Habari rafiki yangu?
Hongera kwa nafasi hii nzuri sana,Ambapo umeweza kuuanza mwaka 2018.
Ni nafasi nyingine kubwa na yapekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupiga hatua kubwa.
Ikiwa ni siku ya kwanza ya mwaka 2018 mimi rafiki yako nimekuandalia mambo mawili muhimu sana unayo paswa kuzingatia kwa 2018 ili ukawe mwaka wa mafanikio makubwa kwako.
Watu wengi wamekuwa wakiutumia muda wao wa mwanzo wa mwaka kama hamasa ya wao kuweka malengo na mipango mizuri ya mwaka mzima hii inatokana na hamasa kubwa ambayo watu wanakuwa nayo baada ya kuuanza mwaka mpya,
Lakini baada malengo na mipango hiyo wengi hushindwa kufikia baada ya kukutana na changamoto nyingi ambazo hazikuwepo wakati wa mipango yao ya mwanzo wa mwaka na hivyo kujikuta kuhamishia malengo hayo kwenye mwaka unao kuja jambo ambalo huwa sio rahisi kabisa kufanikiwa.
Zingatia mambo haya mawili ili mwka 2018 kuwa wa mafanikio makubwa ukilinganisha na miaka mingine yote ambayo ulipata nafasi ya kuwa hai na huku fanya yale yaliyo muhimu na kuweza kupiga hatua kubwa.
1.Kuwa Na Maono Na Ndoto Kubwa Kwa 2018 Na Maisha Yako Kwa Ujumla,
Maisha ya mafanikio ni zaidi ya kufanya kazi au biashara,kupata fedha,kutumia na kwenda kukopa na kisha kufanya kazi tena, kupata fedha tena na kwenda kulipa madeni n.k
Ili 2018 uwe mwaka wa tofauti na wenye mafanikio makubwa kwako ni lazima uwe na sababu kubwa ya wewe Kuamka mapema kila siku,Kuweka juhudi kila siku kwenye kila jambo na kujifunza kila siku n.k sababu hiyo ni Maono na Ndoto ya wewe kuwa hai 2018.
Ni lazima uwe na jambo kubwa linalo kupa hasira kubwa ya kuendelea kuweka juhudi kubwa sana.
Na kama tayari una maono na ndoto kubwa ya maisha yako basi jikumbushe kwa kina ukubwa na upana wa ndoto yako kisha anza mwaka wako kwa hamasa kubwa ya kuweka juhudi kubwa zaidi ili mwaka 2018 kuwa wa mafanikio makubwa kwako.
2.Ishi Misingi,
Hakuna ukuta imara unao weza kusimama pasipo msingi imara na kama itakuwa hivyo basi hauta kuwa ukuta imara bali utakuwa ni ukuta wa hovyo na Utakuwa rahisi sana kuangushwa kwa chochote,
Msingi imara ndio utakao kupa ushindi mkubwa kwa mwaka 2018.
Kama unavyo jua tunaishi kwenye dunia yenye kila aina ya kelele,Kila aina ya fursa,Kila aina ya habari na hivyo vyote vina weza kukuangusha kirahisi kufikia maono na ndoto yako kwa mwaka 2018 na hata maisha yako yote.
Binafsi tangu 2017 nimekuwa nikiishi msingi wa maisha ya mafanikio ambao ni NIDHAMU,UADILIFU NA KUJITUMA kwa kuishi msingi huu Nimeweza kupiga hatua kubwa sana kwa sababu Daima ninafanya Nilicho panga kufanya kila siku pasipo kuahirisha,Ninafanya kitu sahihi kila siku kwa wakati sahihi kwa sababu usipo fanya vitu sahihi ni rahisi sana kuangushwa na vitu hivyo,Licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi sana lakini bado nimekuwa nikienda hatua ya ziada zaidi kila siku na kupata matokeo yaliyo makubwa zaidi,
Hivyo nawe rafiki yangu unaweza kuishi msingi huu wa maisha ya mafanikio.
Pia mwishoni mwamwaka 2017 nimeanza kuishi na kujifunza falsafa ya ustoa ambapo imekuwa ikinipa maisha bora kwa kuishi mambo kwa uasili zaidi ambapo tayari nimeondokana na vitu kama tamaa ya vitu,kuishi wakati nilio nao,Kuishi vitu nilivyo navyo n.k hii inakuwa inanipa furaha wakati wote.
Kwa kuweza kuzingatia mambo hayo mawili nina hakika mwaka huu 2018 utakuwa na mafanikio makubwa sana kwako rafiki yangu .
Kama nilivyo weza kukushirikisha Mwaka 2017 kuwa Mwaka 2018 nitahitaji kuwa na kundi la watu wachache wanao jifunza na kufanyia kazi ya wanayo jifunza kwa vitendo.
Lakini pia nitatumia nafasi hiyo kuwa kama kiongozi kwa watu hao wachache kukahakiksiha nawasimamia kwa ukaribu sana na kuhakikisha wanapiga hatua kubwa sana kwenye maisha yao kwa mwaka 2018.
Iwapo utakuwa ni miongoni mwa watu watakao Penda kufanya kazi nami kwa ukaribu kwa mwaka 2018,
Basi wasiliana nami moja kwa moja kwa kupita WhatsApp number 0715222989 ili kupata mwongozo na utaratibu wake.
Nikutakie kila la kheri rafiki yangu ili mwaka 2018 ukawe na mafanikio makubwa kwako.
Na wako rafiki katika mafanikio
Ernest Lwilla
Contact:0715222989/errynine6@gmail.com
Chapisha Maoni