo udhuria bure,
Lakini bado haikuwa tiketi ya mimi kufikia mafanikio moja kwa moja na hivyo nililazimika kutoa ghalama kubwa zaidi kwenye kufanya kwa vitendo.

Hatua hizi zote zimekuwa na matokeo makubwa sana kwangu kwa 2017.

3.2017 IMENIFUNDISHA KUSOMA VITABU/NA KUSHIRIKISHA WENGINE.
Maisha yangu yote siku wai kununua vitabu,Maisha yangu yote sija wai kusoma kitabu na kukimaliza lakini 2017 nimesoma vitabu na makala nyingi sana.

Tangu nilipo maliza masomo yangu sijawai kufikiria kuwa kuna kusoma vitabu,Makala na video za hamasa lakini 2017 Nimeweza kufanya hayo yote ambapo nilijifunza mambo mengi sana na kwenda kuyafanyia kazi kwa juhudi zilizo niwezesha kupiga hatua kubwa.

Iwapo utasikiliza maneno na swaga za mitaa kwa watu walio kubali kushindwa basi utaona na kusikia kuwa wanao fanikiwa wote ni FREEMASON na hicho ndicho utakacho kijua pekee,
Lakini watu hawa wanao fanikiwa kwa kiwango kikubwa bado wanapenda watu wote wafanikiwe kama walivyo fanikiwa wao na hivyo kutenga muda wao na kuandika vitabu,kuandaa audio na video za hamasa ili kuweza kuwafikia watu wengi na waweze kujifunza kupitia wao lakini Zoezi gumu lipo kwa watu wasio fanikiwa hawana mafanikio na hawana muda wa kujifunza.

Ufunguo mkuu wa mafanikio upo katika kujifunza na kufanya kwa vitendo.

4.2017 IMENIPA KOCHA WA MAFANIKIO/WASHAURI CHANYA WA MAFANIKIO,
Licha ya kutumia muda mwingi katika kujifunza na kufanya kwa vitendo bado mambo haya kuwa rahisi kwangu,
Ambapo changamoto kubwa ilikuwa ni kushindwa kujisimamia kwenye mambo muhimu niliyo panga kufanya hivyo kwa kuwa na Kocha wa mafanikio nilipata muda mzuri wa kushauriana nae kwa karibu sana na hata kuweka mipango ya pamoja na kuitekeleza kwa pamoja.

Yapo mambo ambayo pekee yako hayawezi kwenda kwa namna yoyote,
Hivyo kwa kuwa na Kocha basi inakuwa rahisi kuhamasika na kuendelea kuweka juhudi kubwa.

80% ya maisha kwa ujumla wake yamezungukwa na uwepo wa changamoto hivyo ili uweze kuzipita changamoto ni lazima uwe na mtizamo chanya na uwe na watu ambao unakuwa unashauriana nao kwa karibu hasa unapo kuwa unakwama.
Hii ni kwa sababu upo wakati akili inakuwa haina uwezo mkubwa wa kufikiri zaidi lakini unapo msirikisha mtu mwingine anakupa njia sahihi ya kuzipita changamoto zako.

Kocha na Washauri chanya ni muhimu sana kwenye maisha ya mafanikio ya mtu yeyote hasa kwa wanao tafuta kupiga hatua kubwa sana kwenye maisha yao.

5.2017 IMENIFUNDISHA KUITUMIA FEDHA NA KUWA MFANYA KAZI WANGU KWENYE MAENEO MBALIMBALI YA MAISHA YANGU,
Kwa mwaka 2017 nimejifunza uwekezaji kwa undani na kuanza kuwekeza kwenye baadhi ya maeneo,Nimejifundisha njia sahihi za kufanya fedha ifanye kazi pasipo mimi kuwepo moja kwa moja,Nimejifunza msingi mkuu wa kuongeza zaidi fedha na usimamizi wa fedha kwa ujumla.
Fedha ni mfanya kazi mzuri anaye weza kufanya kazi kubwa ndani ya mda mfupi pasipo kuhitaji muda wako moja kwa moja hata kama ni fedha ndogo kiasi gani.

Ukweli huwezi kufikia mafanikio makubwa kwa wewe kufanya kazi moja kwa moja pekee yako,
Huwezi kuisha maisha yenye uhuru wa kipato kwa kuwa na mkondo mmoja pekee wa kuzalisha kipato chako ni lazima uweze kutumia fedha za watu wengine,Muda wa watu wengine ili kuweza kupiga hatua kubwa na kufikia uhuru wa kifedha.

Yapo mambo mengi niliyo weza kufanya kwa mwaka mzima wa 2017,
Yapo mambo mengi niliyo weza kujifunza kwa mwaka 2017 lakini hayo yote siku yafanya peke yangu.
Wapo watu wengi walio niwezesha mimi kupiga hatua kwenye kila eneO nililo weka nguvu zangu.
Nambua wazi kwamba wapo watu wengi waliweze kuweka mipango yao mkubwa kwa mwaka huu 2017 lakini haikuwezekana kwa changamoto mbalimbali na matatizo mengi yaliyo kuwa nje ya uwezo wao.

2018.
Nitachukua jukumu zito la kuwawezesha watu wengine kupiga hatua kwa kuwasimamia kwa ukaribu zaidi kwa mwaka huo ili nao waweza kufikia hatua kubwa za mafanikio katika maisha yao,
Ambapo kwa mwaka 2018 nitakwenda kutengeneza timu nzuri ya watu wanao fanya kwa vitendo na kuwasimimia kama ambavyo nimekuwa nikisimamiwa mimi mpaka kupiga hatua na hivyo nitafanya hivyo kwa watu wengine watakao kuwa tayari.

Nitachukua muda wangu na kuwafundisha mambo mengi kuhusiana na maisha ya mafanikio n.k

Hivyo nikukaribishe rafiki yangu  nawe uwe ni miongoni wa watu hao wachache nitakao kwenda nao mwaka 2018 ili tuweze kupiga hatua pamoja.

Nikutakie siku njema na yenye mafanikio mkubwa sana.
KARIBU 2018 NIPE NAFASI NIWE KOCHA WAKO KWA MWAKA 2018 ILI TUPIGE HATUA PAMOJA.

Na wako rafiki katika mafanikio.
Ernest Lwilla.
Contact 0715222989/errynine6@gmail.com
Website;www.ufunguowamafanikio.blogspot.com
Karibu.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top